escrow one
JF-Expert Member
- Nov 29, 2014
- 1,473
- 2,868
Leo ikiwa ni Wiki ya Pili ya Tamko la Maaskofu kusomwa Makanisa yote ya Roman Catholic, nimevutiwa na Maneno aliyoyaongea Paroko mmoja kwenye Ibada " Tusikae kimya sasa kusubiri miaka 10 ijayo Rais wetu aandike Kitabu cha kujutia kuingia mkataba huu mbovu wa Bandari, tumkosoe mapema ili akija kuandika kitabu hicho aseme nilishauriwa ila nilikataa Ushauri"
Amenukuu Maneno yaliyopo kwenye Kitabu cha "My Life, My Purpose" cha Hayati Benjamin Mkapa alipojutia mambo mbalimbali ya Ovyo aliyoyafanya wakati wa Utawala wake ikiwemo kashfa maarufu ya EPA "Wahuni walitumia uaminifu wangu kwa chama kunishawishi nikubali Ninajisikia kuwa nilitumika na kusalitiwa..."
"Kama Wahuni waliweza kumlaghai Rais Mkapa kuingia Mikataba ya ajabu basi hawawezi kushindwa kumlaghai Rais Samia kwamba Mkataba huu una tija"
SAUTI YA WENGI NI SAUTI YA MUNGU