Sawa
Unajua kuna kitu unashindwa kuelewa inaweza ikawa per capita ni kubwa lakini ina hizi weakness 2:
Huenda walioshika uchumi ni wachache na welfare iko low maana per capita ni wastani tu ambapo ukubwa wake huwa unabebwa na low population
Angalia mataifa mengi yenye the highest per capita lazima utakuta yana population ndogo
Ndio maana wachumi wakaja na GDP PPP ili kulinganisha ustawi wa watu kiuchumi na kimaendeleo kati ya taifa moja na lingine kwa sababu ya weakness ya per capita
Ambapo Tanzania kwenye GDP PPP bado inafanya vizuri kuliko Uganda na kama haitoshi na bado kwenye nominal GDP iko vizuri zaidi ya Uganda
Unachanganya vitu Mzee, kuna
GDP ambayo Inapima thamani ya vitu na huduma ambayo vimezalishwa ndani ya nchi kujali Nani ambaye amezalisha Kwa kutuma exchange rate rasmi ya nchi husika
GDP per Capita hii Inapima pato la MTU mmoja mmoja Kwa kuchukua GDP ya nchi na kugawanya Kwa idadi ya watu.
GDP per Capita pia hutumika kielelezo cha kuonyesha standard of living the same to GNI per capita- na hivi ndio Kipimo kinachotumika na serikali nyingi kuonyesha improvement ya uchumi
Kama GDP per capita NI ndogo na inapitwa na nchi nyingine inamaanisha GDP hakuwai ama imekuwa kidogo ukilinganisha na nchi nyingine
GDP PPP haijaundwa Kwa sababu ya weakness ya per capita Bali na wala hainyoshi ustawi WA watu kama ulivyodai.
Maana hata GDP PPP kuna GDP PPP per capita.
GDP PPP imeundwa Kwa sababu ya tofauti ya tofauti ya exchange rate za currency na cost of living kutofautiana nchi na nchi.
Yaani GDP PPP Inapima GDP Kwa kuangalia gharama ya hiyo bidhaa iliyozalishwa nchini kwako kwenye nchi nyingine tuseme marekani.
Kwa mfano nimelima maNanasi mawili hapa nchini ambayo thamani yake ni sh 2000 ambayo ni Sawa na $0.7 na mkulima WA marekani akalima nanasi moja ambayo Kwa kule ni $2.
KWa kutuma GDP mimi niliyelima maNanasi mawili uchumi wangu ni 0.7, ambayo ni ndogo kuliko $2 ya nanasi moja USA.
Kwa Kipimo cha GDP PPP uchumi wangu ungekuwa $4, ndio maana china ina uchumi mkubwa duniani Kwa vipimo vya GDP PPP Kwa sababu wanazalisha vitu vingi Sana lakini sio vyote vinauzwa kwenye soko moja la USA. Ndio maana china wenyewe wapendelea zaidi kutumia nominal GDP
Hata GDP PPP haielezei welfare ya watu Bali ni adjustment ya exchange rate.
Pili uchumi WA Tanzania iwe kwenye nominal GDP ama vyovyote ukuaji wake umekuwa na shida na imeshindwa kufikia malengo yaliyoanishwa kwenye dira ya maendeleo ya vison 2025.
Malengo yalikuwa..
Uchumi WA Kati WA $3000 GDP per capita
Ukuaji WA uchumi WA 8% na GDP per capita ya 5% Kwa mwaka,,
Kati ya 2023-2024 GDP per capita imekuwa Kwa chini ya 2% Tu na uchumi kiujumla ni Kati 3%-4%, ndio muda tz imekuwa na tatizo kubwa ukosefu WA dola ya kutosha na tatizo umeme.
Ambapo Tanzania kwenye GDP PPP bado inafanya vizuri kuliko Uganda na kama haitoshi na bado kwenye nominal GDP iko vizuri zaidi ya Uganda
Kati 2018-2023 GDP ya Uganda imekuwa ilikuwa 5.2% na 6.3 ambayo Tanzania Kwa muda mwingi ni 5%. Hivyo TZ wala haifanyi vizuri kuliko ya Uganda in terms of GDP japo TZ ina uchumi mkubwa. Ambayo onezeko GDP Kwa ug imekuwa karibu dola bil 4-5 Kwa mwaka, wakati tz ni bil 3-4.
Kama yakiwa hivi Uganda itaipita GDP ya TZ miaka ya mbeleni ndani ya miongo miwili