Pasu kwa Pasu haiwezekani enyi vijana

Pasu kwa Pasu haiwezekani enyi vijana

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
PASU KWA PASU HAIWEZEKANIKI ENYI VIJANA.

Anaandika, Robert Heriel

Mtu huchagua maisha yake mwenyewe katika Baadhi ya Maeneo, kuchagua uwe Mmiliki au mmilikiwa ni Moja ya uchaguzi binafsi wa mtu, mtu unajiamuliwa mwenyewe.

Ukishachagua upande wa MMILIKIWA elewa Kabisa hakuna kitu kinachoitwa usawa(Pasu Kwa Pasu),
Lakini ukiwa Mmiliki basi yote yapo juu yako,

Rafiki zangu Wasanii wa Muziki Pale Sinza Dar nikikutana nao Baadhi yao hulalamika kuhusu kunyonywa na mameneja, au Baadhi ya Media zinazowasimama, au LEBO za muziki zinazowameneji..

Wanataka Ati wapewe Nusu Kwa Nusu, Pasu Kwa Pasu.
Mfano, Mwanamuziki apige Shoo iliyoingiza labda milioni 30, basi msanii apewe milioni 15. Lakini wao wengi wao wanapewa ikizidi Sana milioni moja au mbili.

Jibu langu siku zote, hakunaga Pasu Kwa Pasu baina ya Mmiliki na mmilikiwa. Hiyo kitu haipo na haitakuja kutokea. Hiyo ipo Kibiashara na kiuchumi.

Ukitaka Maslahi zaidi basi itakupasa Ujitegemee, ujimiliki mwenyewe. Lakini kamwe huwezi hitaji Nusu au zaidi kumzidi anayekumiliki hiyo haipo.

Kipaji chako hakiwezi kukufanya umzidi anayekumiliki hata kama ungeimba kama Malaika.
Kama unahisi unaonewa basi jitegemee, fanya mwenyewe, jisimamie ili ujilipe pesa ya kipaji, pesa ya usimamizi, na kila kitu.

Mtu akutoe huko Makanya, akupromoti jina lako likue, ili aweze kufanya biashara alafu jina lako likikua unataka mgawane pasu Kwa pasu😃😃😃 hizo akili niza wapi?

Wewe ni Daktari, ni kweli unaelimu ya Udaktari na unakipaji cha kutibu watu, lakini hauna Hospotali, hauna vitendea kazi, hauna jina lolote ni kwamba ulimaliza hapo Muhimbili, au nje ya nchi.

Hospitali Fulani imekuchukua, imekikuza kipaji na Fani yako, imekupromoti mpaka kwenye vyombo vya habari sasa Tanzania nzima inakujua, alafu baadaye unahitaji pasu Kwa pasu🙄🙄 umechanganyikiwa,
Unataka ulingane mapato na mmiliki wa Hospitali😃😃 hizo ni Akili za Fisi, tamaa mbaya.

Wewe ni mwanasiasa, hukuwa lolote zaidi ya Kupiga mdomo, ulikuwa na kipaji cha ushawishi na uongozi, lakini hukuwa na jukwaa na chama cha kufanyia Siasa zako, Ukachukuliwa na Chama Fulani labda ni CCM au CHADEMA, Wamekulea, wamekupromoti alafu unataka kuleta za kuleta, 😃😃 wewe ni kichaa.
Hakuna Nusu Kwa Nusu ikiwa utajiweka nafasi ya Kumilikiwa.

Vijana wa sasa wanalalamika ooh! Mishahara midogo sijui Kampuni Fulani wanapunja🤣🤣 Ulitaka wakulipe ngapi? Anzisha biashara yako ujilipe pesa utakayo Kama ni rahisi.

Nenda kachunge Mbuzi, nenda kalime, nenda kavue Samaki, jimiliki uweze kujilipa utakavyo.

Dunia haina Usawa Kama mwenyewe umejiweka kwenye nafasi isiyo yako.
Dunia inausawa Kwa watu waliosawa,

Usipende kulalamika na kuona Kama unaonewa ikiwa wewe mwenyewe ndio ulichagua kufanya hivyo.

Rizika na upewacho tena mshukuru huyo Boss wako Kwa kuanzisha Kampuni ambayo Ukoo wenu wote hakuna hata mmoja aliyeweza kuanzisha, labda angeanzisha Baba yako usingekuwa unalipwa hivyo.
Hiyo ichukue Kama Changamoto ujipange nawe uanzishe kiwanda au Kampuni ili watoto wako au wajukuu wako wasipate shida uliyoipata wewe.

Kusomesha watoto wako haitoshi, ni sehemu tuu ndogo ya kumfanya mtoto wako ajitambue, lakini kama utasomesha ili aje amilikiwe na mtu mwingine basi malalamiko yatakuwa yaleyale.

Mtu atakulipa 10% ya kile unachomzalishia, akijitahidi Sana labda 30%.

Nipumzike sasa

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Dar es salaam
 
Kweli ndondo nitafute mimi halafu wewe utake nusu kwa nusu

Thubutu! Per diem yako badala ya 80k utakula 30k ila nitakutoa lunch kdg nyama nusu utakula na K-Vant ndogo moja, imeisha.


😃😃😃

Wape Pasu Kwa pasu wana
 
Kwa hiyo konde boy alikuwa sahihi kupigwa na kitu kizito na bwana simba ...!
 
Back
Top Bottom