Pasipoti za kielektroniki 193,645 zatolewa ndani ya miaka miwili

Serikali ingeweza kutengeneza pesa nzuri kupitia uhamiaji kwa mkakati wa kuhakikisha Watanzania angalau milioni 4 wanapata Hati za kusafiria.
Passport milioni 4 kila passport Shs.150,000 serikali ingepata shilingi
600,000,000,000 yaani shilingi mia sita bilioni

Kitengo cha passport ni mgodi wa pesa ambao serikali haitaki kuutumia kupata pesa kupitia kutoa passport
 
ni ajabu mtu anaomba pasi ya kusafiria anajaza taarifa ambazo zinapatikana kwenye kitambulisho cha taifa unabaki unajiuliza mifumo haisomani au ni Njia tu ya kujitengenezea mwanya wa rushwa?
NIDA na kitengo cha Passport wote wako chini ya wizara moja ,wizara ya mambo ya ndani

Lakini hawasomani wako ofisi moja

Very interesting
 
Passport milioni 4 kila passport Shs.150,000 serikali ingepata shilingi
600,000,000,000 yaani shilingi mia sita bilioni

Kitengo cha passport ni mgodi wa dhahabu ambao serikali haitaki kuutumia kupata pesa kupitia kutoa passport
Yani pesa ya maana kabsa halaf wapo wamekaa tu wanajisifia bila aibu kwa kutoa pasi 190,000 wenzetu (nchi Jirani) wataendelea kutukimbiza kwenye kiła kitu tukienenda kwa mitazamo hii ya kijima
 
NIDA na kitengo cha Passport wote wako chini ya wizara moja ,wizara ya mambo ya ndani

Lakini hawasomani wako ofisi moja

Very interesting
Aibu sana hii mpaka unajiuliza hawa watu maofisini huma wanaenda kupigwa viyoyozi tu na kuhudhuria semina, vikao, warsha zisizoisha huku wakipanda magari makubwa yenye kubwia mafuta
 
Aibu sana hii mpaka unajiuliza hawa watu maofisini huma wanaenda kupigwa viyoyozi tu na kuhudhuria semina, vikao, warsha zisizoisha huku wakipanda magari makubwa yenye kubwia mafuta
Tatizo maofisi mengi ya serikali hakuna malengo yaani targets kwenye vitengo vyake

Kwa hiyo wafanyakazi huamka asubuhi kwenda kushinda ofisini sio kufanya kazi ofisini

Matokeo ndio hayo
 
Hii nchi itakuwa HURU siku watanzania wakipata akili ya KUWAFUKUZA CCM, yaani wasahaulike kabisa kama ilivyo kwa KANU kule Kenya
 
Nilivyoelewa ni ndani ya miaka miwili. Fanya makisio ndani ya miaka mingine 60+ ni paspoti ngapi zimetolewa?
Pili: natarajia, ingawa sina hakika, paspoti hutolewa kwa wanaohitaji kusafiri na hazigawiwi kama sadaka.
Tatu: nakubali kwamba kuna urasimu usio wa lazima ktk kupata paspoti.
 
Passport sio document ya safari wewe

Vigezo vya nchi zote zinazotunguka Passport hutolewa kwa kila mwenye kitambulisho cha NIDA akiitaka as long una kitambulisho cha NIDA ukitaka unapewa huulizwi mambo ya safari unaenda wapi kufanya nini hiyo sio kazi ya afisa Passport ni kazi ya ubalozi wa nchi a anakoenda kuomba visa wao ndio wamhoji kabla kumpa visa unakuja nchini kwetu kufanya nini?

Kitengo cha passport wanajibebesha majukumu yasio yao .Ya balozi waachie balozi husika

Kupata Passport sio kuwa mtu ataingia nchi ya watu atahojiwa huko ndipo wampe visa aingie kwao


Kitengo cha passport wao watoe passport kwa raia basi

Nchi nyingi zinafanya hivyo

Idara yetu ya passport roho mbaya wamejipa kazi za uofisa viza pia jukumu lisilo lao
 
Haya ubarikiwe chawa wa Samia.
 
Hakika umesema vyema hawa watu wanajipa majukumu yasiyokuwa ya kwao eti unaniuliza safari naenda kufanya nini yeye inamuhusu nini badala ya kuhakikisha watt wengi zaidi wanapata pasi wanajitwika yasiyokuwa ya kwao
 
Ukweli usemwe tu! Passport ni kitu muhimu na haki Kwa kila Mwananchi. Swala.la.kusafiri ni lake. Unaweza kuwa waTanzania Kwa kuwa wengi hawana ndogo za kusafiri nje na ndio maana Serikali na Uhamiaji wameiweka kama kitu Maalumu.

Tembelea tovutinya uhamiaji Marekani uone mwaka Jana 2022 walitoa e passport Millioni 22.

Nina mtu wangu yeye amepata watoto 2 akiwa Marekani na wote wameshapata PP wa mwisho ana miezi 6 tu lakini anayo.
Yuko mwingine amepata mtoto hapa Arusha na Mmarekani mtoto ana miezi 5 Naye aliomba ameshapatiwa Passport ya huyo kuchangia.

Sasa Kwa sisi waTanzania tunafaanyiwa haya na pia bila uhamiaji yenyewe kujua ndio chanzo ya mapato.
Nchi ni ngumu sana ndani ya CCM hii.
 
Passport nihaki kwakila mtu ila ukienda kufata complications kibao nchi hii hatar sana
 
Wakiona unataka kwenda nje roho inawauma, ndiyo maana wanaleta makauzibe kibao. Wapeni watu passport. Anachotaka kufanyia nyie kinawahusu nini. Lebanon ina watu 4M. Walioko nje ya nchi ni 14M. Leo uchumi wa Lebanon umeanguka, ni hawa diaspor ndiyo wanauokoa. Taasisi zimekaliwa na mazeemazee yanayoamini na ushirikina.
 
Idara ya Uhamiaji Tanzania imetoa pasipoti za kieletroniki 193,645 katika miaka miwili ya uongozi wa
Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kati ya watanzania 62,000,000
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…