PART 1: Hawa hapa watu wanaomchukia na kuchukia utawala wa Rais Samia

PART 1: Hawa hapa watu wanaomchukia na kuchukia utawala wa Rais Samia

msovero

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2019
Posts
863
Reaction score
1,534
Katika siasa ni kawaida kabisa kila Rais anayeingia madarakani kukubalika ama kutokukubalika na makundi mbali mbali ya watu.

Kadhalika, Rais anapokuwepo madarakani huwa na mema yake na madhaifu yake pia, na huu ndio msingi wa kukubalika au kutokubalika kwake kwa wananchi anaowaongoza kulingana na kila mmoja anavyogusa na utawala wake.

Haya hapa ni makundi mbali mbali yanayoonyesha kuridhishwa ama kutoridhishwa na utendaji wa Rais wa awamu ya sita, Mh. Samia Suluhu Hassan 'chief hangaya' chifu wa machifu wote Tanzania.

Kwa mujibu wa utafiti mdogo niliofanya kwa takribani miezi miwili iliyopita kupitia watu mbali mbali, nimebaini kuwa haya ndio makundi ya watu wasioridhishwa na utendaji kazi wa Rais Samia.

1. WATU WALIOKATA TAMAA YA MAISHA
Hili kundi linahusisha watu wenye kipato duni wanaoishi katika umaskini wa hali ya chini kabisa 'absolute poverty'. Hawa wengi wao wameshajikatia tamaa ya maisha na kufikiri kwamba maisha waliyonayo hayawezi kubadilika kwa chochote. Hivyo furaha yao ni kuona matajiri wananyanyasika kama ilivyokuwa katika utawala uliopita kwa kuamini kuwa matajiri wakinyanyasika na kuchukuliwa mali zao kwa nguvu kutawaletea ahueni ya maisha kumbe sivyo. na hivyo kundi hili litaendelea kumchukia Rais Samia hadi pale atakapobadili aina ya uongozi na kuanza kuwanyanyasa matajiri kama alivyokuwa anafanya mtangulizi wake, hayati magufuli.

2. WATU WENYE ROHO MBAYA NA WACHAWI
wote tunafahamu kuwa 'mchawi' ni mtu asiyependa maendeleo wala hapendi kuona binadamu mwenzie akifanikiwa au akipiga hatua ya kimaisha.

Kundi hili wakati wa hayati magufuli lilifurahi sana kuona watu wakitahabika na kupitia maisha magumu kwani hayati magufuli alijipambanua zaidi kwenye maendeleo ya vitu na sio maendeleo ya watu. Kwahiyo matamanio ya kundi hili ni kuona Rais aliyepo sasa kujikita zaidi kufanya maendeleo ya vitu na sio kuwekeza kwenye maendeleo ya watu ambapo kutafanya watu kuishi maisha mazuri yenye amani na furaha kama ilivyodhamira ya Rais Samia. Hivyo kundi hili si tu linamchukia Rais Samia bali linachukia hata kusikia habari ya nyongeza ya mishahara kwa watumishi wa umma kwani wanaamini kwa kuongezewa kwao mshahara kutawafanya wainuke kiuchumi huku hali zao zikiendelea kubaki duni.

3. VIJANA WALIOFELI AMA KUACHA SHULE
Hapa nikiri wazi kwamba hakuna kipindi vijana wasomi waliomaliza vyuo hapa nchini wamedharaulika kama kipindi cha hayati magufuli. Kudharaulika kwa vijana wasomi hawa kulitokana na sera mbovu au msimamo wa hayati magufuli kushindwa kuwaajiri pindi wamalizapo vyuo hivyo kuwafanya wazagae mtaani bila kazi huku wakisimangwa na kudharauliwa na hili kundi la vijana ambao waliacha ama walifeli shule.

Kundi hili mkombozi wao alikuwa magufuli kwani alikuwa hatoi ajira kwa vijana wahitimu wa vyuo hapa nchini hivyo kitendo hicho kiliwafurahisha sana hili kundi la wasio soma kwani wanaamini kama ajira hazitolewi basi kutawafanya walingane ama kuwazidi waliosoma hasa kwenye nyanja ya kiuchumi. Hivyo basi, kundi hili linamchukia Rais Samia kwani ameanza kuonyesha dalili za kutoa vibali vya ajira jambo ambalo ni chukizo kwa kundi hili.

4. WANASIASA WENYE UCHU WA MADARAKA
Hili ni kundi la wanasiasa waliokuwa wanufaika wa utawala wa hayati magufuli na wale waliokuwa wanajipanga kuwania kiti cha urais 2025 kwani ujio wa Rais Samia madarakani ni kama umevuruga mipango yao hivyo wanafanya kila hila na ghiriba kwa kupandikiza na kueneza chuki kwa wananchi wa makundi tajwa hapo juu ili Rais Samia aonekane hafai kumbe lengo lao kuu likiwa ni kurudisha 'regime' yao.

5. WAFUASI WA VYAMA WENYE MIHEMKO YA KISIASA
Hapa nazungumzia makundi ya vyama vyote kikiwemo chama cha mapinduzi na vyama vya upinzani.

Tukianza na wanachama wenye mihemko ya kisiasa kutoka chama cha mapinduzi(CCM). Hawa wanaamini nchi haiwezi kuendelea pasipo uwepo wa CCM, hivyo 'upinzani' kwao ni chukizo kubwa na wanatamani wapinzani wapitie mabaya ikibidi hata kuuawa kama ilivyokuwa katika utawala uliopita. Kwakuwa haya hayajaanza kuonekana basi kundi hili kwa sasa linamchukia Rais Samia na kuona ni bora angekuwepo hayati magufuli.

Tukirudi kwa wafuasi wa vyama vya upinzani wenye mihemko ya kisiasa. Hawa hawaambiliki kwani wanaamini adui wa maendeleo katika taifa hili ni CCM hivyo kila Rais anayetokana na chama hicho haijarishi ni mzuri au mbaya wao ni kukosoa na kumpinga tu. Hata hivyo katika utafiti wangu nimebaini kuwa kundi hili la wafuasi wa vyama vya upinzani halitoacha kumpinga kwani linatimiza wajibu wake wa kisiasa katika kutafuta madaraka ya kutwaa dola, hivyo Rais Samia ajipange zaidi kuwaletea wananchi maendeleo ili kuzima hoja za kundi hili.

Itaendelea....
 
Katika siasa ni kawaida kabisa kila Rais anayeingia madarakani kukubalika ama kutokukubalika na makundi mbali mbali ya watu.

Kadhalika, Rais anapokuwepo madarakani huwa na mema yake na madhaifu yake pia, na huu ndio msingi wa kukubalika au kutokubalika kwake kwa wananchi anaowaongoza kulingana na kila mmoja anavyogusa na utawala wake...
Baada ya kupata kiajira cha ualimu unaanza kuwa mshenzi na kudharau wenzako?
 
Tukutane kwenye part II
Kama hujaanza kundi ambalo linazo kila sababu ya kuchukia( walionyimwa ajira,machinga,walioporwa haki zao na baadhi ya viongozi nk) hiyo part 2 yako haitakua na mvuto
 
Back
Top Bottom