tpaul
Platinum Member
- Feb 3, 2008
- 27,843
- 29,350
Bila uoga, kutetereka wala kumuogopa mtu yeyote, mwanahabari na mwanasheria nguli, Mzee Pascal Mayalla ameeleza kinagaubaga bila kuacha shaka jinsi Ben Saanane na Azory Gwanda walivyotekwa na kupotezwa. Wawili hao tangu watekwe hawajawahi kuonekana tena kwenye uso wa dunia hii.
Mzee Mayalla hajaenda mbali na taarifa iliyowahi kutolewa na Profesa Paramagamba Kabudi akiwa Waziri wa Sheria, alipoutangazia ulimwengu kwamba:
“The government is still searching for people who disappeared and died, including Azory Gwanda and Ben Saanane.”
Profesa Kabudi aliyasema hayo wakati akihojiwa na chombo cha habari cha BBC alipokuwa ziarani huko Ulaya. Kwa hiyo, Mayalla amecheza mulemule katika mstari huo.

MAONI YANGU
Namkubali sana huyu mzee na ninamchukulia kama mwalimu wangu wa mfano (role model). Mwandishi wa habari unatakiwa uwe na viwango na ujasiri kama Mzee Mayalla. Hutakiwa kuogopa "nyinyinyi" wala "nywinywinywi." Amepasua jipu pwaaaaa!
Anayemchukia Mayalla ana chuki zake binafsi. Huyu ni mwandishi nguli na wa kupigiwa mfano ambaye tumepata kuwa naye tangu nchi hii ipate uhuru. Tumuunge mkono!
Soma pia Pascal Mayalla: Baada ya kupotezwa kwa Azory, Ben Saanane, Vyombo vya Habari vikaingiwa uoga