Pascal Mayalla aitaka TCRA iufungie mtandao wa Twitter kwani kuna mambo machafu yanayoendelea huko

Pascal Mayalla aitaka TCRA iufungie mtandao wa Twitter kwani kuna mambo machafu yanayoendelea huko

Akizungumza katika kipindi cha Jicho letu ndani ya habari mwandishi nguli Pascal Mayalla amewataka TCRA kuwafuatilia wale wanaoandika uchafu kwenye mtandao wa Twitter na kama wameshindwa basi waufungie mtandao huo hapa nchini.

Na kama hayo yote hayawezekani basi watanzania wazalendo wajulishwe ili waanze kuwaelimisha hao wachafuzi huko huko twittani.

Chanzo: Star tv

My take; Pascal Mayalla anafaa kuwa Msemaji mkuu wa serikali

Maendeleo hayana vyama!
Pascal, unahitaji elimu ya dunia ya leo ilivyo, inaonyesha uko out of date. Huo uchafu hata mie nimeuona sana na ni kweli upo Swali jee mitandao ikifungiwa, jee inamaanisha hayo mambo hayatakuwepo nchini.

Zungumzia majukumu ya wazazi majimbani kwa watoto wao kwanza, wewe na mimi kama wazazi tunafanyaje.

Tunawabunge wanaosemekana wanamahusiani ya ki LGBT, kama ni kweli jee haimaanizhi tunayakubali magusiano hayo? Tuna wasenge wanaojitangaza kuwa walikuwa na uchafu huo na wanajiremba kama wananwake, leo wanajiita Manabii na wanatukuzwa na makanisa kama ya akina Gwajima, kwa kumleta hadharani, na magazeti kuandika habari zao, jee hatuutukuzi huo uchafu kwa kuyazungumzia bila kuya kebehi na kuyakataa.

Tunawaona wasichana wa miaka chini ya 15, wakitembea na watu waZima na kupelekwa MALODGE mitaani, hakuna wa kukemea, na lodge zinaona ni biashara na hawaweki kiwango cha umri.

Pascal be realistic, CHARITY BEGINS AT HOME

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimemusikiliza Paschal, yeye ni team ya sifa na kuabudu, so anatamani kila mtu ajiunge kwenye ujinga huo! Kama ya twitter hayapendi kinachompeleka huko ni kitu gani!? Aache ujinga!
Woga huondoa maarifa, na ukiendekeza ujinga uzaa upumbavu. Kigogo anatumia kalamu /keyboard kuelezea hoja,basi serikali na watetezi wa serikali watumie kalamu/keyboard hiyo hiyo kujibu hoja hizo.

Ukisha kuwa top public figure unakuwa kama golden fish huna sehemu ya kujificha ni mali ya wote utasakamwa, utatukanwa, utabezwa, kejeli, utasingiziwa, utachunguzwa, na wakati mwingine utatupiwa mayai viza.

Lakini kama huwezi hayo, hakuna haja ya kugombea nafasi ya umma, kaa nyumbani na familia yako achana na kazi za umma.
 
Naunga mkono hoja, hata Usa imepitisha sheria kuanza kudeal na watu kama hawa wanaofanya uchochezi na kutukana viongozi kwa kutumia mitandao ya kijamii. Hivyo TCRA iifungie Twitter sababu imekuwa kichaka cha wasiojulikana kuwatukana viongozi wa serikali
Anochozungumzia na uchafu uchochezi sio uchafu na hila ya kuchonganisha, na wajinga tuu ndio watakao chonganishwa bila kuuliza nini kiko nyuma ya hilo jambo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe pasikali Hivi sisi chadema tukichukua nchi halafu watokee watu wanaojipendekeza kwetu watushauri kuwa serikali ya chadema ibomoe kile kighorofa cha Lumumba kwa kuwa kinatumika na Lumumba buku saba kukosoa serikali utaunga mkono kweli mawazo hayo
 
Ana stress za kuachwa na mkewe mama Mark & Linda... issue ya familia yake ya watu 4 imemshinda anataka a deal na mass issues, a-deal na issue zake za familia kwanza kabla ya ku deal na twitter!!
 
