Katibu Mwenezi wa Jimbo la Nsimbo mkoani Katavi, Pascal Anthony, amemshutumu Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche, kwa kukiingiza chama hicho kwenye mpasuko mkubwa, kukataa maridhiano, na kufukuza wanachama wanaokosoa ubadhirifu wa fedha, huku akitangaza kuwa vijana wa mkoa huo wanaandaa maandamano yasiyo na kikomo shinikizo la kumtaka ajiuzulu.
"Kwanza ukiuliza tu swali la ubadhirifu unaoendelea ndani ya chama, wewe hapo ni kufukuzwa. Sasa sisi kama vijana tunajiorganize, tunataka tuandae maandamano makubwa sana hapa mkoa wa Katavi na tunamwambia... tunaandika barua kwa OCD atupe tutandamana, asipotupa tutandamana kwa sababu huu ujumbe inatakiwa Watanzania wajue nini kinachoendelea ndani ya chama.
Sisi hatujanunuliwa ajili ya kumchafua Heche. Sisi tuko kwenye chama muda mrefu, tungenunuliwa muda mrefu. Ndio maana tumesema sisi, ina maana maandamano yetu kwanza yatakuwa sio ya kikomo mpaka atoke. Kwa sababu sisi Watanzania wanatakiwa wajue kwamba yule ni tatizo."