Pascal Mayalla ndiye aliyemchongea Erick Kabendera kwa dola

👏🏽👏🏽👏🏽👏🏽👏🏽👏🏽👏🏽👊🏽👊🏽👊🏽👍🏽

 
Mkuu mbona povu linakutoka mpaka unarusha matusi kwangu? Kwanini ninyi wa aina yako mkishindwa hoja mnakimbilia matusi?
Najibu maswali yako ifuatavyo:
1. Rais Magufuli SI dikteta kwa kuwa alichaguliwa kwa kura za wananchi walio wengi.
2. Utawala wa Rais Magufuli haukiuki Katiba bali ni utawala wa sheria.
3. Rais Magufuli hakandamizi haki za binadamu. Uhuru upo mwingi tu ila uwe na mipaka.
4. Sekta binafsi iliyo halali inakuwa. Kipato cha mtanzania mzalendo asiye fisadi kinakua kila kukicha.

Sitakuita mwehu au mjinga au msukule au jina lolote la kukudhihaki au kukukebehi. Siamini katika matusi. Tuongee hoja hapa. Narudia, siungi mkono mtu yeyote kukosa dhamana. Kwa maoni yangu makosa yote yawe na dhamana. Lakini naunga mkono Serikali kuchukulia hatua za kisheria watu sampuli ya Eric Kabendera kwa kuwa maandiko yao ni hatari kwa usalama na ustawi na taifa na nchi yetu ya watu milioni 55. Kabendera hana tofauti na Hassan Ngeze wakati mauaji ya kimbari dhidi ya Tutsi. Walitumia Kangura na RTLM kueneza chuki dhidi ya Tutsi na wakawa wanatumika katika mauaji ya watu wasio na hatia. Walikuwa wapi The Economist au Human Rights Watch to stop the genocide against the Tutsi? Je, Eric Kabendera baba yake ni raia wa wapi?
 
Mkuu mbona povu linakutoka mpaka unarusha matusi kwangu?
Nimesema anayejifanya hafahamu yanayotokea ni mwehu na mjinga! Na kwa hakika, ikiwa hadi kesho unajifanya huyafahamu yanayotokea, basi mimi nitakuwa ndie mwehu na mjinga nikiwaita watu aina yako kwamba ni werevu!
Kwanini ninyi wa aina yako mkishindwa hoja mnakimbilia matusi?
Hoja ipi uliyoitoa?! Kwamba Kabendera anaweza kuwa Foreign Agent kisa tu anaikosoa serikali na rais?!
Najibu maswali yako ifuatavyo:
1. Rais Magufuli SI dikteta kwa kuwa alichaguliwa kwa kura za wananchi walio wengi.
Sasa nikikuita mjinga unalalamika! Ina maana ulivyofundishwa dikteta ni yule ambae hajachaguliwa na wananchi?Kama ndivyo ulifundishwa, basi ulidanganywa, nakupatia Britanica wanaokuambia kwamba
Dictatorship, form of government in which one person or a small group possesses absolute power without effective constitutional limitations.
Na kwa maana hiyo, Dictator anapatikana kutoka kwenye aina hiyo ya utawala!!
2. Utawala wa Rais Magufuli haukiuki Katiba bali ni utawala wa sheria.

