Pascal Mayalla anafaa kuwa Msemaji wa Serikali

Pascal Mayalla anafaa kuwa Msemaji wa Serikali

Mkuu ninakuelewa, it is possible akapewa hiyo post lakini she is not fit for that post, Paschal Mayalla deserves more to hold the post of Chief Government Spokesperson.
Pascal Mayala hana vigezo, msemaji wa serikali ni nafasi ya utendaji serikalini sio nafasi ya kisiasa kwamba yeyote anawezateuliwa ,kwanza miaka asiwe zaidi ya 45, na pia lazima awe anafanya kazi Serikalini na awe na cheo cha afisa mkuu
 
Unachosema sio kweli hata kidogo.

Kwa mujibu wa Kifungu cha 4 (1) cha Sheria ya Huduma ya Habari, 2016, Rais anatakiwa kumteua mtu kuwa Msemaji Mkuu wa Serikali iwapo ana sifa zifuatazo;

(a) Ana uadilifu wa kiwango cha juu;

(b) Ana elimu na uweledi katika moja wapo ya maeneo ya taaluma zifuatazo;

(i) Huduma ya Habari au;
(ii) Sheria au;
(iii) Utawala wa umma (Public Administration).

Hakuna sharti lolote katika sheria ambalo linataka mtu asiwe na zaidi ya miaka 45, hakuna sharti la kufanya kazi Serikalini na hakuna sharti la kuwa na cheo cha afisa mkuu. Haya masharti hayajawekwa na sheria bali yamewekwa na mwana JF anaitwa mnengene.
 
bora abaki mwanaharakati hivi hivi...wakimchukua na huyu ndo itakuwa basi tena...☹☹☹
 
Kuna Paschal Mayala wawili
1. Mwenye njaa
2. Asie na njaa
Hapa unamuongelea yupi?
1 mwenye njaa
2 Huyo alikuwa wa zamani akishusha mavitu hapa hadi Le mutuz ana subili comment zifike mia enzi zile bora ukose kula kuliko kukosa jamii forum,leo laki si pesa ana njaa balaa bado mawala ndio kabisa kuna jingine mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kuwa Dkt. Hassan Abbas ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ni ambayo ni nafasi yenye majukumu mengi na mazito ya kiutawala huku akiendelea kuwa Msemaji Mkuu wa Serikali, ni rai yangu kuwa Rais amteue Msemaji Mkuu wa Serikali mpya ili Dkt. Abbas apate muda wa kutosha wa kujikita katika nafasi yake ya Ukatibu Mkuu kikamilifu.

Kwa sasa Mitandao ya kijamii ina nguvu na ushawishi mkubwa sana kijamii, kisiasa na kiuchumi kuliko magazeti magazeti, online newspaper, online TV, radio and television Television Stations.

Nguvu na ushawishi wa mitandao ya kijamii kama vile WhatsApp, Facebook, Twitter, na Instagram katika nyanja za siasa, uchumi na kijamii unazidi kuongezeka kwa kasi kubwa kila siku.

Mara kadhaa Serikali, taasisi za Serikali, vyama vya siasa, taasisi za kidini, asasi za kiraia n.k zimejitokeza kujibu tuhuma, hoja, masuala na maswali ambayo yameibuliwa na mitandao ya kijamii na hiki ni kielelezo tosha cha nguvu ya mitandao ya kijamii.

Pia, tasnia ya habari imechangamana sana na teknolojia ya habari na mchangamano huu umeleta changamoto kadhaa za kisheria na za kiteknolojia kwenye sekta ya habari, hivyo, Msemaji Mkuu wa Serikali ambaye pia kwa mujibu wa sheria ni Mkurugenzi wa Idara ya Huduma ya Habari na Mshauri Mkuu wa Serikali wa Masuala ya Habari na Mawasiliano ya Kimkakati na Uchapishaji wa Habari anapashwa kuwa na ABCs za sheria na teknolojia ya habari na mawasiliano.

Hivyo basi, moja wapo ya sifa kubwa na muhimu ambaye Rais na washauri wake wanapashwa kuzingatia katika uteuzi wa Msemaji Mkuu wa Serikali ni uelewa na uzoefu wa kutosha katika nyanja ya mitandao ya kijamii na uelewa wa kiasi fulani sheria na teknolojia ya habari na hata mawasiliano.

