sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
Imagine taifa halina hata rasilimali, sehemu kubwa ni jangwa, mashambulizi mara kwa mara lakini bado uchumi wao ni mkubwa kuliko nchi zote za Afrika mashariki.
Pato la taifa ni Dola bilioni 500+ sawa na shilingi zetu trilioni 1,250, Naomba nieleweke kwamba kiasi hiki hakihusisiani na chochote kuhusu misaada.
Pesa kwa kiasi kikubwa wanapata kwenye ubunifu wa Teknolojia za Kilimo, Computer, Silaha, mabenki, n.k. Israel ni taifa linalotegemewa na makampuni mengi ya simu na software kwenye kubuni teknojia mpya, karibu kila kampuni kubwa ina ofisi ya ubunifu Israel, hata hizi software za kudukua mawasiliano huwa zinabuniwa huko zinauzwa kwa mamia ya mabilioni.
Nashangaa kuona hizi kelele zinazopigwa kisa Marekani anaipa Israel dola bilioni 3 za msaada, Pengine kwa umasikini wa mataifa yetu ni pesa nyingi sana lakini kwa hali iliyopo Israel hii bado ni pesa ndogo lakini inakuzwa sana kuonekana kwamba bila huu msaada Israel inaanguka.