Nimechukua eneo dogo sana la matumizi ya serikali! Msikilize hapo CAG halafu rudi tena hapa utuambie ikiwa utawala unaofuata sheria unaweza kufanya hayo!!
3. Rais Magufuli hakandamizi haki za binadamu. Uhuru upo mwingi tu ila uwe na mipaka.
Hivi hata hili nalo unatakiwa kukumbushwa kwamba Kabendera awali alikamatwa kwa hoja ya kutokuwa raia lakini bado waliendelea kumshikiria over 24 hours kinyume cha sheria hadi pale walipokuja kuibuka na hoja ya uendeshaji sijui wa mtandao wa kihalifu, uhujumu uchumi na utakatishaji fedha! Hivi unaamini rais anayejali haki za binadamu anaweza kuwa na utawala wa aina hiyo?! Au pia unatakiwa kukumbushwa kupitia influence ya Magu mwenyewe, Yusuf Manji alikamatwa na kupewa kesi za kipumbavu kabisa kama vile eti anahatarisha usalama wa taifa!!! Yaani hata aibu huoni wakati kila mmoja hadi sasa hafahamu ni wapi alipo Azory Gwanda aliyekuwa anafuatlia kile kilichoaminika matumizi mabaya ya nguvu za dola huko MKIRU!!! Yaani hata aibu huoni kwa hayo unayosema wakati ni mwaka wa pili huu Tundu Lissu bado anaendelea kuuguza majeraha baada ya kumiminiwa risasi kadhaa tena ndani ya nyumba za Bunge zenye ulinzi wa watu na kamera lakini hadi leo hakuna hata mmoja aliekamatwa! Mwaka wa 4 unaenda na bado haifahamiki Ben Saanane yupo wapi!! Hata vinyangatila kama akina ROMA Mkatoliki eti nao waliwahi kutekwa kisa tu wanaandika mashahiri yanayoikosoa serikali!!! Yote hayo, na mengine mengi yamefanyika under Magu Administration halafu tukisema wasioyaona haya watakuwa ni wehu na wajinga ndo uanze kulia lia!
4. Sekta binafsi iliyo halali inakuwa. Kipato cha mtanzania mzalendo asiye fisadi kinakua kila kukicha.
Unatia aibu aisee! Wakati National Bureu Statistics wanakanusha habari za JF ambazo kimsingi zinazungumzia kuporomoka kwa ajira sekta binafsi, NBS wanasema
Kwa upande mwingine, ajira 137,054 sawa na asilimia 25.0 ya ajira zote zilizozalishwa na Sekta Binafsi zimepungua kutoka ajira 239,017 mwaka 2016/17 hadi ajira 137,054
Na chini kabisa ya ukurasa wa 41 wa ripoti yao kuna jedwali linaonesha:-
Sasa hiyo sekta binafsi iliyo halali unayoisema wewe inakua ni ipi?! Na ikiwa ajira zinashuka, hiyo sekta binafsi yako inakua in terms of what?

Na NBS wanyewe walivyo vilaza, habari tuliyoijadili JF inadokeza kwamba:-
Ajira rasmi zilizotengenezwa na sekta binafsi zimepungua kutoka 239,017 mwaka 2016/2017 hadi kufikia ajira 137,054 mwaka 2017/2018.
halafu tena wanakuja kukanusha kwa kuandika kile kile kilichoandikwa JF!
Sitakuita mwehu au mjinga au msukule au jina lolote la kukudhihaki au kukukebehi. Siamini katika matusi.
Utaniitaje mwehu na mjinga wakati naona uhalisia kama ulivyo tofauti na wewe na wenzako mnaotaka kubishana hata na takwimu za serikali hiyo hiyo mnayoitetea!
Tuongee hoja hapa.
Kwenye post yangu nilihoji,

Lakini wewe ukaishia kusema:
Hapo hakuna hoja kwa sababu, jibu lako #1 jibu lake haliakisi tafsiri ya dikteta! Na mengine yaliyofuata yote, hayaakisi uhalisia huku mengine ukijaribu kutaka kubishana hata na takwimu za serikali yenyewe!!

Mwanzo tu wa post yangu nilikuuliza,
Hujajibu hilo swali!! Jibu hivi sasa!
 
We una matatizo sana!! Kwa mfano gani wa maana ulioutoa?! Yaani unafananisha alichokuwa ameongea Peter Arnett via enemy's state tv tena wakati nchi yake ipo vitani na kile anachoripoti Kabendera kwa kukosoa what's going on in time of "peace"?! Kwa mtindo huo, mtaua sana awamu hii manake the well-minded population will never ever keep quiet! Na ndio maana hata baada ya kumminia Tundu Lissu makumi ya risasi, kumpoteza Azory Gwanda na Ben Saanane, lakini bado watu hawajamaza, na katu hawatanyamaza!
 
I hope ni kupitia maelezo yangu ndo umemjua Peter Arnet. Toa shukrani kwangu! Hiyo ndo tunaita matumizi bora ya JF. Ukiondoa ubishi unaweza kujifunza mengi toka kwetu tunaokuzidi uelewa.

Don't be a pedant person in daily life. At times, yes! At times, No! We are not doing body painting over here. The example of Peter Arnett I gave you should not be taken literary, rather deductively. There you see the logic of dealing with irresponsible citizens wherever they are. When you have stupid creatures who trade blasphemy hoping to receive words of thanks from outside their society, then it's time to deal with them equally, stupidly.
 
Hiyo ni tuhuma nzito sana. Bwana Mayalla sijawahi kuonana naye ila nilikuwa ninamfuatilia tangu enzi zile. ninavyofahamu mimi ni kuwa huyu bwana ni mchokozi na maandiko yake mengi yana mantiki. Kumsingizia kama ulivyofanya bila kutupa uthibitisho siyo sawa kabisa. Lete madini ili nasi tuweze changia inavyostahili.
 
