benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,187
Idara ya Uhamiaji Tanzania imetoa pasipoti za kieletroniki 193,645 katika miaka miwili ya uongozi wa
Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza jijini Dares Salaam, Ofisa Habari wa Idara hiyo, Mrakibu Paul Mselle alisema pasipoti hizo zimetolewa kwa Watanzania waliotaka kusafiri.
"Pasipoti za kielektroniki 193,645 zimeleta mageuzi makubwa, raia wa Tanzania waliohitaji kusafiri nje ya nchi walipata huduma kwa madhumuni mbalimbali,"alisema.
Mselle alisema katika pasipoti za kawaida idara hiyo ilitoa hati hizo za kusafiria 191,822 na kiutumishi 233.
Mselle alisema pasipoti za kidiplomasia zilitolewa 1,582 katika kipindi hicho na pasipoti maalumu ilitoa nane.
Alisema kazi hiyo imefanyika kwa mujibu wa Sheria ya Pasipoti na Hati za Kusafiria Sura ya 42 ya Mwaka 2002 na kanuni zake za mwaka 2018.
Pia Mselle alisema wamefanya maboresho ya sheria, kitaasisi, kimuundo na mifumo ya utendaji kazi. Aidha, aliwaomba Watanzania walioomba pasipoti kwenda ofisi za idara hiyo kuzichukua.