Pascal Mayalla aitaka TCRA iufungie mtandao wa Twitter kwani kuna mambo machafu yanayoendelea huko

Pascal Mayalla aitaka TCRA iufungie mtandao wa Twitter kwani kuna mambo machafu yanayoendelea huko

Tatizo la huyu anaejiita Pascal ni njaa ya uteuzi tu ndio inamsumbua na akumbuke tu lolote asemalo afanyalo hata pata uteuzi... narudia tena hata apata uteuzi
 
Siamini kama maneno hayo aliyasema Pascal maana yeye yupo Twitter na hata mzee mwenyewe yupo. Kwa hiyo anayoandika Pascal huko ni haramu? Au anayoandika huko Magufuli nayo ni haramu?
Mwisho kuna siku tutaambiwa makanisa nayo yafungwe kwa sababu mzee wa upako akipiga konyagi anatukana!
Screenshot_20200607-062609.jpg
Screenshot_20200607-062734.jpg
Screenshot_20200607-062813.jpg
 
Akaambie hukohuko alafu awe na heshima aache kutia aibu hao TCRA hawana uwezo wa kufunga Twitter! 😂
 
johnthebaptist, Pasko ana maono. Twitter , Face na Instagram zifungwe.Uanzishwe mtandao wa serikali ambslo watu waturuhusiwa kuchangia kuhusu juhudi za serikali tu
 
Ukitaka kujua uwezo wa mtu wa kufikiri,basi mpe nafasi aseme.

Ukiona hoja zikipigwa rungu basi ujue uwezo wa kufikiri umefikia mwisho.

Watu waachwe wapumue,kuongea ni haki ya msingi ya watu kutoka kwa Mungu.

Ukiona hutaki kuvumilia mawazo ya watu basi ujue wewe ni ndugu yake ibilisi,na makazi yako ni jehanum.
 
Ni KIGOGO tu hakuna lingine! Bro P anakerwa sana na maudhui ya Kigogo. Hivyo basi fungua macho na ubongo utambue bro P ni Mwana JF Wa namna gani!!!
 
Twitter inaweza fungwa hapa tz umataifa wake ukabaji huko kwingine, tambua hilo.
O P S zinazotumika hata ndani ya ikulu za Tanzania zinatengenezwa Marekani,IT wetu hawajawa na uwezo wa kutengeneza za kwetu,kishapo mjinga mmoja anatulinganisha na wachina.

Bado tuna safari ndefu kwenye fikra zetu.
Uwezo wa kujenga na kujibu hoja huna,unakimbilia kufunga mitandao??
 
Akizungumza katika kipindi cha Jicho letu ndani ya habari mwandishi nguli Pascal Mayalla amewataka TCRA kuwafuatilia wale wanaoandika uchafu kwenye mtandao wa Twitter na kama wameshindwa basi waufungie mtandao huo hapa nchini.

Na kama hayo yote hayawezekani basi Watanzania wazalendo wajulishwe ili waanze kuwaelimisha hao wachafuzi huko huko twittani.

Chanzo: Star TV

My take: Pascal Mayalla anafaa kuwa Msemaji mkuu wa serikali

Maendeleo hayana Vyama!
Huyo Paskali ana mambo mengi ya ajabu. Wewe angalia anayoyaandika...ingekuwa bora angefungwa tu na huyo spika. Kama kweli anasema Twitter ifungiwe? Basi ana shida kubwa. REVISED
 
Naunga mkono hoja, hata Usa imepitisha sheria kuanza kudeal na watu kama hawa wanaofanya uchochezi na kutukana viongozi kwa kutumia mitandao ya kijamii.

Hivyo TCRA iifungie Twitter sababu imekuwa kichaka cha wasiojulikana kuwatukana viongozi wa serikali

Hakuna kitu kama hicho

USA imepitisha executive order ya kuitaka mitandao ya jamii iache kuban ban watu hovyo na kuwafanyia watu censoring. Nyie mmeelewa kinyume!, Hii ilitokana na hiyo mitandao kumfact check Trump, na Trump kwa hasira akasaini hiyo executive order
 
Back
Top Bottom