Kusema kwamba Pasaka sio sikukuu muhimu kwa sababu sio Federal Holiday nchini Marekani ni kuchanganya kati ya umuhimu wa Kikristo na uamuzi wa serikali.
Pasaka ni mojawapo ya sikukuu muhimu zaidi kwa Wakristo duniani kote, kwa sababu inaadhimisha kufufuka kwa Yesu Kristo – msingi wa imani ya Kikristo.
Kutoitwa Federal Holiday hakupunguzi thamani ya kiroho wala athari yake kwa maisha ya waumini. Ukiacha Pasaka, kuna siku nyingine muhimu kiroho ambazo serikali ya US haijazipa hadhi ya likizo ya kitaifa.
Kwa mfano, Jumapili yenyewe ni siku muhimu ya ibada kwa Wakristo, lakini sio Federal Holiday.
Vivyo hivyo, siku ya Pentekoste sio Federal Holiday, lakini ni siku muhimu sana kwa Wakristo kwa sababu ni siku ambayo Roho Mtakatifu alishuka juu ya wanafunzi, na Kanisa likazaliwa (Matendo 2). Bila Pentekoste, hakuna ujasiri wa kuhubiri injili wala nguvu ya kushuhudia.