Pasaka ni sikukuu kubwa kuliko Krismasi - Ikulu ya Marekani yaandaa sherehe nzito!

Soma title kwa utulivu, zerominus10
Ngoja nikufafanulie: Sijasema Pasaka ni sikukuu kubwa Marekani. Nimesema Pasaka ni sikukuu kubwa kuliko Krismasi, na Ikulu ya Marekani wameandaa sherehe nzito(kuadhimisha siku hiyo).
Wamarekani hawanaga upuuzi huo, Makanisa yote wamegeuza makasino.
 
Reactions: Lax
Maelezo uliyotoa hayatoshi kushawishi ukubwa wa pasaka.
 
We majivuno unayo Ila siyo ya pesa.
 
Ukisoma Theology ya wakristo utaelewa kwanini ilikua hivyo,,,huyo hakuja kwa ajili ya maisha ya kimwili ,,,,njia yake inaakisi maisha ya kiroho ya binadamu yanavyotakiwa kua mbele ya Mungu, huo unyenyekevu na kujishusha ndo binadamu anavyotakiwa awe mbele ya Mungu na pia kwa mkristo unaambiwa Yesu yupo ndani yako ni wewe tu kuweka mazingira sawa utaanza kuona nguvu yake ndani yako ,,,na hapohapo unaambiwa Yesu ni Mungu kwahio Mungu yupo ndani yako, ni wewe unaetakiwa kuweka mazingira yako ya kiroho sawa ili hio nguvu ya ndani mwako iweze kufanya kazi.............Ukristo umekaa ki theolojia zaidi huku ukitumia lugha za mafumbo (picha) za kibinadamu ndo maana mtu akiuendea tu kimwili hataelewa ,maana concept ya christ inajulikana tokea enzi za wamisri wakale (kemet) na ukipata muda wakusoma elimu za hao jamaa ndo utauelewa vizuri ukristo..........au kama umeshawahi kusikia hili neno "christ consciousness" utaelewa theology ya kikristo inabeba nini,,,,,,,......kabla ya kusoma kiundani vitabu vya metaphysics ukristo nilikua nauchukulia poa tu na baadhi ya mambo nikawa naona kama stori tu ila baada ya kusoma vizuri elimu za wagiriki na wamisri wa zamani nikaja kuelewa maana nzima ya ukristo,,,,,hii dini ukiyachukulia yale maandiko kwa lugha za kibinadamu unapotea
 
Maelezo uliyotoa hayatoshi kushawishi ukubwa wa pasaka.
Pasaka ndo inabeba maana nzima ya ukristo maana Yesu bila kufa na kufufuka kusingekua na ukristo....na kuja kwake mission yake kubwa ilikua ni hio.....ndo maana kwa mkristo msalaba ni alama ya ukombozi,,,,,,bila Yesu kufa msalabani kusingekua na ukristo......ukubwa wake upo upande wa kiimani sio katika upande wa wingi wa watu kusherehekea.....Kikanisa hii ni sherehe kubwa kuliko Christmas
 
Amen
 
Kiujumla pasaka ni sikukuu ya BWANA, hata Kwa Dini ya kiyahudi kwao pasaka ni sherehe kubwa sana, kwasababu wanakumbuka siku BWANA alivyowapiga pigo la mwisho wamisri ambalo liliwakomboa waisraeli kutoka utumwani.

Kifo na ufufuko wa kristo ni ukombozi mwingine wa BWANA Kwa viumbe wake wote wanaomwamini, na kuishi Imani ya ukombozi. Na ndiyo maana wasiomwamini kristo wanasema hakufa msalabani, Hawa ni wapingaji wa pasaka.
 
Umeandika vizuri. Ubarikiwe ndugu yangu Lighton
 
Hongereni kwa kusherehekea Pasaka, lakini tukio kama hili litakuwa linatambulika na imani tatu kubwa zenye asili moja. Huenda watu wengine wakashangaa, ndiyo Uyahudi, Ukristo na Uislamu unaadhimisha hii sikukuu ya Pasaka kwa aina yake.

Uyahudi unasherehekea Pasaka (Pesach/Passover) na ndiyo asili ya Pasaka kupatikana na ni kutoka kwa Wanaisraeli kutoka utumwani Misri, chini ya uongozi wa Musa.
Mungu aliwaamuru Waisraeli wachinje mwana-kondoo, wapake damu yake milangoni.
Walilindwa wakati malaika wa mauti alipopita kuua wazaliwa wa kwanza wa Wamisri.
Tukio hili liliashiria mwanzo wa uhuru wao kutoka utumwani.
Katika agano la kale inaandikwa katika Walawi 23:5 “Jioni ya siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza mtaadhimisha kwa heshima yangu mimi Mwenyezi-Mungu sikukuu ya Pasaka.

Ukristo nao unasherehekea Pasaka kama maandiko yanavyoeleza:
Matayo 26:17
17- Siku ya kwanza ya sikukuu ya Mikate isiotiwa chachu wale wanafunzi walikuja kwa Yesu wakamwuliza, “Ungependa tukuandalie wapi chakula cha Pasaka?”

Na Paulo anasema:
1 Wakorinto 5:7
Ondoeni chachu ya zamani ili mpate kuwa donge lisilo na chachu, kama mnavyotakiwa kuwa. Kwa maana Kristo ambaye ndiye Mwana-kondoo wetu wa Pasaka amekwisha tolewa kama dhabihu. 8 Kwa hiyo, tusherehekee sikukuu hii, sio kwa chachu ya zamani, chachu ya nia mbaya na uovu bali kwa mkate usiotiwa hamira, wa moyo safi na kweli.

Uislamu unasherehekea Pasaka kama hadthi ya mtume Muhammad (rehma na amani ziwe juu yake)

Mtume alipoingia Madina, aliwakuta Mayahudi wakifunga siku ya Ashura.
Akawauliza: "Kwa nini mnafunga siku hii?"
Wakasema:
"Hii ni siku kubwa ambapo Allah alimuokoa Musa na Wana wa Israeli kutoka kwa Firauni, na Musa alifunga siku hii kwa shukrani."
Mtume akasema:
"Sisi tuna haki zaidi kwa Musa kuliko nyinyi." Kisha akaamuru kufunga siku hiyo.

Ashura ni siku ya kumi (10) ya mwezi wa Muharram, ambao ni mwezi wa kwanza katika kalenda ya Kiislamu (Hijri).
 
Nani alikudanganya pasaka ni sikukuu ya kufufuka yesu? Mbona yesu mwenyewe alisherehekea pasaka akiwa mdogo?

Kasome Luka 2:41–43:*
41 Na wazazi wake walikuwa wakikwenda Yerusalemu kila mwaka kwa sikukuu ya Pasaka.
42 Na alipokuwa na miaka kumi na miwili, wakakwea kwenda huko kwa desturi ya sikukuu.*
43 Hata walipokwisha kuzitimiza siku hizo, walipokuwa wakirudi, mtoto Yesu alikaa Yerusalemu, na wazazi wake hawakujua

Hayo maneno ya kuwa pasaka ni sherehe ya kufufuka yesu mmeyatoa wapi?
 
Hivi yeye alisulubiwa Katikati ya sikukuu ya pasaka au Pasaka ndio alifufuka?🤔, kuna Jambo halipo sawa mahali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…