Paschal Mayala aepuke dharau dhidi ya Lissu Jembe Letu

Paschal Mayala aepuke dharau dhidi ya Lissu Jembe Letu

Na kwa sababu hii pekee "wananchi wa Tanzania" wako tayari kuunga mkono sera ya "no reform no election
Perish the thought . you really expect anything from these stupid Tanzanians? All they do all day is run their mouths about Simba and Yanga games. Aise, you better switch up that mindset!
 
Inatakiwa iwe nini ili ikubarike na sheria?

Wasemavyo Chadema Kuhusu kaulimbiu ya "Bila mabadiliko, Hakuna uchaguzi"

Kulingana na taarifa zilizoko kwenye hotuba za Tundu Lissu, Mwenyekiti wa Chadema, mawazo yafuatayo yanawakilisha msimamo rasmi wa Chadema kuhusu sababu za kaulimbiu ya “Mabadiliko Kwanza, Uchaguzi Baadaye.”

1. Takwimu za uchaguzi wa serikali za mitaa kati ya mwaka 2014 na 2019 zinathibitisha kwamba kwa mujibu wa utaratibu wa sasa wa kisheria, kikanuni, kikatiba na wa kiserikali, uchaguzi salama usioambatana na mauaji, ulio huru, wenye uwazi na unaofanyika kwa haki hauwezekani tena kufanyika ktk nchi hii. Takwimu ziko hivi:

(a) Katika uchaguzi wa mitaa na vijiji wa 2014: Jumla ya vijiji vilikuwa 11,748; CCM ilishinda vijiji 9,378 (80%); na CHADEMA vijiji 1,754 (15%). Jumla ya mitaa yote ilikuwa 3,875; CCM ilishinda mitaa 2,583 (67%); na CHADEMA ilishinda mitaa 980 (25.29%).

(b) Katika uchaguzi wa vijiji na mitaa 2019: Jumla ya vijiji ilikuwa 12,262; CCM ikashinda 12,260 (99.99%); na CHADEMA haikutajwa kabisa. Jumla ya mitaa nchini 4,263; CCM ikashinda mitaa 4,263 (100%); na CHADEMA haikutajwa kabisa.

(c) Katika uchaguzi wa vijiji na mitaa mwaka 2024: Jumla ya vijiji ni 12,271; CCM ikashinda vijiji 12,150 (99%); na CHADEMA ikashinda vijiji 97 (0.79%). Jumla ya mitaa ni 4,264; CCM ikashinda mitaa 4,213 (99%); na CHADEMA ikashinda mitaa 36 (0.84%).

2. Takwimu hizi maana yake ni kuwa, mfumo wetu wa uchaguzi wa sasa unayo matatizo mengi, kiasi kwamba, bila kufanyika kwa mabadiliko ya kisheria, kikanuni na kikatiba, kwanza, basi chaguzi za kiinimacho zenye kuwaumiza wapinzani na kuipendelea CCM zitaendelea milele kwa sababu zilizo wazi.

(a) Mosi, chaguzi za mwaka 2019, 2020 na 2024 zimeweka rekodi za kuenguliwa kwa wagombea wengi wa vyama vya upinzani kwa vigezo visivyo vya kikatiba, mfano kukosea jina, na kukosea kuandika jina la chama. Lakini wagombea wote wa CCM wanabakizwa kwa madai kuwa wao hawana dosari yoyote.

(b) Mfumo wa sasa wa uchaguzi ni mfumo wenye sura ya siasa za chama kimoja. Ulitengenezwa na CCM, kwa ajili ya CCM, unaifaidisha CCM na kwa sababu hiyo si mfumo wa kidemokrasia na unawaumiza wananchi na nchi yote.

(c) Ni mfumo wa CCM kwa kuwa, uchaguzi mkuu unasimamiwa na Tume ya Uchaguzi ambayo ni ya CCM ambayo huteuliwa na kupewa maelekezo na Mwenyekiti wa CCM ambaye mara zote huwa ndiye Rais wa nchi.

