Pasipoti za kielektroniki 193,645 zatolewa ndani ya miaka miwili

Pasipoti za kielektroniki 193,645 zatolewa ndani ya miaka miwili

Je utayari wa Watanzania kupata pasipoti ukoje? sawa ni haki ya kila mtanzania lakini unapaswa kupewa hati ya kusafiria pale ambapo una "proof" ya safari sio document ya kupewa uweke kabatini
Then kama huelewi "miaka miwili ya Rais Samia" sina la kuongeza maana inajitosheleza
Kwani bure? Si serekali inapata kipato? Acha ukenge wewe!
 
Kwamba kuna Diplomats 1500+ wameteuliwa?

Au ndo Ikulu imeanza kuuza Passport za Kidplomasia, ili watu wasisumbuliwe kuchukua Visa?

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Huu mradi gharama iliyotumika inatakiwa watoe passport milioni 4 ili kurudisha gharama.
Hadi leo Tanzania ina Passport chini ya 400,000, nchi ya watu 60mil

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Mreta mada mnazidi kumchafu huyo bibi yenu kwa kumpamba pamba na taharifa zisizo chakachuliwa kwanza,Unakuja kumpongeza kisa passport laki .1.9 wakati tupo watanzania tupo mln 61+?.
Kama kila miaka 2 anaweza kufanya kazi kidogo hivyo si ataondoka madarakani ata kujenga shule yenye vyumba 7 hajamaliza?
Yule bichwa komwe mbona hakutoa hata 50,000?

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Kwa takwimu za huyo afisa uhamiaji maana yake kwa mwaka walitoa passport 96,900.kwa wastani

Watanzania tuko milioni 60

Wao kutoa passport kwa Watanzania milioni 10 kwa spidi hiyo itawachukua miaka 103 kwa wao kufikia lengo la kutoa passport milioni kumi

Kuhakikisha Watanzania hata milioni.tano wanapata passport itawachukua miaka 50 kufikia hilo lengo kwa spidi hiyo

Very sad
Sasa utagawa passport kwa watu wasiotaka safiri?

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Ni SAWA ndio lakini je waTanzania walioko kuendana na takwimu za sensa ya mwaka Jana ni kubwa kulingana na hii namba. Passport ni haki ya Mtanzania! Wangeleta namba ya Millioni 10 + ingeeleweka. Hapo Kuna urasimu mkubwa sana.

Na unaposema ndani ya miaka miwili ya Rais una maana gani??
Hakuna watu wenye urasimu kama uhamiaji,..mpaka wananikera.
 
Sasa utagawa passport kwa watu wasiotaka safiri?

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Aliyekwambia kazi ya passport ni ya kusafiria tu nani?

Passport ni kama kitambulisho cha NIDA tu yenyewe kwa sasa ni kitambulisho cha kimataifa kinatumika kuomba kazi ,scholarship na tenda mitandaoni za nje ya nchi

Hata ukitaka kusoma kozi za kimataifa online mfano hata kingereza cha kimataifa pale British Council Dar es salaam.mfano huwezi kusajiliwa bila passport

Matokeo yake wamejaa wahindi tu ndio hufanya hiyo mitihani na kupata scholarship za nje kibao ndio maana huwaoni wakisoma vyuo vya Tanzania

Sisi ofisa passport, kijana akienda kuomba linawaza tu kuwa anahitaji kwa ajili ya kusafiria tu

Tatizo uhamiaji bado wako wazee wengi wasioenda na kasi ya mabadiliko ya Dunia utasikia toka wakati wa Nyerere sisi tupo hapa passport ni kwa ajili ya kusafiria onyesha uthibitisho wa safari tukupe!!!
 
Kwa nini wanaitwa za kielectronic wakati ni kitabu hard kama zamani? Au wanadhani kitendo Cha KUHIFADHI data kwenye mtandao basi kinaifanya kuwa ya ki electronic? Nadhani wangeita pasport ya TANZANIA tu tabtosha
 
Sasa utagawa passport kwa watu wasiotaka safiri?

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Kenya wana target za kutoa passport lengo ni kutoa passport milioni 10 ndani ya miaka mitano kwa raia wake

Uhamiaji yetu sijui hata kama wa target yeyote wapo wapo tu

Kenyan passport​

“All eligible applicants for the Kenyan passport are advised that passport booklets are now available in sufficient numbers and processing of passports has been expedited to conform to international standards,” said Prof Kindiki.
“The ministry has set a target of tripling the number of Kenyan passport holders from the current 3.5 million to 10 million in the next five years,” he added.
 
Kwa nini wanaitwa za kielectronic wakati ni kitabu hard kama zamani? Au wanadhani kitendo Cha KUHIFADHI data kwenye mtandao basi kinaifanya kuwa ya ki electronic? Nadhani wangeita pasport ya TANZANIA tu tabtosha
Tena makaratasi ambayo yanachanika na kulowana
 
Idara ya Uhamiaji Tanzania imetoa pasipoti za kieletroniki 193,645 bkatika miaka miwili ya uongozi wa
Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza jijini Dares Salaam, Ofisa Habari wa Idara hiyo, Mrakibu Paul Mselle alisema pasipoti hizo zimetolewa kwa Watanzania waliotaka kusafiri.

"Pasipoti za kielektroniki 193,645 zimeleta mageuzi makubwa, raia wa Tanzania waliohitaji kusafiri nje ya nchi walipata huduma kwa madhumuni mbalimbali,"alisema.

