Pascal Mayalla aitaka TCRA iufungie mtandao wa Twitter kwani kuna mambo machafu yanayoendelea huko

Pascal Mayalla aitaka TCRA iufungie mtandao wa Twitter kwani kuna mambo machafu yanayoendelea huko

johnthebaptist,
Ni kweli TCRA wana uwezo na mamlaka ya kufungia mtandao wa Twitter kuwepo Tanzania kimawasiliano lakini sioni sababu za msingi kufanya hivyo. Swala ni kuwashughulikia ambao wanapotosha kama ilivyotokea kwa Zito Kabwe

Sheria zipo, cha muhimu ni kuchukuliwa hatua za kisheria kwa wale wanaokuwa wanatumia hiyo service vibaya ie kukiuka sheria. Sio vibaya kwa Serikali kuongeza budget ya wataalam ili kuweka nchi hii salama.
 
Naunga mkono hoja, hata Usa imepitisha sheria kuanza kudeal na watu kama hawa wanaofanya uchochezi na kutukana viongozi kwa kutumia mitandao ya kijamii.

Hivyo TCRA iifungie Twitter sababu imekuwa kichaka cha wasiojulikana kuwatukana viongozi wa serikali

Muongo na ni dhahiri una matatizo na lugha ya kiingereza. Amri (sio sheria - sheria za marekani hupitishwa na bunge la wawakilishi) ya Trump ni ya kuwaondolea wamiliki wa twitter kinga kadhaa dhidi ya maudhui yanayopandikwa.

Amri hiyo haihusu kuondolewa kwa twitter nchini Marekani wala serikali kufungia au kushitaki wachangiaji.
 
Wakisha kuifunga twitter kuna ugumu gani kuifunga JF?

Hayo si maneno yanayopaswa kutoka kwa mwanahabari na mwanasheria. It's scaring. Be careful what you wish for kaka Pascal!
 
Hivi kweli serikali imeshondwa kuifungia twita hapa nchini? Sidhani kama tunaihitaji kiasi hicho maana kuna utovu mkubwa wa nidhamu unaendelea huko na wahusika hawakamatwi na kuchukuliwa hatua.
 
Serikali inatumia twitter, hadi Rais anayo account huko. Sasa Mayalla ukiona uchafu twitter basi ujue ni wewe ndio ume follow hao waandika uchafu!
Yaani MTU kama Kigwa ukimfungia twitter, kuna twitter gulio kuna biashara nyingi sana zipi Twitter, kuna elimu kuna madeal.
Yaani wasukuma bwana Mungu atuepushe ni hawa watu.

Kigogo atasababishà furs nyingi zipotee kama Magufuli atachukua huu ushauri. Na msishangae akaifunga. Meko is unpredictable
 
Muongo na ni dhahiri una matatizo na lugha ya kiingereza. Amri (sio sheria - sheria za marekani hupitishwa na bunge la wawakilishi) ya Trump ni ya kuwaondolea wamiliki wa twitter kinga kadhaa dhidi ya maudhui yanayopandikwa.

Amri hiyo haihusu kuondolewa kwa twitter nchini marekani wala serikali kufungia au kushitaki wachangiaji.
Inawezekana wewe ndio hujui lugha. Kwa sababu executive order ni sheria. Ni tamko la rais ambalo linakuwa ni sheria (japokuwa haijapitishwa na congress) na fikiri hata hapa Tz vitu kama hivi vipo ila kuelewa kuwa orders an declarations za viongozi wakuu huwa ni sheria ambazo hazijapitishwa na bunge mpaka uwe una weledi kidogo.
 
Mnafiki Mayalla
12E117D2-F505-41A7-B597-77FB1F8B353C.jpeg
 
Yaani wewe ukiwa mwanahabari unapinga uhuru wa maoni, unashangaza ... Pasco use or find other tactics/ways za kum win Magufuli hizi zinachosha, na ndio maana hakupi huo uteuzi, sisi kama binadamu hatupendezwagi kuona mtu yuko desperate..it is nature!!!..unakosea sana
 
Ku dili na watu sawa lakini sio kufungia source, Twitter ina tatizo gani kwa mfano, uadhibu watumiaji wote kwa sababu umeshindwa kudili na mtu mmoja.
😃😃 yaani uchome nyumba unayoishikisa mmoja ya watoto wako ni mtukutu...
hii itazidi kudhihirisha kwamba intellegence ya tz ni ya hovyo sana
yaani TCRA wawe tayari kukosa mapato kwaajili ya mtu mmoja tu?

huyo mayalla amekula maharage ya wapi😃😃
 
Kipindi hiki cha karibuni kimekuwa kigumu sana kimaisha kwa wengi wetu na hata kwa nchi pia.

Wenyewe wanajiita wajanja wa mjini wamejipanga kugeuza kila kitu fursa panapo majaliwa. Mambo mengine baadaye.

Hata kwa mambo wasiyoyaamini wao wenyewe wamekuwa wakiyasimamia macho makavu kweli kweli. Unaweza usiamini kuwa huyu naye amefikia hatua hii? Ali mradi mkono uende kinywani.

Alisema baba wa taifa (rip), "mtu anasema anachukia rushwa, lakini ukimwangalia usoni unajiuliza. Huyu?! Kweli anachukia rushwa huyu?" Mwisho wa kumnukuu.

Wengine wa kuwaelewa tu wakuu. Ni kukaza vilivyo kwa vyuma tu. Hali ikiboreka tutaelewana huko huko mbele kwa mbele.
😃😃 indeed
 
Jamani si haki yke kikatiba kutoa maoni yke kikubwa wa jitaidi kuheshim na mawazo ya wengine ilo ndio kubwa...
 
Back
Top Bottom