Pasco Mayalla ana vielement vya unabii afungue kanisa

Haha nimekusoma kumbe ni mkubwa! Nikadhani ndo mdogo
 
Hebu tuache mambo mengine bhana sio fresh kumpaka matope hivi..
Mkuu Hardbody, kwanza sio kunipaka matope, ni kweli enzi zangu nilikuwa a bod boy!, let the bygones be bygones
Staha itawale
Naunga mkono hoja , hii ni mada ya kuhusu umalaika, hivyo tusikumbushie enzi za ushetani, hata shetani mwanzo alikuwa malaika, alipoasi ndio akageuka shetani. Shetani nae akitubu anageuka malaika kama Saulo na Paulo
P
 
Sasa kama hao tunaowaamini wanatudanganya je? Ni mangapi ambayo tumewahi na tunazidi kudanganywa na hao tuliowaamini na wakatuaminisha tuwachague. Unadhani kwa akili ndogo hao watu wana kila sababu ya wao kuwepo hapo?
 
Kiti moto kinarudi mzee
 
Mkuu am 4 real , mimi nafahamika na wengi ni Mzee wa kutembea na Joni Mtembezi, hivyo kudhani nikifungua kanisa, badala ya kutumia divai nitamtumia Joni Mtembezi na waumimi wangu watakuwa ni watembezi wenzangu wa Joni Mtembezi.
P
John walker 😊😊😊😊 ni vizuri kabisa kama ukitumia hausumbui mtu Wala kusababisha madhara kwa majirani ,ndugu, jamaa, marafik na familia Kwa ujumla....

Jana usiku mke wangu alipigiwa simu na dada yake mkubwa kua mmewe amerud amelewa na anatukana njia nzima akifika nyumbani anaanza mtukana mkewe sana matusi ya maungo mengine mengi mbele ya watoto hii imekua tendency Sasa ila akiwa mzima ni mstaarabu sana Kwa uzoefu wako hapo tupe darasa kidogo from your experiences...

Nimeishi na watu wanakunywa pombe hawatukani,hawasahau maongezi na makubaliano wanatunza wake zao na familia Kwa ujumla....

Ni nini maoni yako Kwa watu mbali mbali kuhusu pombe...?

paschal Mayalla
 
yaani JF home of great thinkers, mnaleta uzi wa utani utani kama huu, kweli?
 
Lengo la kilevi ni relaxation, ila ukizidisha unalewa. Ukilewa sana unapoteza all sense of proportions ndio kule kukosa balance, kusema ovyo, kutukana sometimes hadi kuzimika.

Akisemacho mtu ulevini ndicho cha kweli akiwazacho. Hii maana yake kuna tatizo akiwa sober hawezi kutukana, ila akilewa ndio anatukana, ina maana anatukanaga kimoyomoyo akilewa ndio aibu inakata anatukana kwa sauti.

Mtu akizidisha ulevi unageuka ni ugonjwa, mtu anakuwa an alcoholic, na wengine wanapata uraibu, bila kulewa hawezi kufanya chochote!. Alcoholism ni ugonjwa kama mateja, unatibika sober house.

Kwa kadri unavyokunywa ulevi wa bei poa ndivyo ulevi huo unavyokuwa na madhara makubwa kimwili, kiafya na kiakili, mfano hard drinks, piwa, bongo, chang'aa zote ni familia ya konyagi, k-vant, gin, vodka , whiskey and brandy.

Mimi sijawahi kabisa kunywa bia, mimi napiga vikali tuu!. Nikitembea na Joni Mtembezi alama nyeusi, stimu yake ni short lived, haina harufu na haina hangover!, uki sip tuu, unaanza kuwaza mawazo ya mambo mazuri. Nilkilewa wale wadada unawaona kama vinyago!.

Lakini nikinywa kilevi kama Nyagi au K Vant, stimu zake zinashuka, kuanzia wahudumu unawaona ma miss!.