Mselle alisema katika pasipoti za kawaida idara hiyo ilitoa hati hizo za kusafiria 191,822 na kiutumishi 233.

Mselle alisema pasipoti za kidiplomasia zilitolewa 1,582 katika kipindi hicho na pasipoti maalumu ilitoa nane.

Alisema kazi hiyo imefanyika kwa mujibu wa Sheria ya Pasipoti na Hati za Kusafiria Sura ya 42 ya Mwaka 2002 na kanuni zake za mwaka 2018.

Pia Mselle alisema wamefanya maboresho ya sheria, kitaasisi, kimuundo na mifumo ya utendaji kazi. Aidha, aliwaomba Watanzania walioomba pasipoti kwenda ofisi za idara hiyo kuzichukua.
Jamaniiii waTanzania wenzangu Mbona tumesinzia? Hiyo ni idadi ndogo Mnoo, kulinganisha na idadi yetu. Wapeni passport vijana wakapambane na dunia huko mbele.
 
Kenya wana target za kutoa passport lengo ni kutoa passport milioni 10 ndani ya miaka mitano kwa raia wake

Uhamiaji yetu sijui hata kama wa target yeyote wapo wapo tu

Kenyan passport​

“All eligible applicants for the Kenyan passport are advised that passport booklets are now available in sufficient numbers and processing of passports has been expedited to conform to international standards,” said Prof Kindiki.
“The ministry has set a target of tripling the number of Kenyan passport holders from the current 3.5 million to 10 million in the next five years,” he added.
Na kweli wanamanisha. Hakuna fursa utakayokimbizana nayo huku duniani usimkute Mkenya! Never!
 
Ndio, ameshakaa sana, amevumilia sana, mm siwezi kumlaumu coz ameshakataa posa nyingi akinisubiria, pia kakata tamaa kwa sababu walikua taari wanamsumbua sana

Pole sana mkuu
Katika kitengo kilichooza basi ni hiki, uhamiaji, mazee kuna wanaume malaya hii idara, sijui wana shida gani mbwa hawa

Aisee
 
Kwa nini wanaitwa za kielectronic wakati ni kitabu hard kama zamani? Au wanadhani kitendo Cha KUHIFADHI data kwenye mtandao basi kinaifanya kuwa ya ki electronic? Nadhani wangeita pasport ya TANZANIA tu tabtosha
Pasport za sasa zina chip ndo mana zinaitwa hivo, hiyo page ya kwanza yenye lamination ina chip kama line za simu.
Kwa hiyo wanahoja.
 
Je utayari wa Watanzania kupata pasipoti ukoje? sawa ni haki ya kila mtanzania lakini unapaswa kupewa hati ya kusafiria pale ambapo una "proof" ya safari sio document ya kupewa uweke kabatini
Then kama huelewi "miaka miwili ya Rais Samia" sina la kuongeza maana inajitosheleza
Proof ya safari ya kazi gani kamą mtu anataka pasi ya kusafiria anavigezo vyote mpatie kamą safari akipata ghafla aanze mlolongo wa kufatilia uhamiaji? Aweke ndani hilo ni juu yake
 
Aliyekwambia kazi ya passport ni ya kusafiria tu nani?

Passport ni kama kitambulisho cha NIDA tu yenyewe kwa sasa ni kitambulisho cha kimataifa kinatumika kuomba kazi ,scholarship na tenda mitandaoni za nje ya nchi

Hata ukitaka kusoma kozi za kimataifa online mfano hata kingereza cha kimataifa pale British Council Dar es salaam.mfano huwezi kusajiliwa bila passport

Matokeo yake wamejaa wahindi tu ndio hufanya hiyo mitihani na kupata scholarship za nje kibao ndio maana huwaoni wakisoma vyuo vya Tanzania

Sisi ofisa passport, kijana akienda kuomba linawaza tu kuwa anahitaji kwa ajili ya kusafiria tu

Tatizo uhamiaji bado wako wazee wengi wasioenda na kasi ya mabadiliko ya Dunia utasikia toka wakati wa Nyerere sisi tupo hapa passport ni kwa ajili ya kusafiria onyesha uthibitisho wa safari tukupe!!!
Acha ushamba wewe, passport maana yake ni ya kupita mpakani.

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Ndo maana idadi ya Watanzania wanaotafuta fursa nchi za nje ni ndogo sana ukilinganisha na Jirani zetu tazama pasi tu ya kusafiria mtu atazungushwa mpka aache au atoe rushwa wakati Serikali ingeweza kutengeneza pesa nzuri kupitia uhamiaji kwa mkakati wa kuhakikisha Watanzania angalau milioni 4 wanapata Hati za kusafiria. Lakini huoni hayo yakifanyika zaidi ya kuja na kujitapa na hii aibu wito kwa kamishna wa uhamiaji hebu fanya kazi kwa weledi maafisa wako kutwa kucha kufatilia maeneo yenye miradi ya Ujenzi walipo raia wa China na wengineo ili wapate chochote, ni ajabu mtu anaomba pasi ya kusafiria anajaza taarifa ambazo zinapatikana kwenye kitambulisho cha taifa unabaki unajiuliza mifumo haisomani au ni Njia tu ya kujitengenezea mwanya wa rushwa?
 
Back
Top Bottom