Pato la taifa la Uganda (GDP) yaizidi ya Tanzania kwa mwaka 2025 kwa mujibu wa shirika la fedha duniani -IMF

Pato la taifa la Uganda (GDP) yaizidi ya Tanzania kwa mwaka 2025 kwa mujibu wa shirika la fedha duniani -IMF

Kaguta mseveni Yuko makini sana kwenye uchumi wa Nchi yake.Siyo sisi Huku tunamrembua macho tu
 
Mama Damaso haupigi huo mwingi? Asingeupiga huo mwingi ungekuwepo wewe leo? Siku moja moja amkeni na akili zenu basi wasifieni hata Mama zenu nao wajisikie angalau
Au sio?! Kwamba Samia ni Mama yangu?!
 
Waganda wengi wanapambana katika kukuza uchumi wao
Tofauti na sisi kutwa kulia ajira na huku wahusika hawajui njia za kufanya waendelee
 
Au sio?! Kwamba Samia ni Mama yangu?!
Mama Domaso Sa100 sio mama yako hajakuzaa wewe Sa100 watoto wake ni Wanu Amir Hafidh, Abdul Amir Hafidh, na wengine wewe haupo kwenye list ya watoto wake
 
Haishangazi, GDP per capita ya Tanzania imekuwa na onezeko dogo Sana tangu 2016, mwenendo WA uchumi WA Tanzania chini ya Samia sio mzuri kabisa hata Kwa kumtazama exchange rate ya tZ ndani ya mwaka mmoja utaliona hili.

Acha uzushi wa kitoto basi,kwamba wastani wa ukuaji wa GDP awamu ya 6 na 5 ni 2.1 & 3% Kwa takwimu za chanzo kipi hasa?

Wastani wa ukuaji wa Uchumi kuanzia 2021 umekuwa ni 4% na hii ni sababu za Hali ya kidunia na so vinginevyo.

Hata hivyo Tanzania imekuwa na ukuaji mzuri kushinda Nchi zote za EAC Kwa miaka yote Toka 2021 isipokuwamwaka Jana na juzi baada ya Uganda kuanza kula hela za Mafuta.
 
Ila Nchi yenu ndio Marekani ya Afrika au sio?
Tanzania ikikohoa EAC lazima wastuke wote.

Hao Uganda wanabumbuliwa na hela za Mafuta na hapo Bado Iko projected kufikia 11% ya growth lakini kwenye Haki halisi ya income disparity, unemployment wako hovyo kabisa.
 
Waliopo madarakani wakaona njia ya kupata pesa ni kuchapisha pesa mpya!
 
Nilikuwa na wasiwasi na hili jambo kwa muda mrefu sana naona linatokea.

Hivi majuzi naona nao wametangaza kuanza ujenzi wa SGR tokea mwezi March.

Tusipokuwa makini tutaburuza mkia hapa E.A.

Hata Burundi wakitulia watatupiga bao.
 
Tofauti ya watu around 10million sio kitu cha kujitetetea, Tanzania ilipaswa iwe mbali sana, ni aibu kujilinganisha na viinchi vidogo vidogo kama Uganda au hata Kenya.
Tanzania ni nchi kubwa sana na yenye kila aina ya raslimali.
Mume ni daktari na mke ni mwalimu wa sekondari. Wana watoto watatu. Jumla ya pato ni million 10 kwa mwezi. Wastani wa kipato ni million 2 kwa kila mwanafamilia kwa mwezi.
Mume ni Mwalimu wa sekondari na mke ni mwalimu wa shule ya msingi. Wana mtoto mmoja. Pato ni million 6 kwa mwezi. Wastani ni million 2 kwa kila mwanafamilia.
Familia ipi itakuwa na maisha mazuri zaidi?
All factors constant.
 
Zinapikwa wapi?

Kwamba zikiegemea positive zimepikwa.ila.zikiegemea hasi hazijapikwa 😂😂

Zero brain
Na haziwezi kupikwa ili ziegemee negative sasa kama ni hivyo basi hamna haja ya kupika.
 
Unafahamu weakness ya kutumia GDP per capita?

Unafikiri inakupa hali halisi ya welfare au standard of living ya watu katika nchi husika?
Nazifahamu zote, GDP(GNI) kiujumla inadeal na quantity hai-count vitu vingi kama income distribution.
 
Na haziwezi kupikwa ili ziegemee negative sasa kama ni hivyo basi hamna haja ya kupika.
Taarifa za deni la Taifa ambalo alikuwa anaongea Mpina zilitoa wapi?

Juzi kamati ya Bunge imeeleza hasara kibao za ATCL zimetoka wapi?

CAG Huwa anatoa taarifa gani?

Punguzeni ujinga basi
 
Acha uzushi wa kitoto basi,kwamba wastani wa ukuaji wa GDP awamu ya 6 na 5 ni 2.1 & 3% Kwa takwimu za chanzo kipi hasa?

Wastani wa ukuaji wa Uchumi kuanzia 2021 umekuwa ni 4% na hii ni sababu za Hali ya kidunia na so vinginevyo.

Hata hivyo Tanzania imekuwa na ukuaji mzuri kushinda Nchi zote za EAC Kwa miaka yote Toka 2021 isipokuwamwaka Jana na juzi baada ya Uganda kuanza kula hela za Mafuta.
Nadhani umeni-quote vibaya na ume-refer hiyo linki ambayo imezungumzia wastani wa ukuaji WA GDP per capita na hoja yangu iko hapo

Hizi ni data kutoka IMF

2021 - USD 1140
2022- USD 1210 ongezeko la 5.7%
2023-USD 1250 ongezeko la 3.3%
2024 - USD 1220 pungufu Kwa 2.4% (-2.4)
Wastani WA ukuaji WA GDP per Capita ya TZ kwenye miaka mitatu ni 2.2%,

Mzee hata haishangazi GDP per capita ya Uganda kuipita TZ
 
Sasa kwa akili zako 10 million ni ndogo?

Halafu GDP per capita sio kipimo sahihi cha kupima strength ya uchumi wa nchi

Mfano China's GDP per capita ni ndogo ukilinganisha na mataifa mengine lakini inapokuja kwenye suala la nominal GDP ni taifa namba 2 kwa uchumi mkubwa duniani.

Nominal GDP ndio kipimo hasa cha strength ya uchumi wa nchi kingine ni GDP in Purchasing Power Parity (GDP PPP)

Tulinganishe Uganda na Tanzania tuone ipi iko vizuri

Tanzania GDP PPP: USD 2,787
Uganda GDP PPP: USD 2,339

Tanzania is ahead of Uganda in both basic aspects of strong economy


Aibu sana, sasa hiyo tofauti ndogo hapo inakupa usingizi??
 
Back
Top Bottom