Namuomba Mungu aniwezeshe ili nitoke kwenye Black Label niende kwenye Gold Label na Blue Label.
P
 
Umemalza kila kitu Mkuu Ulitumia vyema nguvu za Psychic A.k.A Psychic Powers kama Ule Uzi Wako mmoja somedays hahaaa 😂 😂 😂
 
Thanks brother paschal umekua msaada sana Kwa taifa na hata humu ndani Jf
Nimejifunza mengi sana kwenye hii comment yako
Ni hakika mtu Alie lewa kusema yaliyo jificha moyoni...
 
Mkuu Pascal ,heko kwako je ulishawahi kuwa na wazo la kuandika memoir?

Nadhani pia utakua ni msomaji mzuri sana wa vitabu je unaweza kurecommend hapa your best five books ever ambavyo watu wanaweza kuvisoma?
 
Hapa pia unabii unaendelea
Wanabodi, kwenye bandiko hili Ndugu, Jamaa na Marafiki, Njooni Tumtetee Makonda Dhidi ya Mapapa Wauza Unga Wanaomzushia... nilishauri
Hata baada ya kuteuliwa kuwa Mwenezi wa CCM, Paul Makonda bado anapigwa vita na wasiomtakia mema, wasioitakia mema CCM na wasio itakia mema Tanzania.

Japo Tanzania ni nchi ya vyama vingi, na kwa mujibu wa katiba ya Tanzania, mamlaka kuu ya nchi ni wananchi, kupitia katiba, serikali ya CCM ilifanya mabadiliko ya katiba kinyume cha katiba na kupoka ukuu wa mamlaka kuu ya wananchi, na kuikakabidhi kwa chama cha siasa, ambapo sasa mamlaka Kuu ya nchi ni chama tawala, CCM ndio imeshika hatamu kuongoza serikali, hivyo katika ukuu wa chama, CCM ndio kila kitu, hivyo Makonda kama msemaji wa CCM, kikao cha CCM kinaweza kumwagiza Rais wa JMT atekeleze jambo lolote lililoelekezwa kwenye ilani ya CCM, Katibu Mwenezi ndie msimamizi wa ilani ya CCM, ana mamlaka yote ya kumuamrisha hadi Rais wa JMT, atekeleze ilani ya uchaguzi ya CCM, hivyo Makonda yuko very right kumuamrisha Waziri Mkuu na kumpa ultimatum ya miezi 6 kumaliza migogoro yote ya ardhi ya nchi hii.

Na baada ya miezi 6, kama Waziri Mkuu, Majaliwa Kasim Majaliwa atashindwa kuitatua migogoro yote ya ardhi, atakuwa ni ameshindwa kazi, Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi, itakutana na kumuagiza Rais wa JMT, kumuondoa Waziri Mkuu, kwa kushindwa kazi na kumteua Waziri Mkuu mwingine mwenye uwezo.

Hata ikitokea Rais Samia ameshindwa kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM, chama kinaweza kumfuta uanachama na hivyo kupoteza urais!, hivyo Mwenezi wa CCM ni mtu mkubwa sana, kuliko serikali yote ya Tanzania, na hii ndio maana halisi ya Party Supremacy, CCM ndio imeshika hatamu za kuiongoza serikali ya Tanzania .

Hongera sana Mwenezi mpya wa CCM, Paul Makonda, kuiheshimisha CCM, endelea kutoa maagizo na ultimatum kwa viongozi wote kuhusiana na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM, wewe ndiye msimamizi wa ilani ya CCM!.

Angalia ilani ya CCM imeelekeza nini kuhusu Bunge la JMT, toa maelekezo kwa Spika with ultimatums, Spika akishindwa kutekeleza Spika anaondolewa!, enzi za Spika Sitta, aliponea chupu chupu kuondolewa, kuna mtu mmoja very powerful ndani ya CCM aitwae "The King Maker" ndie alimuokoa Spika Sitta kwa kumpa maelekezo Mwenyekiti wa CCM, JK, na hii ndio salama yake!.

Makonda angalia ilani ya uchaguzi ya CCM inasema nini kuhusu mhimili wa Mahakama, toa maagizo with ultimatum kwa Jaji Mkuu atekeleze.

