Pole sana. Kuna mambo kadhaa yanachangia gari yenye engine inayotumia petroli kutumia mafuta mengi isivyotakiwa. Ila hii yako inabidi ichekiwe mara moja
* Engine inapokuwa haina matunzo mazuri na service kwa wakati matokeo huwa ni kushuka kwa utendaji kazi mzuri na ulaji wese. Service ni pamoja na kubadilisha spar plugs, air cleaner, fuel filter pamoja na mantainance ya throttle valve pamoja na oxygen sensors.
* Utumiaji Engine oil isiyo na viwango - tumia oil yenye kiwango cha viscosity kilichopangwa kwa gari yako
* Utumiaji AC wakati unaendesha
* Matairi yaliyochoka
* Utumiaji wa gia kimakosa
* Clutch kuchoka
Kama huna fundi makini nakupa namba ya mtu makini na siyo mpiga ramli, ni fundi na ameajiriwa lakini huwa anapata muda weekends na anakuja kwako anafanya kazi ukiwa unaona.
Rich Mavoko 0746121263
Kama ikiwa high consumption inasababishwa na umeme wa gari atakusaidia pia.
Binafsi natumia gari yenye cc2500 na consumption ni kama Toyota wanavyosema inatakiwa iwe ambayo ni KM 8.51 hadi 11.2 kwa lita. Kwahiyo nikipata sita kwa lita ntapaki kwa marekebisho.
OOh pia uendeshaji wako unaweza kuchangia utumiaji mafuta mengi ama kidogo