#COVID19 Pascal Mayalla: Viongozi wa Umma wajitokeze kuchanjwa, wasiopenda wakae kimya

Mbona hii Chanjo imeingizwa kwenye Siasa wakati ni jambo muhimu la kutolewa ufafanuzi kama anavyofanya Gwajima ambae ni opposer sasa wale proposer wanatakiwa watetee kwa hoja na sio Mipasho
Gwajima inatakiwa afunguliwe kasi ya kuujumu uchumi
 
Naunga mkono hoja, hiki alichokisema Waziri Gwajima, ni kitu cha kweli, kama serikali yako imekubali chanjo na rais wako kachanja, wewe kiongozi wa umma, lazima uonyeshe uongozi kwa vitendo na kwa mfano, kwa viongozi wote wakuu wa umma lazima wachanje hadharani, ule uhiari, hauwahusu viongozi wa umma, kwa viongozi wa umma kuchanja ni lazima, asiyechanja aachie ngazi!.

Niliwahi kusema mahali, chanjo ya Korona japo inasemwa kuwa ni hiyari, hii ni hiyari ya lazima, kuna nchi mtu huruhusiwi kuingia bila cheti cha chanjo ya Corona. Hivyo sasa tunaanza mdogo mdogo kwa viongozi wa umma, chanjo sio hiyari ni lazima,
kama wewe ni kiongozi wa umma na huamini chanjo, achia ngazi!.
P.
 
Wito huu ni muhimu sana, kilichobaki ni CCM kuonyesha uwezo wa kuwashikisha adabu.

Mtu huwezi kumdharau rais wa JMT na Mwenyekiti wa CCM. Najua wote watapiga magoti kuomba msamaha, nashauri kwa Polepole na Gwajima, msamaha wao iwe ni kuchanja hadharani, kisha wawahamasishe wafuasi wao kuchanja. Jerry Slaa asamehewe tuu bila masharti.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…