Mimi kwa maoni yangu naweza kusema P. Mayala ni miongoni mwa Waandishi wa Habari wachache Wakongwe kwenye tasnia ya Habari. Waliokuwa wakijituma kwa kupenda kazi zao. Walifanya kazi kwa weledi mkubwa. Achana na hawa wasaka fursa/manoti.
Pascal aliwavutia watu wengi miaka ya nyuma hasa kwa kipindi chake maarufu cha KITI MOTO kilichokuwa kikirushwa hewani kupitia ITV na Radio One. Na alifanikiwa sana kujijengea umaarufu wakati ule.
Kwa kadri miaka ilivokuwa ikisonga mbele, Wanasiasa walianza kuvitumia Vyombo vya Habari kwa manufaa yao binafsi. Wako waliofanikiwa na pia walioshindwa kwa kutofikia makubaliano navyo.
Wale walioshindwa hasa kutoka Chama kile walianza kuvichongea Vyombo vile kwa Serikali. Ndiyo vikaanzishwa Sheria lukuki kuvibana Vyombo vile. Kupitia Sheria na kanuni zile wengi waliumizwa.
Hapo ndipo pakaanza kuzaliwa hivi vitabia vya kupidisha habari kuwa favour Wanasiasa fulani wa Chama kile. Wale wachache walioamua kusimamia kanuni yaani ku balance story wakaanza kushughulikiwa. Wapo waliopotezwa, waliouawa na wengine kusababishiwa ulemavu wa macho kwa kumwagiwa tindikali.
Pascal kama binadamu mwingine kaona isiwe taabu. Kama nimewashindwa kwa kutumia vema kalamu yangu, basi acha niungane nao. Baada ya kuungana nao bado nafsi yake ilimsuta na kujaribu kurudi nyuma. Yaani alipokumbuka Uzalendo kwa Nchi yake. Hapo usumbufu huanza kutoka kwa wale wa Chama kile. Kutaka kumkosesha mkate wake wa kila siku.
Pascal siyo mtu wa tamaa. Hana wivu wala chuki. Anapenda kuwa Mwalimu kwa kile anachokifahamu kwa yeyote yule mwenye uhitaji bila kuangalia itikadi, kabila wala imani. Labda tamaa ya kuishi.
Nayasema haya toka moyoni mwangu kwani namfahamu fika P. Kulikuwa kuna Club maarufu iliyokuwa Sinza Makaburini. Miaka hiyo tulikuwa tukikutana sana nyakati za jioni kupata moja mbili. Kwa sasa tumeshakuwa Madingi tumepotezana.