#COVID19 Pascal Mayalla: Viongozi wa Umma wajitokeze kuchanjwa, wasiopenda wakae kimya

#COVID19 Pascal Mayalla: Viongozi wa Umma wajitokeze kuchanjwa, wasiopenda wakae kimya

Leo tarehe 02 Agosti 2021, waandishi wa vyombo mbalimbali vya Habari walipata chanjo dhidi ya UVIKO 19 pale Karimjee Dar.

Miongoni mwa waliopokea chanjo ni mwandishi nguli pasco Mayala. Katika mahojiano aliongea jambo muhimu sana kuhusu hili zoezi la chanjo.

Amewatala viongozi wote wa umma kujitokeza kuchanja na kama wapo wasiopendelea basi wanyamaze kimya. Kwa sababu chanjo inahusu nchi nzima na wanapaswa kuonyesha uwajibikaji wa pamoja.

Ameenda mbali zaidi kwamba, kama yupo kiongozi anapiga zoezi hili basi ajiweke pembeni yaani ajiuzulu kisha aanze kupinga zoezi hili.

Ninaona ni point muhimu sana katika kuhamasisha kinga dhidi ya UVIKO 19. Lakini pia kwenye kijiwe chetu cha Alkasusu wapo wanaodai Pasco analinyemelea tena jimbo la Kawe.

Lakini yote heri

NA WAO WANAOCHANJA WAKAE KIMYA SIYO KUWANANGA WASIOCHANJA.... AU WANAOPINGA KUCHANJA. Mbona wao Serikali walisema Barakoa za nje si salama na hawakunangwa .?
 
Hii ni nchi huru ambapo kila mtu yuko huru kusema chochote bila kuathiri sheria za nchi. Kama wao wanatangazia wengine kwenda kuchanjwa, kwanini tusiochanjwa tukiwatangazia wenzetu kutochanjwa inakuwa nongwa?

Kama hawataki watu kuhamasishana kukataa chanjo waanze wao kusitisha kampeni ya kuwambia wengine wakachanje. Kila kundi likae kimya. Thats all
 
maambukizi yanaongezeka, vipi kuhusu vifo vya wakati huu wa chanjo na kabla ya chanjo?
Hata Wakati huu pia vifo vinzidi kuongezeka sema tupo kipindi ambacho tushazoea hii hari hata tukiona habari za vifo hatuchukulii kwa uzito huo, kama covid-19 ilivo ingia kwa mara ya kwanza. That why tunaona kawaida tushazoea hayo mapito
 
kwakweli ukiwa na magonjwa hatari kama Ukimwi, Moyo, Sulari, TB, Presha ni bora upate chanjo mapema maaana ukichelewa unahatarisha uhai wako.
 
wagonjwa wa,
1.KISUKARI
2.PRESHA
3.MOYO
4.SARATANI
5.UKIMWI
wagonjwa wa maradhi hayo wanapaswa wachue tahadhari sana maana Corona itatumaliza sana.
 
Back
Top Bottom