Pascal Mayalla amchambua Dkt. Bashiru, adai aliandaliwa kuwa Rais 2025

Pascal Mayalla amchambua Dkt. Bashiru, adai aliandaliwa kuwa Rais 2025

"Aliandaliwa kuwa Rais", inazidi kuthibitika sio wananchi wanaoamua nani awe Rais wa hii nchi, ni kikundi kidogo cha watu ndio kinatuchagulia Rais wamtakaye.

Watanzania tunahitaji Katiba Mpya sasa kuliko wakati mwingine wowote.
Na ndio maana Ufipa wanakuja kuokota Lumumba wagombea maana hawana maandalizi.
 
Mwana JF nguli, Akihojiwa Radio DW Pascal Mayala, amemchambua Dr Bashiru. Amesema Dr Bashiru kapata ajali kubwa Sana kisiasa na hatoinuka tena. Pia kadai Magufuli amiini usiamini alikuwa akimwandaa Dr Bashiru kuwa Rais 2025.

Mayala amedai Dr Bashiru aliyeibukia kuwa Katibu Mkuu wa CCM baada ya kuhakiki Mali za chama hicho alichukuwa mno kutokana na style ya uongozi.

Amesema amekinyoosha mno chama hadi kupitiliza na kusababisha kuchukiwa mno kuliko Katibu Mkuu yeyote ktk Historia ya CCM. Pia amedai Dr Bashiru no mjamaa mno au Mnyerere na Marehemu Magufuli alimkubali na kumpenda Sana na alipanga kumuacha Urais 2025.

Mayala amedai pia haoni njia ya Bashiru kufufuka tena kisiasa na ndiyo hivyo Mama Samia Suluhu ameshampoteza na Wana CCM wamefurahi mno.

Amesema kwa uhakika utawala wa Mama Samia Suluhu atakuwa Rais mzuri Sana kuliko Rais Magufuli.

Source: Radio DW Swahili, Leo mchana saa Saba, 01/04/2021.
Mr. Njaa zimefyatuka
 
"Aliandaliwa kuwa Rais", inazidi kuthibitika sio wananchi wanaoamua nani awe Rais wa hii nchi, ni kikundi kidogo cha watu ndio kinatuchagulia Rais wamtakaye.

Watanzania tunahitaji Katiba Mpya sasa kuliko wakati mwingine wowote.
Wewe unadhani Magufuli asingeweza kumuandaa Mtu peke yake? Yule alithibiti CCM, Bunge, Baraza la Mawaziri, Mahakama na Deep state au Mhimili uliojichimbia zaidi.
 
Mayalla yuko sawa asilimia 100. Huyo ndo kapotea jumla. Yeye asubiri kwenda kuomba Ubunge Jimboni kwake. He is completely finished.
 
Dr. Bashiru Ally Kakurwa...rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania 2025....[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji2839][emoji2839][emoji2827][emoji2827][emoji2827][emoji2827] !!! Mipango ya mtu mwana adamu si ya Mungu muumbaji
Na wote tuseme Amina

Lakini Paskali uwiiii ameshindikana kheee
Huu undumilakuwili ni dhahiri hana amani ndani ya moyo. Leo wa kusema Mama ni mzuri sijui bora kuliko aliyemtangulia?! Huu ni Unafiki Uchawi wa kupitiliza. Kwa nini hakukaa kimya kujiheshimu kuliko kujitengenezea maadui
Paskali punguza misifa isiyo ya lazima
Ulaghai dah
Usimtegemee Mwanadamu leo weye wa kumponda Magu ! Dunia inaenda mbio sana
Paskali muombe sana Mungu akufunulie msaidie na mwenzako msando wote mko na tatizo kwenye mioyo yenu

Pasaka Njema
 
Watu wanajua tafsiri ya Mjamaa au ?

Au Maana ya Mjamaa ni kulimbikiza mali kwa wajamaa wachache (CCM) na kuacha wengine wasio na vyama na wasio CCM kama watazamaji ?
 
Naunga mkono hoja ya Paschal Mayala

Hata hivyo utawala wa Magufuli ilikuwa umegibikwa na uhaba wa uhuru wa habari mchanganyiko zinazo hitajika katika kila jamii ,watu waliogofya na kuogioa haswaa ,waandishi wa habari hawakuandika habari yeyote inayo ihusu serikali hasa inapo kuwa haiendi sawa ,Badala yake kulisikikika habari za sifa na kuabudu tu mfalme .

Hii Ni hatari Sana ,na utawala wa namna hiyo huwa haudumu na haufurahishi watu wengi Bali wacheche walio kwenye mfumo .
Na hii inaweza kuwa ndicho chanzo kikuu Cha kumng'oa Bashiru kitini .

Tujitahidi kuishi na watu vizuri!
 
Kina Slow Slow na Bashiru walipotamba kushikisha watu adabu, waliambiwa wao ndio watakuwa wa kwanza kushikishwa adabu. Kinachowatokea hawaamini macho yao. Kwenye siasa hakuna mbabe. Tuishi kwa kuheshimiana. Now u cant imagine 2025 kina Bashiru hawatoweza tena kumla kichwa mgombea yeyote.
 
Back
Top Bottom