GuDume
JF-Expert Member
- Jan 18, 2015
- 6,651
- 14,337
Mkuu tusaidie vitabu vya Akajase Mbamba
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Zipo mkuu. Nakumbuka kuzisoma nikiwa mtoto. Pinokyo 1 na Pinokyo 2 kama sikosei.Sidhani kama tunazo kwa Kiswahili
MPIGA FILIMBI WA HAMELIN4. Adili na Nduguzee
5. Mpiga filimbi wa hamelini (yaani kisiasa kukiwa na mada nzito...jamaa wanapiga filimbi kuzusha jambo jingini ili kutuhamisha kimawazo)
Mkuu naweza kupata hiyo audio kwa whatsp? Please nicheck inbox kama kuna uwezekano.Nina audio book
Fadhy mzee wa HUBA, Kama una PDF file ya huba tuimwage humuMPIGA FILIMBI WA HAMELIN
Hamelin ni mji nchini Ujerumani. Kulikuwa na janga kubwa sana la panya. Panya waliharibu kila kitu. Walileta maudhi makubwa sana kwa watu wa Hamelin.
Wakazi wakamjia juu Meya na Baraza la Mji kuwa wafanye kila liwezekanalo kuwaondoa panya hao. Maamuzi yakafanyika. Likatolewa tangazo kuwa, zawadi ya pesa elfu moja itatolewa kwa yeyote atakayefanikiwa kuwaondoa panya hao.
Watu wengi wakajitokeza, hata wasifanikiwe. Wananchi wakaja juu, "Kuna haja gani Meya na Baraza lake kufana kwenye mavazi yao nadhifu ilhali wameshindwa kuwaondoa panya?"
Meya na Baraza lake wakakosa raha. Wananchi wamecharuka kweli kweli.
Mara, akatokea bwana mmoja. Mrefu, mwembamba. Akivalia nadhifu. Walimpohoji jinale, akasema yuaitwa, Mpiga Filimbi. Akawaeleza, ameisikia shida yao. Kwamba, amesafiri kutoka mbali kweli. Zaidi, akipiga filimbi yake, hakuna mnyama awaye yoyote juu ya ardhi aweza kuihimili.
Meya akamkaribisha kwa bashasha. Akamwambia, akifanikiwa kuwatokomeza panya, hatompa tena pesa elfu moja, bali laki moja.
Mpiga Filimbi akaanza kazi yake. Aliipiga filimbi kwa ustadi mkubwa sana. Panya walitoka kote walikokuwapo. Si panya mzee. Si mtoto, hata alozaliwa dakika hiyo hiyo. Wakamfuata Mpiga Filimbi. Akawapeleka mtoni. Ukawa ndiyo mwisho wa panya mjini Hamelin.
Mpiga Filimbi akaenda Ukumbi wa Mji kwa Meya kuchukua chake. Meya akamwambia, tena kwa ukali na jeuri ya kiuongozi, huku akimdhihaki, "Hiyo pesa yote kwa kazi gani ya maana uliyoifanya?"
Mpiga Filimbi akamjibu, "Lakini uliahidi!"
Meya akamwambia kwa dhihaka, "Ile ilikuwa dhihaka tu. Chukua pesa hamsini uende zako!"
Kwa hasira, Mpiga Filimbi akamwambia, "Kama usiponilipa, si punde utatamani ungekuwa umenilipa. Nitaipiga hii filimbi hata ushangae!"
Huku akicheka, Meya akamwambia, "We nenda kapulize filimbi lako, ikibidi hadi ipasuke."
Mpiga Filimbi akasema, "Basi sawa!" Tena, huku akitabasamu. Akaanza kupita mitaani akipuliza filimbi. Awamu hii, akiwa amebadili sauti ya muziki. Sauti tamu. Iliyapasua mawimbi kwa muziki mtamu ambao haukuwahi kusikika kabla. Ulikuwa muziki ambao hakuna mtoto alikubali kuukosa.
Watoto walikurupuka kutoka huku na kule. Waliokuwa wakinyonya waliacha kunyonya. Waliokuwa wakiogeshwa waliyakimbia mabeseni. Waliokuwa mashuleni hata usiseme. Wakamfuata Mpiga Filimbi bila hata kufahamu, wala kujali, walikokuwa wakienda.
Wanamji wakashituka. Kila namna waliyojaribu kumzuia Mpiga Filimbi walishindwa. Akawapeleka mahali palipokuwa na pango kubwa kwenye mlima wa Koppelberg. Watoto wote wakaingia ndani. Pango likajifunga kwa sauti kali mithili ya radi kwa kishindo chake. Mtoto mmoja tu alibaki nje. Alikuwa mlemavu akitembelea gongo, hivyo hakuendana na kasi ya mbio ya watoto wenzake.
Mji wa Hamelin ukabaki hauna watoto. Ukawa mkiwa na mpweke kwa miaka mingi sana.
Meya na Baraza lake walifukuzwa nje kabisa ya mji huo.
Wananchi wakaweka bango la mawe lililochongwa vema juu ya mlango wa pango hilo walimopotelea watoto wao wote.
