#COVID19 Pascal Mayalla: Viongozi wa Umma wajitokeze kuchanjwa, wasiopenda wakae kimya

#COVID19 Pascal Mayalla: Viongozi wa Umma wajitokeze kuchanjwa, wasiopenda wakae kimya

Mbona hii Chanjo imeingizwa kwenye Siasa wakati ni jambo muhimu la kutolewa ufafanuzi kama anavyofanya Gwajima ambae ni opposer sasa wale proposer wanatakiwa watetee kwa hoja na sio Mipasho
Gwajima inatakiwa afunguliwe kasi ya kuujumu uchumi
 
Leo tarehe 02 Agosti 2021, waandishi wa vyombo mbalimbali vya Habari walipata chanjo dhidi ya UVIKO 19 pale Karimjee Dar.

Miongoni mwa waliopokea chanjo ni mwandishi nguli Pascal Mayalla. Katika mahojiano aliongea jambo muhimu sana kuhusu hili zoezi la chanjo.

Amewataka viongozi wote wa umma kujitokeza kuchanja na kama wapo wasiopendelea basi wanyamaze kimya. Kwa sababu chanjo inahusu nchi nzima na wanapaswa kuonyesha uwajibikaji wa pamoja.

Ameenda mbali zaidi kwamba, kama yupo kiongozi anapiga zoezi hili basi ajiweke pembeni yaani ajiuzulu kisha aanze kupinga zoezi hili.

Ninaona ni point muhimu sana katika kuhamasisha kinga dhidi ya UVIKO 19. Lakini pia kwenye kijiwe chetu cha Alkasusu wapo wanaodai Pasco analinyemelea tena jimbo la Kawe.

Lakini yote heri
Waziri wa Afya, Dorothy Gwajima karudi na rungu.

Ametoa rai kuwa viongozi ambao mpaka sasa hawajachanjwa, watatakiwa waachie ngazi kwani hawawezi kusimamia kampeni ya kusimamia uchanjwaji dhidi ya corona.

Waziri wa Afya amesema kama Rais kachanja ili iwe mfano, sasa hao viongozi hawatetei msimamo wa Serikali

Tulisha liona hili huko nyuma: #COVID19 - Kuchanja sasa kuwe lazima, hasa wafanyakazi serikalini. Chanja au achia ngazi

View attachment 2028866
Naunga mkono hoja, hiki alichokisema Waziri Gwajima, ni kitu cha kweli, kama serikali yako imekubali chanjo na rais wako kachanja, wewe kiongozi wa umma, lazima uonyeshe uongozi kwa vitendo na kwa mfano, kwa viongozi wote wakuu wa umma lazima wachanje hadharani, ule uhiari, hauwahusu viongozi wa umma, kwa viongozi wa umma kuchanja ni lazima, asiyechanja aachie ngazi!.

Niliwahi kusema mahali, chanjo ya Korona japo inasemwa kuwa ni hiyari, hii ni hiyari ya lazima, kuna nchi mtu huruhusiwi kuingia bila cheti cha chanjo ya Corona. Hivyo sasa tunaanza mdogo mdogo kwa viongozi wa umma, chanjo sio hiyari ni lazima,
kama wewe ni kiongozi wa umma na huamini chanjo, achia ngazi!.
P.
 
Leo tarehe 02 Agosti 2021, waandishi wa vyombo mbalimbali vya Habari walipata chanjo dhidi ya UVIKO 19 pale Karimjee Dar.

Miongoni mwa waliopokea chanjo ni mwandishi nguli Pascal Mayalla. Katika mahojiano aliongea jambo muhimu sana kuhusu hili zoezi la chanjo.

Amewataka viongozi wote wa umma kujitokeza kuchanja na kama wapo wasiopendelea basi wanyamaze kimya. Kwa sababu chanjo inahusu nchi nzima na wanapaswa kuonyesha uwajibikaji wa pamoja.

Ameenda mbali zaidi kwamba, kama yupo kiongozi anapiga zoezi hili basi ajiweke pembeni yaani ajiuzulu kisha aanze kupinga zoezi hili.

Ninaona ni point muhimu sana katika kuhamasisha kinga dhidi ya UVIKO 19. Lakini pia kwenye kijiwe chetu cha Alkasusu wapo wanaodai Pasco analinyemelea tena jimbo la Kawe.

Lakini yote heri
Wito huu ni muhimu sana, kilichobaki ni CCM kuonyesha uwezo wa kuwashikisha adabu.

Mtu huwezi kumdharau rais wa JMT na Mwenyekiti wa CCM. Najua wote watapiga magoti kuomba msamaha, nashauri kwa Polepole na Gwajima, msamaha wao iwe ni kuchanja hadharani, kisha wawahamasishe wafuasi wao kuchanja. Jerry Slaa asamehewe tuu bila masharti.
P
 
Back
Top Bottom