(d) Aidha, Mwenyekiti wa CCM ambaye naye mara zote huwa ni mshiriki na mshindani ktk uchaguzi ndiye anayeteua Mwenyekiti wa Tume, wajumbe wote wa Tume na mkurugenzi wa uchaguzi wa Tume. Ndiye mwajiri na mteuzi wa wasimamizi wa uchaguzi wa majimbo (wakurugenzi wa halmashauri za miji, wilaya, manispaa na majiji), watendaji wa kata na wa vijiji. Katika mazingira haya, hawa kamwe hawawezi kutenda haki Bpbali watampendelea aliyewateua.

(e) Mfumo wa ugawaji majimbo ya uchaguzi sio wa haki kwa kuwa hauzingatii idadi ya watu ambao ni wakazi. Maeneo ambayo CCM ina uhakika wa kushinda imeyagawa katika vijimbo vingivingi Ili mradi iingize wabunge wengi bungeni. Mfano Dar Es Salaam yenye wapiga kura wengi 3,427,000, ambazo ni takwimu za Tume ya Uchaguzi za mwaka 2020, iko sawa na wapiga kura wa mikoa ya Rukwa, Pwani, Songwe, Iringa, Katavi na Njombe kwa pamoja. Lakini DSM ina majimbo 10 tu, sawa na na wastani wa wapiga kura 327,000 kila jimbo la Dar. Lakini, katika mikoa hiyo sita (6) kwa ujumla ikiwa na majimbo 37, kuna wastani wa wapiga kura 91,000 katika kila Jimbo. Wapiga kura 91,000 katika kila Jimbo kwenye mikoa hiyo ni mara 3.5 ya wapiga kura 327,000 katika jimbo la Dar. Hakuna usawa hapo.

(f) Kwa upande wa Zanzibar, majimbo ya uchaguzi yana wastani wa wapiga kura 10,000. Hii maana yake ni kwamba mbunge kutoka Zanzibar anaweza kuchaguliwa na watu wasiozidi 2,500 akaja Dodoma na akawa na haki sawa na mbunge anayehudumia wapiga kura 327,000 mkoani Dar Es Salaam. Hakuna usawa hapo.

3. Kwa hiyo, hitimisho la ikimantiki ni kwamba, Watanzania tunapaswa kuzuia chaguzi za kiinimacho zisifanyike kwa kujenga hoja kwa wananchi, wanachama wetu, taasisi za kiraia na za kidini, viongozi wa dini, nchi wahisani wa Tanzania, taasisi za haki za kibinadamu za kitaifa na kimataifa hadi waelewe na kutuunga mkono. Hii ndio maana ya msemo kwamba “Mabadiliko Kwanza, Uchaguzi baadaye,” yaani “No Reforms, No Election.

4. Kutokana na hitimisho hapo juu, mapendekezo ya msingi kuhusu mabadiliko yanayotakiwa kufanyika kwa sasa yanapatikana kwenye Ripoti za Tume mbalimbali. Kuna Tume ya Jaji Francis Nyalali (1991) iliyoundwa na Rais Hayati Ally Hassan Mwinyi; Tume ya Jaji Robert Kissanga (1998) iliyoundwa na Rais Hayati Benjamin Mkapa; Tume ya Jaji Mark Bomani (2003) iliyoundwa na Rais Hayati Benjamin Mkapa; na Tume ya mabadiliko ya Katiba ya Jaji Joseph Sinde Warioba (2014/2015) iliyoundwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete. Tume hizi zote zilipendekeza mabadiliko yafuatayo:

(a) Lazima tuwe na Tume Huru ya uchaguzi yenye Mwenyekiti na wajumbe wake wanaoteuliwa na mtu baki badala ya Rais; yenye bajeti inayojitegemea kutoka Bungeni kwa ajili ya kuendesha shughuli zake; yenye wafanyakazi wake wa kudumu na wa mikataba ya muda mfupi/maalumu inayowajiri yenyewe wakiwajibika kwa Tume pekee; na yenye wasimamizi wa vituo vya kupigia kura hadi kwa Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na wakurugenzi wa Tume wasiowajibika kwa Rais.

