Pata ushauri, michango na mawazo ya ufugaji wa bata wa kienyeji kibiashara

Pata ushauri, michango na mawazo ya ufugaji wa bata wa kienyeji kibiashara

Mjasiriamali huwa ni "risk taker" hivyo pambana tu na hivyo changamato za kuku. Kama una soko la uhakika nakuomba usiache kufuga kuku.
yote kwa yote shikamoo Tutor B

Marhabaaaaaaaaaaaaaaa!
 
MORIA... upo wapi .... I have the same idea ya kufuga in large scale kwa matunzo ya kisasa zaidi .... nimejaribu kuwatunza watoto 11 wa bata walioanguliwa mwezi wa 7 kwa kuwapa broiler starter in first three weeks na baade kuwapa growers mash ikichanganywa na portion ya pumba za mahindi na matokeo ni mazuri sana ... watoto hawa sasa ni wakubwa sana with a high yield in growth

ninachotaka kufanya sasa hivi ni kununua mayai ya bata kwa wafugaji mbalimbali na kuyapeleka kuanguliwa kwa incubator machine .... naanza na mayai 50 ... then from there I can propel the project well

kumbuka bata wanakuwa vizuri kwa malisho ya majani (grazing) na maji kwa ajili ya spreening
Ahsante kwa mawazo yako.
 
Kumbuka kubadirisha madume mara kwa mara kuepuka kuzalishana ndugu kwa ndugu (inbreeding). Vinginevyo ukubwa wa bata hupungua.
 
TAFADHALI KAMA HUTOJALI ITAKUWA MSAADA KWETU TUNAOFIKILIA KUINGIA HUKO UNAKOACHA WEWE KAMA UTATUELEZEA KWA KINA CHANGAMOTO ULIZOKUTANA NAZO. PIA NAMNA ULIVYOPAMBANA KUZITATUA MPAKA UKACHUKUA UAMUZI WA KUTAKA KUJARIBU MKAKATI WA PILI. AKSANTE

WASALAAM
 
soko lipo kubwa tu mkuu ni juhudi zako kufanya research kujua nani anahitaji na ni wakati gani na je wateja wako ni wapi na je wanamudu bei.
kaka hao bata bukin bado wapo?ni wale weupe au?
 
Analisha wenzake kivipi?
bata mmoja anauzwa laki na hamsini(150,000) hata wakiwa 30 kwa mwezi hawawezi kula zaidi ya gunia so fanya hivi uza bata mmoja nunua kila mwezi gunia moja 15,000* 10 ni 150,000 bei ya bata mmoja na wakitaga vizuri ukivuna vifaranga 20 kwa astani kwa bata 5 utakuwa na faida kiasi gani
 
wadau habari, na poleni kwa majukumu ya kila siku

Kama mada inavojieleza , mimi ni kijana na ninafikiria kuanzisha ufugaji wa bata, ninachoomba kwenu ni, yeyote yule mwenye uelewa juu ya ufugaji huu naomba anipe elimu kuhusu yafuatayo

1.Aina ipi nzuri ya kufuga, nahitaji kufuga bata wa kienyeji

2.Je bata wanahitaji kupewa chakula kama kuku au wao hujitafutia tuu,, na kama jibu ni wanahitaji chakula , je chakula gani ni suitable kwao katika ukuaji wao

3.je bata huathiriwa na magonjwa kama kuku,, kama jibu ni ndiyo huathiriwa, je ni magonjwa gani hasa yanayowaathiri, na dawa zipi hutumika kuwatibu

4.mwisho naomba kufahamu kuhusu changamoto za ufugaji huu

Nb;nahitaji kufuga kama biashara na sio ufugaji kwa ajili ya kitoweo

Natanguliza shukurani zangu za dhati kwa wote…!!!
 
mkuu kuna jamaa mmoja amebobea kwenye hiyo fani. mtafute kama uko dsm ukamuone atakushauri vizuri sana kuhusu ufugaji wa bata kibiashara. profile yake hiyo. pia youtube anapatika na huwa hachaji chochote kwa wanaomtembelea. huyu anashauri ufuge bata weupe soko lake kubwa ni wachina na wana bei nzuri.
 
mkuu kwa hawa bata wa kienyeji huwa hawana shida wao wanazaliana sana cha muhimu matunzo tu tafuta dume zuri na tetea hapo hakikisha unanunua mbegu kutoka sehemu tofauti ili usifuge wa ukoo mmoja,andaa sehemu nzuri ya kuwaweka na chakula tafuta pumba ya mahindi unawawekea kwenye chombo na pembeni unawawekea maji mengi ya kunywa wao ni maji tu halafu ili wapate vitamini kila siku iwe unawatupia mboga za majani na mabaki ya vyakula mbona utafurahi sana kuhusu dawa mimi huwa siwapi dawa yoyote wao hawana shida
 
Kuna tatizo lolote kufga bata wa ukoo mmoja
 
Kuna tatizo lolote kufga bata wa ukoo mmoja
ndio mkuu inatakiwa mbegu utafute kwenye vyanzo tofauti na wakishazaliana madume ya mwanzo pamoja na yale yaliyozaliwa unayasambalatisha unaleta madume mapya hiyo iko kwa ndege wote<br />Hapo kwenye kusambalatisha nina maana unaweza wauza madume yote ukanunua dume wengine au ukawafanya kitoweo
 
Hilo tatizo ni lipi la ukoo mmoja??

Labda magonjwa?

Kudumaa?

Au ni nini tatizo hasa
 
Back
Top Bottom