Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Leo tarehe 02 Agosti 2021, waandishi wa vyombo mbalimbali vya Habari walipata chanjo dhidi ya UVIKO 19 pale Karimjee Dar.
Miongoni mwa waliopokea chanjo ni mwandishi nguli Pascal Mayalla. Katika mahojiano aliongea jambo muhimu sana kuhusu hili zoezi la chanjo.
Amewataka viongozi wote wa umma kujitokeza kuchanja na kama wapo wasiopendelea basi wanyamaze kimya. Kwa sababu chanjo inahusu nchi nzima na wanapaswa kuonyesha uwajibikaji wa pamoja.
Ameenda mbali zaidi kwamba, kama yupo kiongozi anapiga zoezi hili basi ajiweke pembeni yaani ajiuzulu kisha aanze kupinga zoezi hili.
Ninaona ni point muhimu sana katika kuhamasisha kinga dhidi ya UVIKO 19. Lakini pia kwenye kijiwe chetu cha Alkasusu wapo wanaodai Pasco analinyemelea tena jimbo la Kawe.
Lakini yote heri