Wakenya wamegeuzwa biashara na WHO. Uhuru anapewa chake na shirika la kibeberu, anapima watu na vifaa vilivyojazwa virus feki.
Matokeo yake kila mtu ni corona positive.
Corona is a scam in the first place. Hakuna kitu kama corona. Ni upumbafu na ujinga mtupu.
Sent using
Jamii Forums mobile app
Japo sikubaliani nawe, yawezekana ugonjwa uliopo ni mafua makali kama yaliyotokea mwishoni mwa mwaka 2019. Kwa watu wenye ngozi nyeupe, hata mafua ya kawaida huwasumbua kwelikweli.
Yawezekana pia, vifo ninavyotokea sasa hivi Afrika, ni vya magonjwa mengineyo, ila kwa kuwa kuna hofu ya mlipuko wa COVID-19, na kwa kuwa vifo awali havikuwa vikitangazwa kama sasa, kila kifo kinahusishwa na korona. Wengine, hasa wanaotengwa kwa kisingizio cha kuambukizwa, wanakufa kwa kukosa tiba sahihi ya magonjwa mengine yanayowasumbua. Mungu azilaze roho zao pema peoni.
Iwapo kweli kuna huo ugonjwa, usingechukua maisha ya watu hasa wenye kipato kizuri na wa mijini. Kwa mfano, machinga, mama ntilie, wahudumu wa mabaa, na wachumia tumbo mijini, kutwa wanakutana na watu wengi lakini wako salama tu.
Hofu itagharimu maisha ya wengi, hasa kama watumishi wa afya, kwa sababu hiyo, watawanyanyapaa wagonjwa.
Kwa vyovyote vile tuzingatie kanuni za afya kujikinga dhidi ya maambukizi ya COVID-19. Kufanya hivyo, kutatusaidia pia kuimarisha afya zetu dhidi ya magonjwa mengine na hatimaye kutupunguzia gharama za matibabu. Kinga ni bora kuliko tiba.
JIKINGE UMKINGE JIRANI
JILINDE UWALINDE WAPENDWA WAKO