Pascal Mayalla kutoka kuwa Mwandishi Nguli hadi Mtangazaji wa kawaida East Africa Radio inamaanisha nini katika Tasnia?

Lionel Messi wa FC Barcelona ( La Pulga na Le Football Magician ) leo hii akiwa Kit Manager wa Yanga SC ya Tanzania Kwako Wewe ni sawa Ndugu?
Rivado alitoka huko akaenda kucheza Angola, mbona Charles katoka BBC sasa hivi yupo Azam anatangaza na kina Ivona? Kuna watu wana mahaba na fani zao ndugu! Ila aangalie asijechinganya akaitwa ' takataka' na kina Haji!
 
Mi mwenyewe mmojawapo, teknolojia imeharibu soko letu
 
kwani yy mwenyew anasemaje?
 
Tunaowasema hapa huwa tunawaomba Pesa za Kula au Wao huwa wanakuwa wametuomba pia? Mpuuzi Mmoja Wewe hebu nitokee hapa....!!
Unazidi kuonyesha ni namna gani ulivyomweupe kichwani..ulianzisha uzi ukiwa na mawazo hasi na ulitarajia wachangiaji watakuunga mkono. Naona umeishia kutoa maneno ya kejeli kwa wote ambao hatukuungi mkono.
Nikuulize swali.. Hivi karibuni Dangote na Mo Dewji wameteuliwa kuwa washauri wa uchumi wa serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kusini...Je nao utajiri wao umeisha? La hasha.
 
huyu jamaa toka aambiwa mayala ni njaa ameadhirika sana kisaikolojia.

pole sana Pascal Mayalla yatapita, kuna kupanda na kushuka, tupo pamoja.
 
Mayala najuwa utasoma ila mimi sikujui wala hunijui personal na wala sio muhimu ila kwa ukweli kabisa na naongea hili kwa dhati mjitahidi media kwa ujumla Tanzania na waandishi wetu wajenge uwezo na kuongea au kuuliza mambo katika upeo wa juu sio mambo ya kureport tu unachosikia bila kuchambua taarifa kwa haki na weledi. Na wala hapa sisemi jambo zuri ni kupinga serikali tu hapana mazuri yasemwe lakini yaulizwe yanayoweza kuboresha zaidi sijui kiswahili fasaha constructive criticism. Hata wapinzani waulizwe maswali magumu maana sisi tunawasema CCM lakini pia wapinzani wanatabia zileile mtu akiwauliza basi kishakuwa adui. Mimi sina utaalamu wa habari lakini naamini haya yanawezeka na hii itachangia nchi kwenda pazuri. Media yoyote ichukue hoja upande na pia ichukue upande mwingine balance stories halafu watu watajuwa u ukweli ni upi kwa bahati mbaya news channel zote akiitwa mgeni basi unajuwa huyu wa upande huu, najuwa hili sio jambo la mtu mmoja lakini nyinyi na wengine wengi tu hili linawezekana bila kuwa na uadui wala msichukue side, kwenye hili wa Kenya wametuacha na tusiachwe zaidi ya hapa. Media zetu sio mtu anakurupuka tu anaita press watu wamejaa hakuna hoja yoyote kuna watu hawastahili kupata hata coverage lakini mambo ya msingi hawako. Sina solution ya moja kwa moja katika hili ila ningependa kuona free press bila uadui.
 
Rivado alitoka huko akaenda kucheza Angola, mbona Charles katoka BBC sasa hivi yupo Azam anatangaza na kina Ivona? Kuna watu wana mahaba na fani zao ndugu! Ila aangalie asijechinganya akaitwa ' takataka' na kina Haji!
Haji alimlenga Shaffih Dauda.
 
huyu jamaa toka aambiwa mayala ni njaa ameadhirika sana kisaikolojia.

pole sana Pascal Mayalla yatapita, kuna kupanda na kushuka, tupo pamoja.
Bora yeye alijaribu na ni mtu pekee katika awamu ya tano alimface JPM kuuliza swali gumu hakuna mtu yoyote aliyethubutu kumuuliza JPM uso kwa uso wala hakuna kiongozi yoyote aliyethubutu katika hili. kwa kuwa alijaribu nampa sifa zake leo JPM amezikwa lakini kuna watu mpaka leo wanamuogopa. Simtetei Mayalla lakini katika atabaki kuwa ni mtu pekee alimpiga swali JPM ambalo JPM alichukia wengine wanasema wakiwa wamejificha. Alijaribu lakini mfumo wetu mgumu wala nchi usije kujifanya shujaa utapotezwa wakati ule unajiunga nao tu. Mbowe mwenyekiti wa chama alitiwa ndani na wanachama wenyewe waliufyata sembuse Mayalla.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…