Akizungumza katika kipindi cha Jicho letu ndani ya habari mwandishi nguli Pascal Mayalla amewataka TCRA kuwafuatilia wale wanaoandika uchafu kwenye mtandao wa Twitter na kama wameshindwa basi waufungie mtandao huo hapa nchini.
Na kama hayo yote hayawezekani basi Watanzania wazalendo wajulishwe ili waanze kuwaelimisha hao wachafuzi huko huko twittani.
Chanzo: Star TV
My take: Pascal Mayalla anafaa kuwa Msemaji mkuu wa serikali
Maendeleo hayana Vyama!
====
Alichokisema Pascal Mayallani kuwa wamewaandikia barua TCRA ili wajue kuhusu mambo yanayoendelea kwenye mitandao ya kijamii hasa twitter, kuwa tumeshindwa, hii ni kwa kuwa mambo yanayoendelea huko yanakarahisha. Ili kama tumeshindwa basi tuhamasishane kutosoma yanayoendelea twitter
Kuna mambo makubwa na mazito anategemewa kuyazungumzia Pascal Mayalla anapopata hizo nafasi adimu, hayo ya twitter awaachie huko huko twitter au ajibizane nao huko.
Naunga mkono hoja, hata Usa imepitisha sheria kuanza kudeal na watu kama hawa wanaofanya uchochezi na kutukana viongozi kwa kutumia mitandao ya kijamii.
Hivyo TCRA iifungie Twitter sababu imekuwa kichaka cha wasiojulikana kuwatukana viongozi wa serikali
Naunga mkono hoja, hata Usa imepitisha sheria kuanza kudeal na watu kama hawa wanaofanya uchochezi na kutukana viongozi kwa kutumia mitandao ya kijamii. Hivyo Tcra iifungie Twitter sababu imekuwa kichaka cha wasiojulikana kuwatukana viongozi wa serikali
Kipindi hiki cha karibuni kimekuwa kigumu sana kimaisha kwa wengi wetu na hata kwa nchi pia.
Wenyewe wanajiita wajanja wa mjini wamejipanga kugeuza kila kitu fursa panapo majaliwa. Mambo mengine baadaye.
Hata kwa mambo wasiyoyaamini wao wenyewe wamekuwa wakiyasimamia macho makavu kweli kweli. Unaweza usiamini kuwa huyu naye amefikia hatua hii? Ali mradi mkono uende kinywani.
Alisema baba wa taifa (rip), "mtu anasema anachukia rushwa, lakini ukimwangalia usoni unajiuliza. Huyu?! Kweli anachukia rushwa huyu?" Mwisho wa kumnukuu.
Wengine wa kuwaelewa tu wakuu. Ni kukaza vilivyo kwa vyuma tu. Hali ikiboreka tutaelewana huko huko mbele kwa mbele.
Naunga mkono hoja, hata Usa imepitisha sheria kuanza kudeal na watu kama hawa wanaofanya uchochezi na kutukana viongozi kwa kutumia mitandao ya kijamii. Hivyo Tcra iifungie Twitter sababu imekuwa kichaka cha wasiojulikana kuwatukana viongozi wa serikali
Pascal Mayalla katika ubora wake wa kipekee. Yaani mwandishi wa habari nguli na mbombezi anaamini katika njia ambayo kimsingi inazuia upatikanaji huru wa habari.
Watafungia vyombo vingapi vya habari? Kwa nini wasichague tu hizi njia mbili! Kupuuza au kujirekebisha/kubadilika?
Hapana mimi suingi mkono hoja, hao wanaotukana acha wamalizie hasira zao twitter kwa kutukana. Hasira ziishie huko, Kuliko wakikosa pakumaliza hasira zao wakatafuta namna nyingine mbaya zaidi ya kumaliza chuki zao.