Mwanzoni Simba ilikuwa inacheza pasi fupifupi na taratibu baada ya ujio wa Patrick aussems Simba inacheza pasi za haraka na counter attack.
Lakini pia kitendo chake cha kuwapa nafasi karibia wachezaji wake wote kwenye kikosi chake kwa lugha nyingine anafanya rotation makocha wachache Sana wanafanya hiv. Ila kwenye CAF champion league ameangushwa na usajili wa miemuko wa viongozi wa Simba.
Hivi inaingia akili kwel unamsajili Deo Kanda mcheza na jukwaa unamuuacha Okwi mzee wa kazi,unamuuacha Haruna Niyonzima unamsajili Shubob wakati kulikuwa hakuna ulazima wakufanya hivo,wale wabrazili ndo takataka kabisa hata sitaki kuwazungumzia unaona kazi anayofanya Kenneth Juma anajua kutumia urefu wake vizuri anawin mipira yote ya juu tumeona kwenye mech ya Jana kiasi ambacho Wawa akawa kama yupo likizo lakini Lile librazili Gerson ni mrefu lakini hajui kutumia urefu wake lakini mara nyingi anakuwa out of position.
Unaenda kumsajili kiungo wa kibrazili ambaye hata robo ya uwezo wa Kotei hana hii ni akili au matope.
NB: next time uongozi wa Simba msifanye usajili wa miemuko ili mumsaidie Patrick Aussems kufanya kazi yake kwa ufanisi.