Wakaandika; AHADI IKITOLEWA, SHURTI ITEKELEZWE DAIMA.
©Fadhy Mtanga
Journey to the WestZipo mkuu. Nakumbuka kuzisoma nikiwa mtoto. Pinokyo 1 na Pinokyo 2 kama sikosei.
Asante kwa uzi mzuri.
Ongezea na za Kichina tafadhali.
1.Mfululizo wa hadithi za "Mfalme Kima"
2. Hekaya za Avanti.
Akili kufundishwa, hadithi ya shing'weng'eMasala Kulangwa
Hichi kitabu nakumbuka mzee alitinunulia nyumbani. Kinaitwa sijui pied piperMPIGA FILIMBI WA HAMELIN
Hamelin ni mji nchini Ujerumani. Kulikuwa na janga kubwa sana la panya. Panya waliharibu kila kitu. Walileta maudhi makubwa sana kwa watu wa Hamelin.
Wakazi wakamjia juu Meya na Baraza la Mji kuwa wafanye kila liwezekanalo kuwaondoa panya hao. Maamuzi yakafanyika. Likatolewa tangazo kuwa, zawadi ya pesa elfu moja itatolewa kwa yeyote atakayefanikiwa kuwaondoa panya hao.
Watu wengi wakajitokeza, hata wasifanikiwe. Wananchi wakaja juu, "Kuna haja gani Meya na Baraza lake kufana kwenye mavazi yao nadhifu ilhali wameshindwa kuwaondoa panya?"
Meya na Baraza lake wakakosa raha. Wananchi wamecharuka kweli kweli.
Mara, akatokea bwana mmoja. Mrefu, mwembamba. Akivalia nadhifu. Walimpohoji jinale, akasema yuaitwa, Mpiga Filimbi. Akawaeleza, ameisikia shida yao. Kwamba, amesafiri kutoka mbali kweli. Zaidi, akipiga filimbi yake, hakuna mnyama awaye yoyote juu ya ardhi aweza kuihimili.
Meya akamkaribisha kwa bashasha. Akamwambia, akifanikiwa kuwatokomeza panya, hatompa tena pesa elfu moja, bali laki moja.
Mpiga Filimbi akaanza kazi yake. Aliipiga filimbi kwa ustadi mkubwa sana. Panya walitoka kote walikokuwapo. Si panya mzee. Si mtoto, hata alozaliwa dakika hiyo hiyo. Wakamfuata Mpiga Filimbi. Akawapeleka mtoni. Ukawa ndiyo mwisho wa panya mjini Hamelin.
Mpiga Filimbi akaenda Ukumbi wa Mji kwa Meya kuchukua chake. Meya akamwambia, tena kwa ukali na jeuri ya kiuongozi, huku akimdhihaki, "Hiyo pesa yote kwa kazi gani ya maana uliyoifanya?"
Mpiga Filimbi akamjibu, "Lakini uliahidi!"
Meya akamwambia kwa dhihaka, "Ile ilikuwa dhihaka tu. Chukua pesa hamsini uende zako!"
Kwa hasira, Mpiga Filimbi akamwambia, "Kama usiponilipa, si punde utatamani ungekuwa umenilipa. Nitaipiga hii filimbi hata ushangae!"
Huku akicheka, Meya akamwambia, "We nenda kapulize filimbi lako, ikibidi hadi ipasuke."
Mpiga Filimbi akasema, "Basi sawa!" Tena, huku akitabasamu. Akaanza kupita mitaani akipuliza filimbi. Awamu hii, akiwa amebadili sauti ya muziki. Sauti tamu. Iliyapasua mawimbi kwa muziki mtamu ambao haukuwahi kusikika kabla. Ulikuwa muziki ambao hakuna mtoto alikubali kuukosa.
Watoto walikurupuka kutoka huku na kule. Waliokuwa wakinyonya waliacha kunyonya. Waliokuwa wakiogeshwa waliyakimbia mabeseni. Waliokuwa mashuleni hata usiseme. Wakamfuata Mpiga Filimbi bila hata kufahamu, wala kujali, walikokuwa wakienda.
Wanamji wakashituka. Kila namna waliyojaribu kumzuia Mpiga Filimbi walishindwa. Akawapeleka mahali palipokuwa na pango kubwa kwenye mlima wa Koppelberg. Watoto wote wakaingia ndani. Pango likajifunga kwa sauti kali mithili ya radi kwa kishindo chake. Mtoto mmoja tu alibaki nje. Alikuwa mlemavu akitembelea gongo, hivyo hakuendana na kasi ya mbio ya watoto wenzake.
Mji wa Hamelin ukabaki hauna watoto. Ukawa mkiwa na mpweke kwa miaka mingi sana.
Meya na Baraza lake walifukuzwa nje kabisa ya mji huo.
Wananchi wakaweka bango la mawe lililochongwa vema juu ya mlango wa pango hilo walimopotelea watoto wao wote.
Wakaandika; AHADI IKITOLEWA, SHURTI ITEKELEZWE DAIMA.
[emoji2398]Fadhy Mtanga
Hichi kitabu nakumbuka mzee alitinunulia nyumbani. Kinaitwa sijui pied piper
View attachment 1873130