Patrick Aussems ameibadilisha sana Simba SC

Patrick Aussems ameibadilisha sana Simba SC

Wazee wa tathmini , hata mzunguko wa pili bado mshaanza mambo yenu.

Tatizo Bongo kila mtu mchambuzi.
 
Ulichoongea ni ushabiki wa kijinga tutaona hao wabrazili Kama watadumu hapo Simba zaidi ya mwaka mmoja
Kweli wewe shabiki maandazi aisee..yani unataka kila mtu akubaliane na utumbo ulioandika hapo juu?? Sijui kama kweli wewe ni shabiki wa mpira achilia mbali kuwa shabiki wa Simba.
 
Hivi nyie huwa mnaongea kitu ambacho hamna habri nacho. Madhaifu ya timu ya Simba ni yapi?
Simba msimu huu haijafungwa na timu yoyote.
Kweli kutolewa CAF champion ni kumevuruga malengo ya Klabu, Lakini lazima tukubaliane kua Kwenye mpira hilo jambo la kawaida.
Sisi wanasimba tunatakiwa tushikane ili kutetea ubingwa wa Tanzania ili mwakani tuendelee na malengo ya timu.
Shida watu mnaingizwa Kwenye porojo za vipensi fc, hao saizi wanatafuta wapi pa kujificha baada ya nao kutolewa.
@ Simba nguvu moja
 
Mwakani tena tunapeleka timu 4 CAF msihofu huyo 5imba atacheza tu msiumie roho
 
Wenzio mliokuwa nao walifungwa magoli 10+?
Ni sawa na mwanachuo aliemaliza degree ya kwanza kwa kupata sup 7 na carry 2 GPA 1.8.
Vita alitufunga 5 lakini akashika mkia kwenye kundi hilo hilo, Simba ikatinga robo fainali
 
Fraga(kiungo mkabaji haswaa) unamuona afai kwasabau hana mbwembwe za kupiga kanzu,tobo ila ni mchezaji mwenye kutekeleza majukumu yake uwanjani. Ila ni mchezaji mzuri tu.

Je nikikuuliza Fraga alichokosea nini kwenye mechi alizopangwa mkuu.
Jamaa hajui mpira, Fraga anakaba sana na hana madoido anacheza mpira wa kufundishwa, wengi hawalielewi hilo. Anajua ni kwanini kocha anampanga sana kwa sasa.
 
Hahaa nadhani hili ni jibu sahihi kabsa

5imba wanajipima uwezo na Vilaza halaf wakikutana na team ya kawaida kama UD SONGO wanapigwaa

endeleeni kusubiri msimu ujao
Simba were the quarter finalists in the African Club Championship, huko hawakukutana na timu mbovu za ligi kuu ya bongo.
 
Wenzio mliokuwa nao walifungwa magoli 10+?
Ni sawa na mwanachuo aliemaliza degree ya kwanza kwa kupata sup 7 na carry 2 GPA 1.8.
Lakini degree si amepata? Huwezi kumlinganisha na mwenye Diploma. Hata hivyo kazini hawahitaji kujua ulisup au hukusup wanachotaka ni degree na utendaji wako. Be pragmatic dogo.
 
Jamaa hajui mpira, Fraga anakaba sana na hana madoido anacheza mpira wa kufundishwa, wengi hawalielewi hilo. Anajua ni kwanini kocha anampanga sana kwa sasa.
Kabisa hajui mpira jamaa.

Anataka kiungo mkabaji awe na mbwembwe za kanzu, tobo ndio anajua mchezaji katimia
 
Mwanzoni Simba ilikuwa inacheza pasi fupifupi na taratibu baada ya ujio wa Patrick aussems Simba inacheza pasi za haraka na counter attack.

Lakini pia kitendo chake cha kuwapa nafasi karibia wachezaji wake wote kwenye kikosi chake kwa lugha nyingine anafanya rotation makocha wachache Sana wanafanya hiv. Ila kwenye CAF champion league ameangushwa na usajili wa miemuko wa viongozi wa Simba.

Hivi inaingia akili kwel unamsajili Deo Kanda mcheza na jukwaa unamuuacha Okwi mzee wa kazi,unamuuacha Haruna Niyonzima unamsajili Shubob wakati kulikuwa hakuna ulazima wakufanya hivo,wale wabrazili ndo takataka kabisa hata sitaki kuwazungumzia unaona kazi anayofanya Kenneth Juma anajua kutumia urefu wake vizuri anawin mipira yote ya juu tumeona kwenye mech ya Jana kiasi ambacho Wawa akawa kama yupo likizo lakini Lile librazili Gerson ni mrefu lakini hajui kutumia urefu wake lakini mara nyingi anakuwa out of position.

Unaenda kumsajili kiungo wa kibrazili ambaye hata robo ya uwezo wa Kotei hana hii ni akili au matope.

