Pasaka ni sikukuu kubwa kuliko Krismasi - Ikulu ya Marekani yaandaa sherehe nzito!

Pasaka ni sikukuu kubwa kuliko Krismasi - Ikulu ya Marekani yaandaa sherehe nzito!

Huo ni mtazamo wao, haukulazimishi nawe kuiona kuwa sikukuu kubwa
Hujasoma post #2.
Nimeeleza kwanini Pasaka ni sikukuu kubwa. Na huu uzi lengo langu ni kusisitiza kuwa Pasaka ni sikukuu kubwa. Yesu asingefufuka, imani yetu ingekuwa bure. Lakini sasa Jesus is alive! Haleluya! Ndio sababu hata "Rais wa dunia" anaandaa "dinner" ya nguvu 🙂
 
Marekani pasaka wala sio public holiday, kazi kama kawa! Hiyo sherehe nzito umeionea online? Au umehadithiwa?
kwani public holiday watu hukatazwa kufanya kazi? Watu hufanya kazi kama kawaida, hata idi watu wapo kazini kama kawaida
 
kwani public holiday watu hukatazwa kufanya kazi? Watu hufanya kazi kama kawaida, hata idi watu wapo kazini kama kawaida

Sio official holiday labda nibadilishe language, haitambuliwi na serikali!
 
Hujasoma post #2.
Nimeeleza kwanini Pasaka ni sikukuu kubwa. Na huu uzi lengo langu ni kusisitiza kuwa Pasaka ni sikukuu kubwa. Yesu asingefufuka, imani yetu ingekuwa bure. Lakini sasa Jesus is alive! Haleluya! Ndio sababu hata "Rais wa dunia" anaandaa "dinner" ya nguvu 🙂
Waambie ndugu zako wakuwahishe hospital,
 
Nilimsikia ustadh mmoja akisema skukuu ya Pasaka ni yao kwakuwa wao bado wanachinja wanyama wa sadaka kama waasisi walivyochinja Pasaka ya zama za Musa:
 
Easter dinner inaliwa leo Ikulu ya Marekani, wewe unasema Pasaka haitambuliwi na serikali?!!
Screenshot (5).png


Kwani wakila dinner ndio official? We unagoogle mi naziishi! Tafuta pasaka hapo mkandamizaji
 
View attachment 3305961

Kwani wakila dinner ndio official? We unagoogle mi naziishi! Tafuta pasaka hapo mkandamizaji
Waliopanga hiyo holiday schedule ni watu wasiojua umuhimu wa Pasaka, kama wewe. Trump ametambua watu hawajui umuhimu wa kufufuka kwa Yesu. Anawafundisha kwa vitendo kwa kuandaa dinner Ikulu. Wewe shikilia tu hiyo kalenda yako, wenzako wanashikilia mapaja ya kuku leo, na kesho kutakuwa na Easter service, watamsifu Mungu. Fuatilia sherehe hizo.
 
Marekani pasaka wala sio public holiday, kazi kama kawa! Hiyo sherehe nzito umeionea online? Au umehadithiwa?
Pasaka huwa ni Jumapili, ambayo generally huwa sio siku ya kazi. Ila kama serikali ya Marekani huwa inafanya kazi siku za jumapili basi upo sahihi, Pasaka sio public holiday, japo huwa naona pale ubalozini kwao huwa hawafanyi kazi siku za Jumapili
 
Wiki hii kote ulimwenguni Wakristo watasherehekea Pasaka. Pasaka ni sikukuu kubwa kwa Wakristo kwa sababu ni siku ya kuadhimisha tukio muhimu sana katika imani ya Kikristo — kufufuka kwa Yesu Kristo kutoka kwa wafu. Bila Pasaka, hakuna Ukristo. Ndiyo sababu Wakristo huiona Pasaka kuwa ni siku kuu ya kipekee kuliko Krismasi.

Nchini Marekani, wiki hii inatambulika kuwa ni Wiki Takatifu(Holy Week). Mwaka jana Rais Mstaafu, Joe Biden aliiadhimisha wiki ya Pasaka kwa kutoa tangazo la kuwatambua watu waliobadili jinsia!! Rais Trump amepindua uchafu huo na kuipa heshima wiki hii kwa kuandaa matukio makubwa ya kuadhimisha Pasaka.

Wiki hii, Jumatano jioni, wafanyakazi wa Ikulu ya Marekani watakuwa na "Dinner" nzito ya Pasaka. Alhamisi itakuwa siku ya maombi na kumwabudu Mungu kwa wafanyakazi wote wa Ikulu ya Marekani. Siku hiyo wafanyakazi hao watapata pia nafasi ya kusikiliza Neno la Mungu kutoka kwa Wahubiri mbalimbali.

Jumapili iliyopita, Rais Trump aliahidi kuilinda imani ya Kikristo mashuleni, katika Jeshi na katika maeneo yote ya kazi. Alisisitiza pia kwamba ataendelea kulinda uhuru wa kuabudu katika nchi hiyo.

Rais Trump haoni aibu kumtangaza Yesu na yuko tayari kuujulisha ulimwengu wote kuhusu imani yake.

Baada ya kuanza muhula wake wa pili, Rais Trump alianzisha "White House Faith Office" kupitia agizo la kiutendaji tarehe 7 Februari 2025, akiwa na lengo la kuyasaidia mashirika ya kidini na ya kijamii katika juhudi za kuimarisha familia za Marekani na kulinda uhuru wa kidini. Ofisi hii ndiyo inayoandaa sherehe kubwa za Pasaka, Ikulu ya Marekani, mwaka huu.

Wewe je, umeandaa nini kusherehekea Pasaka? Karibu nyumbani kwetu ule vinono!

Grace and peace to you this Easter season. God bless you abundantly.
Ati pasaka ilikua kufufuka kwa yesu?mbona yesu nae alisherehekea pasaka??alikula pasaka ya nini sasa?ndo mnavosomewa na wachungaji na manabii wenu hivo?soma kutoka sura ya 12 yote uilewe pasaka na sio hii unayoisema eti ni kufufuka kwa yesu.pasaka ni kumbukumbu ya wa israel kutolewa utumwani misri.soma kutoka sura ya 12 yote na ulete hoja.soma luka mtakatifu sura ya 22:1 tu.pasaka ni sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu,hio mnaiitaga ijumaa kuu natesekaga kupata nyama,eti hawali nyama wanakumbuka mateso ya yesu kwahio kula nyama ni kosa siku hio.nina mwaka wa kumi siingii kanisan pumba tu.biblia inapatikana nishindwe kusoma na kuelewa?
 
My friend Nyani Ngabu soma title kwa utulivu.
Ngoja nikufafanulie: Sijasema Pasaka ni sikukuu kubwa Marekani. Nimesema Pasaka ni sikukuu kubwa kuliko Krismasi, na Ikulu ya Marekani wameandaa sherehe nzito(kuadhimisha siku hiyo).

Nimefafanua kwanini Pasaka ni sikukuu kubwa katika Post #2.
Nadhani wewe unaangalia idadi ya watu wanaoisherehekea Krismas ukilinganisha na wanaosherehekea Pasaka.
Huna akili
 
Ujumbe umeupata. Yesu amefufuka!
Sema: "Amefufuka kwelikweli"
Itakuwa wewe ni mmojawapo ya wale wanaotembea na spika barabarani na kuanza kushusha neno, au wewe unakuwaga kwenye mabasi?
 
Back
Top Bottom