Wewe mwenyewe hapo tayari una ukabila. Kwani gazeti linapoandikwa halitakiwi kusomwa na makundi yote hadi umlaumu Paschal Mayallah kwamba ndo aliwaamsha usalama kusoma hiyo habari ya Kabendera kwenye gazeti la The Economist?. Acha Uhaya yeye viachie vyombo vya dola vifanye kazi yake.
 
Unachekesha sana. Seriosuly unaamini ni peke yako unayemfahamu huyo Peter Arnett?! Ni kipi kinachokufanya udhani ni peke yako unayemfahamu huyo jamaa?! Au kwavile unapenda sana kutumia Kiingereza ndo unadhani unajua kuliko wengine?!

Man, nenda kapekue kule International Forum uone ni mara ngapi nimeshiriki kikamilifu kwenye mijadala ya International and Geo-politics za US-Russia-Middle East Politics!! Pekua uone ni mara ngapi nime-fully participate kwenye China-US Trade and Politics!!! Kwahiyo ni ushamba wa hali ya juu kudhani kumfahamu/kumsikia Peter Arnett unayeshindwa hata ku-spell jina lake sawasawa, ni kitu special sana!!!!

Btw, ni nini kinachokufanya uamini unanizidi uelewa?! I mean no disrespect lakini humu JF sijawahi kuona ukijadili jambo lolote la maana zaidi ya kutetea mfumo wa kidhalimu!! Au hivyo Viingereza vyako unavyopenda kuvitumia kial wakati ndo vinakufanya udhani una uelewa mkubwa? Yaani nyie wana-Lumumba ni kansa kubwa sana kwa taifa, sawa na Rais wako anayedhani kuwa na PhD ndo kujua kila kitu!!
 
Para ya mwisho umeharibu
 
Unatumia nguvu nyingi sana kujipa uhalali wa hapa JF. Unaweza kumfahamu Arnet au uli google ukamfahamu. Lakini nahisi hukujua chochote. Ungekuwa unafahamu hilo, usingeandika yaliyotangulia. Ni kama ulikuwa ignorant na dunia hii.

Kama huna ignorance, basi una udhaifu wa kusahau kama viumbe wengine walivyo.
 
Hoja yako imejaa ubinafsi.
ni vema ungerejea mengi yaliyowahi/kwisha ibuliwa humu na serikali ikayachukulia hatua stahiki ndio uone kuwa Pasco hana baya alilikusudia zaidi ya kuweka uzalendo na kuitetea nchi.
 
Angalia ulivyo lofa!!! Eti natumia nguvu kujipa uhalali hapa JF!! Uhalali wa nini?! Nijipe uhalali kupitia wewe ambae unaonesha wazi hujui lolote na upo hapa kutetea mfumo dhalimu?! Btw, nini nilichondika kinachowiana na Arnett hata useme lau kama ningemfahamu basi nisingeandika?! Ni wewe na ujinga wako ndo maana ulimlinganisha Peter Arnett na Kabendera wakati ni vitu viwili tofauti!! Kama sio ujinga, hebu eleza hapa ni kipi kinachomfanya Eric Kabendera alinganishwe na Arnett kupitia kazi zao?!

Hivi we mzee mbona mshamba sana wewe??!!! Of all people, why Arnett?!Kwanza kwa jinsi unavyoongea, napata shaka ikiwa hata huyo Peter Arnett mwenyewe umewahi kumfuatilia zaidi ya kujua habari zake juu juu hasa kwavile blunder yake ya Iraq ilitangazwa sana!!!
 
Bandiko zuri Sana limejaa majungu na uzuzu wa uchambuzi, ili niungane na wewe naomba unifaamishe yafuatayo
Ndugu yetu kabendere amekamatwa na kosa gani?
Ndugu yetu Kabendere makosa yake yaliyomfanya awemahakamani ni yapi?
Na kama unayosema ni kweli ni makosa mtu kwenda kutoa taarifa polisi kuwa ndugu yake ni jambazi na muuaji?
 
Acha matusi basi! Kutukana ni kujidhalilisha. Si unajua JF inaweza kukupiga ban? Umesoma taratibu za JF, au hujali? Unatukana mtu ambaye humfahamu. Unamuita mzee mtu ambaye hata humfahamu. Alichokifanya Arnet siyo blunder kama ulivyoandika, labda kama una maana tofauti ya neno blunder.

Ichukuwe JF kama Dunia. Sehemu ambayo kuna wanaokuzidi uwezo, sehemu unayoweza kujifunza mapya. Ukihangaika kuonesha kwamba unawazidi wote utapoteza nafasi ya kujifunza. Hata kufikiri ni jambo la kujifunza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…