Angalia ilani ya uchaguzi inasema nini kuhusu majeshi, ulinzi na usalama, toa maelekezo with ultimatum kwa Amiri jeshi Mkuu na kwa Mkuu wa majeshi, IGP , etc.

Ila kwa nafasi ambazo sio za kichama kama Jaji Mkuu, Mkuu wa Majeshi, CAG, Mwenyekiti wa NEC, Msajili wa Vyama vya Siasa, Wakuu wa vyombo vya Ulinzi, Mwenyekiti wa Tume ya Utawala Bora na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma ambao ni wateule wa rais, Paul Makonda anaweza kuwapa maelekezo bila ultimatums kwasababu hawa chama hakiwezi kuwafanya chochote, na badala yake, chama kitampa maelekezo mamlaka yake ya uteuzi ambaye ni Rais wa JMT, awaondoe!.

Kiukweli ninamkubali sana Paul Makonda!, Tangu nilipoanza kumkubali Nimemkubali Sana DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam
He has never let me down!. Tena niliwahi kushauri Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa sana, kwasababu ana uthubutu kuliko hata JPM!. Apunguze... ushauri huu still stands, kwasababu miaka hii 4 ya Mama ni kumalizia awamu ya Magufuli, awamu ya baada ya Magufuli inaanza 2025, ila Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke hivyo you never know with politics, everything is possible!.

Paul Makonda kanyaga mwendo, chapa kazi, kazi iendelee!.
Paskali.
 
Mkuu unataka kutuambia ...hakuwa Mtanganyika!?
Kwa mujibu wa mwana JF britanicca,
Baba Mhutu, mama Mtanzania Mhaya!, biological father alivuka upande huu, akampenda binti yetu, akamtwaa, akaenda nae kwao, akamzalisha watoto wawili, a boy and a girl ambao wote walizaliwa kwao!.

Kule akam mistreat dada yetu, dada akawasomba wanae na kurejea nao Tanzania, wakiwa 7 years a girl na 5 years a boy!. Akarejea kwa wazazi wake Tanzania. Babu akawabadili majina na kuwapa majina ya kihaya hivyo kuwageuza kabila!.

Huku Tanzania, akatokea Mtanzania, wa kabila lile, akampenda mama despite kuwa na watoto wawili kabla, akamuoa. Kabila hilo ndilo kabila linaloongoza kwa wanaume kupenda!, Uncle wangu, amependa Mwanamke wa Tanga, mwenye watoto 3, na wote akawachukua. Hata mimi nina watoto 4 US, wawili ni wangu, na wawili walizaliwa mimi nikiwa huku, hata hivyo ni wangu kwasababu mke ni wangu na nawapenda kwa dhati!.

Ngosha akamchukua mama, na kwenda kuishi nae kwake, wale watoto wawili wa yule Baba wa mwanzo, wakabaki kwa babu!.

Wa kike alifanya kazi za nyumbani, wa kiume alichunga mbuzi wa babu, hakuna kwenda Shule.

Mama kule akawa hana raha kuhusu wanawe hawa, Msukuma kuuliza kipi kikusikitishacho, mama akajibu mwanangu hasomi anachunga tuu mbuzi wa babu yake!. Ndipo akachukuliwa na Baba wa watu aka wa adopt the traditional way, akaandikishwa shule kwa jina la huyo baba na hivyo kugeuka kabila lile ndio akawa Mtanzania!.

Niliposhauri Ili kuepuka possibility ya kutawaliwa na wageni, kuna haja kutumia DNA kuthibitisha asili halisi za viongozi wetu wakuu? nilimaanisha, na sasa kuna huyu mwingine!, kiukweli kabisa wale 'jamaa zetu' ni bure kabisa!, hakuna kitu pale!.
P
 
Mkuu naomba niongeze nyama nilikuwa na mfanyakazi wangu Mzee mmoja wa kibondo waliporudi walirudi huku wakiwa hawana kitu wakapokelewa kibondo anasema mwendaze alikuwa hajui Kiswahili na alikuwa mkorofi Sana .anamjua in personal Hadi jina lake la kihutu
 
Haya mambo tumeyaongea sana humu,


P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…