Hivyo basi, kwa maoni yangu ninaona Paschal Mayalla wa JamiiForums anafaa kuvaa viatu vya Dkt. Hassan Abbas kwa kuwa ana uzoefu wa kutosha kwenye tasnia ya habari na ana added advantages kadhaa ikiwemo ya kuwa mwanasheria na kuwa uelewa na uzoefu mkubwa wa mitandao ya kijamii na ana ABCs za teknolojia ya habari na ni multi-knowledge au polymanth kwa maana ya kwamba ana maarifa na uelewa wa kiasi fulani ambao sio wa formal training karibu kila taaluma au tasnia kama vile siasa, historia, sheria, theolojia, lugha, soshiolojia, falsafa na kadhalika.

Watu ambao ni Polymanth au multi-knowledge ni viumbe adimu sana hapa duniani na hususani Tanzania na kwenye baraza la mawaziri Polymanth au multi-knowledge ni yuko mmoja tu Prof. Kabudi pekee.

Hivyo, Mhe. Rais ninakushauli kutumia mamlaka yako chaini ya Kifungu cha 4 (1) cha Sheria ya Huduma ya Habari, 2016, kumteua Ndugu Paschal Mayala kuwa Msemaji Mkuu wa Serikali, Mkurugenzi wa Idara ya Huduma ya Habari na Mshauri Mkuu wa Serikali wa Maswala ya Habari na Mawasiliano ya Kimkakati na Uchapishaji wa Habari.

Naomba kuwasilisha.
Mkuu Abeto Malakoti , kwanza salaam, pili asante sana kwa uzi huu, maana mtu au watu kukuona unafaa kwa nafasi fulani, hiyo ni heshima!, asante kuniheshimisha!, tatu huwezi amini, jf ni kubwa sana!, pamoja na watu kibao kunitag kwenye uzi huu, lakini amini usiamini, ndio nauona leo!.

Kwenye mfumo wa serikali kuna ajira za aina 4
1. Permanent pensionable- ni ajira kuu ya serikali mtu unaombakazi unaajiriwa permanent, unatakiwa kustaafu at 55 kwa hiyari au at 60 kwa lazima. Umri wa mwisho kwa ajira hii ni 45 years ili angalau ufanye kazi kwa miaka 15 kustahili pensheni.
2. Contract - hizi ni ajira za mkataba wa muda maalum, kama majeshi, polisi, magereza, zimamoto na ajira mbalimbali za kitaalamu, mfano mtu mwenye cheo cha luteni jeshini anatakiwa kustaafu na miaka 38, cheo cha captain ni miaka 47 etc. Hizi ajira za mkataba hazina cut of point, mtu anaweza kufikisha umri wa kustaafu kwa mujibu wa sheria, miaka 60, ila utaalamu wake bado unahitajika, anastaafu rasmi na kupewa mkataba wa miaka miwili miwili renewable once.
3. Appointment,- hizi ni ajira za uteuzi wa rais nazo zimegawanyika makundi mawili,
3.1 ni appointment za executives nafasi za kiutendaji, hizi zinafuata zile zinafuata kanuni Ama za permanent Ama za contracts kama wakurugenzi wakuu wa taasisi za umma, RC, DC, RAS, DED etc
3.2 Political appointees kama mawaziri, wenyeviti wa bodi, mabalozi, wabunge, mtu anaweza kuteuliwa na umri wowote.

Mimi ni mtu wa 60's, hivyo by the time bandiko hili linapanda ile 2020, I was already over 50!, sasa naitafuta 60!, hivyo nimeisha bypass sifa za kuteuliwa kwenye executives positions, asante sana kunipendekeza!.

Mimi ni mzalendo wa kweli wa nchi yangu, na nilijaribu kulitumikia taifa mara mbili, kwanza kupitia ubunge wa jimbo, kisha kupitia EALA, kote huko nilipungukiwa sifa hivyo sikuteuliwa na badala yake wakateuliwa watu wenye sifa kunizidi.

Mtu ukiwa ni mzalendo kwa taifa lako, utaendelea kulitumikia taifa lako hata bila uteuzi wowote, hivyo mimi naendelea kulitumikia taifa langu kupitia kalamu yangu kwa safu yangu ya Malala za "Kwa Maslahi ya Taifa" Amazon's zinachapishwa kwenye magazeti kadhaa, na zinakwenda sambamba na TV series zenye jina hilo hilo.

