Pascal Mayalla aitaka TCRA iufungie mtandao wa Twitter kwani kuna mambo machafu yanayoendelea huko

Pascal Mayalla aitaka TCRA iufungie mtandao wa Twitter kwani kuna mambo machafu yanayoendelea huko

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Akizungumza katika kipindi cha Jicho letu ndani ya habari mwandishi nguli Pascal Mayalla amewataka TCRA kuwafuatilia wale wanaoandika uchafu kwenye mtandao wa Twitter na kama wameshindwa basi waufungie mtandao huo hapa nchini.

Na kama hayo yote hayawezekani basi Watanzania wazalendo wajulishwe ili waanze kuwaelimisha hao wachafuzi huko huko twittani.

Chanzo: Star TV

My take: Pascal Mayalla anafaa kuwa Msemaji mkuu wa serikali

Maendeleo hayana Vyama!

====
Alichokisema Pascal Mayalla ni kuwa wamewaandikia barua TCRA ili wajue kuhusu mambo yanayoendelea kwenye mitandao ya kijamii hasa twitter, kuwa tumeshindwa, hii ni kwa kuwa mambo yanayoendelea huko yanakarahisha. Ili kama tumeshindwa basi tuhamasishane kutosoma yanayoendelea twitter

 
Naunga mkono hoja, hata Usa imepitisha sheria kuanza kudeal na watu kama hawa wanaofanya uchochezi na kutukana viongozi kwa kutumia mitandao ya kijamii. Hivyo Tcra iifungie Twitter sababu imekuwa kichaka cha wasiojulikana kuwatukana viongozi wa serikali

Cc chagu wa malunde
Ku dili na watu sawa lakini sio kufungia source, Twitter ina tatizo gani kwa mfano, uadhibu watumiaji wote kwa sababu umeshindwa kudili na mtu mmoja.
 
Kipindi hiki cha karibuni kimekuwa kigumu sana kimaisha kwa wengi wetu na hata kwa nchi pia.

Wenyewe wanajiita wajanja wa mjini wamejipanga kugeuza kila kitu fursa panapo majaliwa. Mambo mengine baadaye.

Hata kwa mambo wasiyoyaamini wao wenyewe wamekuwa wakiyasimamia macho makavu kweli kweli. Unaweza usiamini kuwa huyu naye amefikia hatua hii? Ali mradi mkono uende kinywani.

Alisema baba wa taifa (rip), "mtu anasema anachukia rushwa, lakini ukimwangalia usoni unajiuliza. Huyu?! Kweli anachukia rushwa huyu?" Mwisho wa kumnukuu.

Wengine wa kuwaelewa tu wakuu. Ni kukaza vilivyo kwa vyuma tu. Hali ikiboreka tutaelewana huko huko mbele kwa mbele.
 
Naunga mkono hoja, hata Usa imepitisha sheria kuanza kudeal na watu kama hawa wanaofanya uchochezi na kutukana viongozi kwa kutumia mitandao ya kijamii. Hivyo Tcra iifungie Twitter sababu imekuwa kichaka cha wasiojulikana kuwatukana viongozi wa serikali

Cc chagu wa malunde
Ku dili na watu sawa lkn sio kufungia source, Twitter ina tatizo gani kwa mfano, uadhibu watumiaji wote kwa sababu umeshindwa kudili na mtu mmoja.

After all mtandao wa Twitter au Facebook sio sawa na gazeti la UWAZI kuwa unaweza kuzifuta kirahisi.
 
Serikali ya Magufuli itaufunga mtandao wa twitter kwa sababu ya kigogo? Yaani wamemshindwa Kigogo ataanzisha group kule telegram na tutamiminika.

Kiufupi huwezi kushindana na technology.

Paskali aje aseme mwenyewe hapa tumpe elimu.

Asiitie aibu UDSM.
 
Mwandishi wa habari huyu.

Yaani wakati waandishi wa habari Duniani kote wanapambania Uhuru wa habari, na kwa kuzingatia hali halisi nchini ambapo waandishi wanabanwa sana.

Yeye anakuja kuongea utopolo wa namna hii.

Twitter ni kama JF, kikubwa ni uhakika wa habari na habari ziwafikie watu.

Pascal Mayalla kwa hili umeharibu sana, na utapoteza watu wengi wanaokufatilia.

Usishangae mavipindi yako yakabaki kutizamwa na Lumumba tu.
 
Back
Top Bottom