NB: next time uongozi wa Simba msifanye usajili wa miemuko ili mumsaidie Patrick Aussems kufanya kazi yake kwa ufanisi.
mikia FC hiyo.
 
Tunataka Mshambuliaji Wilka acheze Mpira.
Tumechoka kuto mwona uwanjani.
Tumechoka na janjajanja
 
Ukitaka ujue simba mbovu icheze na timu inayojitambua,honestly ligi yetu ni mbovu sana,yaani ukiangalia mechi zinatia kinyaa maana hazina mvuto na kiwango kibovu sana.
 
Naungana nawe mkali, unawaacha wachezaji zaidi ya sita alafu unasajili wngn kupitia picha za youtube c usenge huu ndy maana this time simba imefeli mapema sana
Mwanzoni Simba ilikuwa inacheza pasi fupifupi na taratibu baada ya ujio wa Patrick aussems Simba inacheza pasi za haraka na counter attack.

Lakini pia kitendo chake cha kuwapa nafasi karibia wachezaji wake wote kwenye kikosi chake kwa lugha nyingine anafanya rotation makocha wachache Sana wanafanya hiv. Ila kwenye CAF champion league ameangushwa na usajili wa miemuko wa viongozi wa Simba.

Hivi inaingia akili kwel unamsajili Deo Kanda mcheza na jukwaa unamuuacha Okwi mzee wa kazi,unamuuacha Haruna Niyonzima unamsajili Shubob wakati kulikuwa hakuna ulazima wakufanya hivo,wale wabrazili ndo takataka kabisa hata sitaki kuwazungumzia unaona kazi anayofanya Kenneth Juma anajua kutumia urefu wake vizuri anawin mipira yote ya juu tumeona kwenye mech ya Jana kiasi ambacho Wawa akawa kama yupo likizo lakini Lile librazili Gerson ni mrefu lakini hajui kutumia urefu wake lakini mara nyingi anakuwa out of position.

Unaenda kumsajili kiungo wa kibrazili ambaye hata robo ya uwezo wa Kotei hana hii ni akili au matope.

NB: next time uongozi wa Simba msifanye usajili wa miemuko ili mumsaidie Patrick Aussems kufanya kazi yake kwa ufanisi.
 
Kila mtu humu anaujua mpira kuliko team ya simba, sasa sijui mnacheza ligi gani bora zaidi ya hii VPL
 
Aussens angekuwa kocha AL Ahly ya Misri alafu timu itoke awali angewatambua waarabu..
 
Rekebisha andiko lako Kwanza ndio tuendelee, gerson ndio mbrazil mrefu?? Shwaini
 
Kwa Fragas na Deo Kanda sijui wenzangu mnatumia vigezo gani. Wachezaji wapya wanaposajiliwa tunategemea wawazidi wale waliowakuta na waliondoka. Tukianza na Fragas je anakitu gani cha kumzidi sana Mkude pamoja na mapungufu yake? Je Kotei angekuwepo huyo Fragas angemuweka benchi. Tukija kwa Deo Kanda tulitegemea yeye ndio azibe pengo la Okwi lakini maajabu Miraji Athumani ndio anaziba pengo.

Tunapowazungumzia Deo Kanda na Fragas hatuna maana ni wachezaji wabaya hapana bali ni wachezaji ambao waliletwa ili kuiongezea Simba ufanisi lakini viwango vyao ni vya chini kulinganisha na wachezaji wazawa na wageni wenzao waliowakuta. Kwani tunategemea mchezaji mgeni akija alete ufundi ambao utawapa changamoto wachezaji wazawa. Na kwa Deo Kanda ndio kwanza benchi linamhusu atamfuata mwenzie Kahata kwenye mbao ndefu muda si mrefu kadiri injini ya Miraji inavyopata moto.

Ni wakati sasa viongozi wa Simba wakae chini na Miraji wamuongezee mshahara na marupurupu na wamfunge mkataba mpya wa muda mrefu wenye maslahi kwa pande zote mbili kwani umri unaruhusu na ameonyesha uwezo mkubwa kuliko hata wachezaji wa kigeni.

Na viongozi wasilaumiwe kwani unaweza kumuona mchezaji ni mzuri kwenye timu nyingine ukamsajili kwenye timu yako akacheza chini ya kiwango. Hata vilabu kama Barca, Madrid, Man U n.k. huwa vinakutana na tatizo hili.
Kwa wachezaji wa kibongo ninavyowajua hyo Dogo wakimuongezea mkataba na marupurupu kibao atabweteka na kujiona kafika....

Km unakumbuka kichuya alivyokuja simba alikuwa na moto wa hatari, walivyo mboreshea mkataba tu! Akaanza kuzingua
 
Back
Top Bottom