Pascal Mayalla amchambua Dkt. Bashiru, adai aliandaliwa kuwa Rais 2025

Freed Freed

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2017
Posts
6,547
Reaction score
7,167
Mwana JF nguli, Akihojiwa Radio DW Pascal Mayala, amemchambua Dr Bashiru. Amesema Dr Bashiru kapata ajali kubwa sana kisiasa na hatoinuka tena. Pia kadai Magufuli amiini usiamini alikuwa akimwandaa Dr Bashiru kuwa Rais 2025.

Mayala amedai Dr Bashiru aliyeibukia kuwa Katibu Mkuu wa CCM baada ya kuhakiki Mali za chama hicho alichukiwa mno kutokana na style yake ya uongozi.

Amesema amekinyoosha mno chama hadi kupitiliza na kusababisha kuchukiwa mno kuliko Katibu Mkuu yeyote katika Historia ya CCM. Pia amedai Dr Bashiru ni mjamaa mno au Mnyerere na Marehemu Magufuli alimkubali na kumpenda Sana na alipanga kumuachia Urais 2025.

Mayala amedai pia haoni njia ya Bashiru kufufuka tena kisiasa na ndiyo hivyo Mama Samia Suluhu ameshampoteza na Wana CCM wamefurahi mno.

Amesema kwa uhakika utawala wa Mama Samia Suluhu atakuwa Rais mzuri Sana kuliko Rais Magufuli.

Source: Radio DW Swahili, Leo mchana saa Saba, 01/04/2021.
 
Tangu akutane ikulu na ule Mhimili uliojikita chini zaidi ya mingine akaishia kufilisika na kukataliwa kufanya kazi yoyote ya serikali kaka paskali ameathirika sana kisaikolojia na hata kiuchumi na kiafya msameheni bure tu kwasababu hajui atendalo , yaani baada ya mhimili ule kufutika duniani ndio anaamka sasa pole yake sana
 
"Aliandaliwa kuwa Rais", inazidi kuthibitika sio wananchi wanaoamua nani awe Rais wa hii nchi, ni kikundi kidogo cha watu ndio kinatuchagulia Rais wamtakaye.

Watanzania tunahitaji Katiba Mpya sasa kuliko wakati mwingine wowote.

Mayalla alipiga kelele kwa Magufuli mpaka akachoka akanyamaza alipoona jamaa hana habari nae, naona amegeuza mapambio yake upande wa pili wa mama ajaribu bahati yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…