Pamoja kwamba wewe ni kada wa CCM. Nikwambie tu. Kigogo asiwafanye mtake kufunga twitter. Twitter mtandao wa kimataifa.

Hadi JPM yumo. Mawaziri wamo. Sio kitu kirahisi kama unavyodhani.
Unajiita nani vile ?eti sio jambo rahisi kwani hujui kuwa kuna nchi kibao zimefungia Facebook. Twitter na takataka zingine

Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
 
Naunga mkono hoja, hata Usa imepitisha sheria kuanza kudeal na watu kama hawa wanaofanya uchochezi na kutukana viongozi kwa kutumia mitandao ya kijamii.

Hivyo TCRA iifungie Twitter sababu imekuwa kichaka cha wasiojulikana kuwatukana viongozi wa serikali

Uko sahihi, ila viongozi wa serikali wao wanaweza kuvunja sheria za nchi, kama kunajisi chaguzi za nchi, na kuaigiaz mahakama kutokutenda haki. Na kwa kutumia madaraka yao, wao wanaweza kubadili sheria ili wasishitakiwe!
 
Ni mwanahabari nguli!

Nilitegemea Paskali angehoji ni kwanini viongozi wanataka kutunga sheria ya kutoshitakiwa iwapo kweli wanafanya matendo mema. Lakini naona kaamua kujichukulia pointi za mezani.

Nilimsikia akisema hata yeye iko siku ataomba msamaha kama kina Kinana, Nape nk ili mambo yake yaende vizuri. Hata hiyo kuitaja Twitter ni kama anaweka mazingira vizuri ili apewe ulaji.
 
Khaaaa ifutwe twitter, then? Akitaka yeye afunge akaunti asione kinachoendelea huko... Asituharibie
 
Nilitegemea Paskali angehoji ni kwanini viongozi wanataka kutunga sheria ya kutoshitakiwa iwapo kweli wanafanya matendo mema. Lakini naona kaamua kujichukulia pointi za mezani. Nilimsikia akisema hata yeye iko siku ataomba msamaha kama kina Kinana, Nape nk ili mambo yake yaende vizuri. Hata hiyo kuitaja Twitter ni kama anaweka mazingira vizuri ili apewe ulaji.
Bwashee wewe unafurahishwa na mambo machafu ya huko Twitter?

Maendeleo hayana vyama!
 
Unjiita nani vile ?eti sio jambo rahisi kwani hujui kuwa kuna nchi kibao zimefungia Facebook. Twitter na takataka zingine

Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
For the record ni nchi tatu tu. Zilizo zuia mtandao wa.twitter. China, North Korea ,Iran.

Nchi zilizuia Facebook ni China na Iran, pakistan, syria, vietnam, mauritius, Egypt.

According to last statistics. For the record ni kuwa hii ndio mitandao ambayo iko active sana duniani kwa sasa. Hizo takataka zingine no body cares.

So hizo.nchi kibao zilifunguia ni zipi? For the record tu hata 10 hazifiki.
 
Tatizo sio mtandao wa twitter ila tatizo ni hao watumiaji wanaovujisha hizo taarifa mnazoziita "nyeti".
 
Bwashee wewe unafurahishwa na mambo machafu ya huko Twitter?

Maendeleo hayana vyama!

Sifurahishwi na tabia chafu ya popote, achia mbali hiyo twitter. Mada iliyokuwa mezani ilikuwa ni ya magazetini, kuhusu hotuba ya rais jana kwenye baadhi ya magazeti. Kisha mwananchi kuhusu sheria ya viongozi kutoshitakiwa, na Tanzania daima kuhusu msamaha wa Kinana.

Lakini hakugusia chochote kuhusu viongozi kutishitakiwa, kwa mantiki viongozi wakifanya mambo chafu ni sawa, ila uchafu wa twitter ndio unamtesa, maana hao wenye uchafu huko twitter hawawezi kumpa cheo. Paskal aache unafiki.
 
Wakifungia Twitter tutahamia Badoo.

Kama wameshindwa kuendesha nchi si wapumzike Kwani ni lazima waendelee kuwa viongozi?
 
Back
Top Bottom