(b) Ugawaji wa majimbo lazima ufanyike upya kwa kuzingatia kigezo cha idadi ya watu kama ilivyokuwa katika sheria za uchaguzi na katiba kuanzia mwaka 1961 hadi 1991. Kigezo cha miumdombinu na jiografia ya eneo hakifai.

(c) Daftari la wapiga kura litengenezwe upya kwa kuandikisha wapiga kura wote upya kwa kuondoa wapiga kura hewa wote. Aidha, daftari la wapiga kura lisiwe Siri Bali lazima liwe wazi (accessible) kwa yeyote anayetaka kuliangalia Ili mradi kuweka utaratibu rahisi na wa wazi kufanya hivyo.

(d) Utaratibu wa kuengua wagombea wote iwe wa CCM, CHADEMA au chama chochote kwa sababu ambazo si za kikatiba ukomeshwe na kupigwa marufuku na sheria tutakazotunga.

(e) Utaratibu wa vyombo vya dola kuwafanyia vurugu wagombea wa vyama pinzani na CCM upigwe marufuku na sheria na sheria iweke utaratibu wa kuwashitaki, kuwalipisha fidia na kufukuzwa kazi mwenye mamlaka yeyote atakayetumia mamlaka yake vibaya kwenye eneo hili.

(f) Barua rasmi tu ya chama cha siasa ambako wakala anatoka ili kusimamia kura za mgombea wake inatosha kumfanya wakala atambuliwe na msimamizi wa kituo cha uchaguzi. Hivyo, utaratibu wa Sasa wa mawakala wa wagombea wa vyama vya siasa kuapishwa kiapo cha kutunza siri ni batili na hauna sababu na unaleta urasimu usio na maana yoyote kwa sababu kwenye kituo cha kupigia kura hakuna Siri ya kutunzwa hapo kwa sababu kila kitu kinatakiwa kufanyika kwa uwazi huku kila mtu akiona.

(g) Utangazaji wa matokeo ya uchaguzi kwa nafasi zote kuanzia kwenye kituo cha kupigia kura ufanyike tu pale ambapo mawakala wa wagombea wote wameridhika na kusaini fomu za matokeo. Kwenye kituo cha majumuisho matokeo yatangazwe pale tu ambapo wagombea wote wameridhika na kusaini fomu ya matokeo. Kama mgombea au wakala wa mgombea hajaridhika kwa sababu yoyote sheria iseme ni marufuku kwa msimamizi wa kituo kutangaza matokeo hayo. Na ikitokea hivyo, basi mgogoro wa namna hiyo uende mahakamani kuamuliwa.
 

View attachment 3247924
Paschal Mayalla

Paschal Mayala, ameandika makala yenye kichwa cha maneno “Wapinzani wasaidiwe kuachana na siasa za hadaa," katika gazeti la Nipashe, toleo la Jumapili, tarehe 23 Februari 2025, ukurasa wa saba (7), chini ya safu ya “Fikra Mbadala.”

Hoja ya Mayalla

Kimsingi, hoja ya Mayala inaweza kufupishwa kwenye matamko matano yafuatayo:

  1. Lissu anapoulizwa kuhusu maandalizi ya uchaguzi ndani ya chama chake yanaendeleaje, anasema kuwa Chadema haifanyi maandalizi yoyote ya uchaguzi kabla ya mabadiliko ya kimfumo, yaani ‘no reform no election’ na sio vinginevyo.
  2. Lakini, Tundu Lissu na Chadema yake hawana “uwezo” wa kuzuia uchaguzi mkuu kufanyika mwaka huu wa 2025, iwe ni kwa kujenga hoja sanaifu au kutumia mabavu.
  3. Kwa hiyo, sera ya “no reform no election” inayohubiriwa na Tundu Lissu ni “siasa za hadaa,” maana haziendani na uhalisia wa kisiasa uliopo nchini Tanzania.
  4. Siasa ambazo haziendani na uhalisia wa kisiasa uliopo nchini zinapaswa kupuuzwa na kila mtu makini.
  5. Kwa hiyo, siasa za hadaa kama vile sera ya “no reform no election” zinazohubiriwa na Tundu Lissu zinazopaswa kupuuzwa na kila mtu ikiwemo CCM na serikali yake, mpaka hapo wapinzani watakapokuwa tayari kuendana na uhalisia kwa kufanya “real politics.”
Uchambuzi wa hoja ya Mayala