Makala hizo zimesaidia sana, unaweza kuzisoma baadhi hapa "Ombeni Mtapewa", "Tafuteni Mtapata", "Bisheni Hodi Mtafunguliwa" Je, Wajua Kuna "Kauli" na "Kauli Umba" Ambazo Huumba? Shuhudia

Msaada wangu mkubwa kwa nchi yangu na viongozi wetu ni kupitia mabandiko yangu ya "the voices from within" kama hii Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke
Hizo voices from within, sio sauti yangu ni sauti YAKE, inasaidia sana taifa wetu!.

Hivyo hata bila uteuzi wowote, mimi bado nipo na ninasaidia sana taifa langu.

Paskali
 
Kwa kuwa Dkt. Hassan Abbas ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ni ambayo ni nafasi yenye majukumu mengi na mazito ya kiutawala huku akiendelea kuwa Msemaji Mkuu wa Serikali, ni rai yangu kuwa Rais amteue Msemaji Mkuu wa Serikali mpya ili Dkt. Abbas apate muda wa kutosha wa kujikita katika nafasi yake ya Ukatibu Mkuu kikamilifu.

Kwa sasa Mitandao ya kijamii ina nguvu na ushawishi mkubwa sana kijamii, kisiasa na kiuchumi kuliko magazeti magazeti, online newspaper, online TV, radio and television Television Stations.

Nguvu na ushawishi wa mitandao ya kijamii kama vile WhatsApp, Facebook, Twitter, na Instagram katika nyanja za siasa, uchumi na kijamii unazidi kuongezeka kwa kasi kubwa kila siku.

Mara kadhaa Serikali, taasisi za Serikali, vyama vya siasa, taasisi za kidini, asasi za kiraia n.k zimejitokeza kujibu tuhuma, hoja, masuala na maswali ambayo yameibuliwa na mitandao ya kijamii na hiki ni kielelezo tosha cha nguvu ya mitandao ya kijamii.

Pia, tasnia ya habari imechangamana sana na teknolojia ya habari na mchangamano huu umeleta changamoto kadhaa za kisheria na za kiteknolojia kwenye sekta ya habari, hivyo, Msemaji Mkuu wa Serikali ambaye pia kwa mujibu wa sheria ni Mkurugenzi wa Idara ya Huduma ya Habari na Mshauri Mkuu wa Serikali wa Masuala ya Habari na Mawasiliano ya Kimkakati na Uchapishaji wa Habari anapashwa kuwa na ABCs za sheria na teknolojia ya habari na mawasiliano.

Hivyo basi, moja wapo ya sifa kubwa na muhimu ambaye Rais na washauri wake wanapashwa kuzingatia katika uteuzi wa Msemaji Mkuu wa Serikali ni uelewa na uzoefu wa kutosha katika nyanja ya mitandao ya kijamii na uelewa wa kiasi fulani sheria na teknolojia ya habari na hata mawasiliano.

Hivyo basi, kwa maoni yangu ninaona Paschal Mayalla wa JamiiForums anafaa kuvaa viatu vya Dkt. Hassan Abbas kwa kuwa ana uzoefu wa kutosha kwenye tasnia ya habari na ana added advantages kadhaa ikiwemo ya kuwa mwanasheria na kuwa uelewa na uzoefu mkubwa wa mitandao ya kijamii na ana ABCs za teknolojia ya habari na ni multi-knowledge au polymanth kwa maana ya kwamba ana maarifa na uelewa wa kiasi fulani ambao sio wa formal training karibu kila taaluma au tasnia kama vile siasa, historia, sheria, theolojia, lugha, soshiolojia, falsafa na kadhalika.

Watu ambao ni Polymanth au multi-knowledge ni viumbe adimu sana hapa duniani na hususani Tanzania na kwenye baraza la mawaziri Polymanth au multi-knowledge ni yuko mmoja tu Prof. Kabudi pekee.

Hivyo, Mhe. Rais ninakushauli kutumia mamlaka yako chaini ya Kifungu cha 4 (1) cha Sheria ya Huduma ya Habari, 2016, kumteua Ndugu Paschal Mayala kuwa Msemaji Mkuu wa Serikali, Mkurugenzi wa Idara ya Huduma ya Habari na Mshauri Mkuu wa Serikali wa Maswala ya Habari na Mawasiliano ya Kimkakati na Uchapishaji wa Habari.

Naomba kuwasilisha.
Yeye mwenyewe anasemaje
 
Back
Top Bottom