Hoja ya Mayala ni potofu kimantiki kuanzia kwenye dokezo la pili hapo juu, kama nitakavyoeleza hapa chini:

Raia yangu ni kwamba, Tundu Lissu na Chadema yake wanao “uwezo” wa kuzuia uchaguzi mkuu kufanyika mwaka huu wa 2025 kwa njia ya kujenga hoja sanifu hata bila kutumia mabavu. Hoja ya Lissu ni kama ifuatavyo:

  1. Tangu mwaka 2014 Tanzania tumekuwa tunafanya uchaguzi unaokiuka kanuni za haki, uhuru, ushindani na uwazi.
  2. Tumekuwa tunafanya uchaguzi unaokiuka kanuni za haki, uhuru, ushindani na uwazi kwa sababu ya ubovu uliomo kwenye Katiba, sheria, na kanuni za uchaguzi zilizopo.
  3. Hivyo, bila mageuzi ya Katiba, sheria, na kanuni za uchaguzi hakuna uchaguzi unaoheshimu kanuni za haki, uhuru, ushindani na uwazi unaoweza kufanyika nchini Tanzania.
  4. Lakini, Watanzania wengi wanataka tufanye uchaguzi unaoheshimu kanuni za haki, uhuru, ushindani na uwazi.
  5. Kwa hiyo, bila kushurutishwa na yeyote kwa njia ya mabavu, tunapaswa kusogeza mbele ratiba ya uchaguzi mkuu wa 2025 ili kupisha mageuzi ya kimfumo yanayotakiwa na umma wa Watanzania.
Hitimisho na mapendekezo

Paschal Mayala aachane na siasa za hadaa, akubali ukweli mchungu kwamba Tanzania ni dola ambayo ni Jamhuri ya KIkatiba na Kidemokrasia isiyopaswa kunajisiwa na wanasiasa matapeli wanaiba uchaguzi mchana kweupe.

Pia aache dharau kwa Lissu Jembe la Kimataifa na aepuke utapeli wa kucheza na maneno dhidi ya Watanzania.

Kama akijifunza kutofautisha maana za maneno "uwezo" na "uwezekano" atagundua kwamba sera ya ‘Hakuna Uchaguzi Kabla ya Mabadiliko’ inawezekana

Nawasilisha.
Paschal anaogopa sana uzee unaomshambulia kwa kasi anahitaji kupata wataalamu kutoka Mirembe hospitali
 
Hatuko tayari kushiriki uchafuzi sio uchaguzi .kwa hiyo nanukuu, nape alisema ccm hawategemei kura ktk sanduku la kura . Bali wananjia nyingine za ushindi wao wakimaliza Wana muomba mungu Hawa samehe ktk wizi wao wa kura
 
ili kumsaidia Mayala kuachana na tabia ya kuparamia mambo yaliyo nje ya uwezo wake.
Dokta Mama Amoni, asante kunianzishia thread, bandiko hili ndio nimeliona leo.

Limenisaidia sana, nimebadilika sasa namheshimu TAL, na sita paramia tena haya mambo makubwa yaliyo nje ya uwezo wangu.

Mambo ya uwezo wangu ni kama haya, Uliwahi kula vyakula gani kutoka sehemu mbalimbali Duniani ukafaidi? kufuatia urefu wa bandiko lako, limenisababishia njaa fulani, ya kula chakula fulani!.

Something is telling me wewe ni mtu wa Bukoba, kama sio, then you have the traits za huko. Kama nimepatia, then ...
Kama nimekosea sorry just have a good day!.

P
 
Back
Top Bottom