Patrick Mwalunenge (Mwenyekiti CCM Mkoa wa Mbeya) Atinga Site na Vipimo Kutatua Mgogoro wa Fidia Ujenzi wa Barabara Njia Nne

Patrick Mwalunenge (Mwenyekiti CCM Mkoa wa Mbeya) Atinga Site na Vipimo Kutatua Mgogoro wa Fidia Ujenzi wa Barabara Njia Nne

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

PATRICK MWALUNENGE (MWENYEKITI WA CCM MBEYA) ATINGA SITE NA VIPIMO, KUTATUA MGOGORO WA FIDIA UJENZI WA BARABARA NJIA NNE

Mwenyekiti wa chama Cha mapinduzi CCM Mkoa wa Mbeya amefika eneo la takio na vipimo baada ya Wananchi wa kata za Nzovwe na Mabatini Mkoani himo kulalamika kitendo Cha kutolipwa fidia na serikali licha ya kusimamisha uendelezaji wa makazi yao na shughuli nyingine za kiuchumi kwa zaidi ya miaka kumi na mbili kutokana na mabadiliko ya sheria ya hifadhi za barabara ya kuongeza mita saba mbele kutoka mita 22.5 za awali.

Wananchi hao wamepaza kilio hicho kwa chama Cha mapinduzi Mkoa wa Mbeya na kuiomba serikali kuwalipa fidia zao, ambapo wamedai walifanyiwa tathimini ya nyumba zao toka mwaka 2012 na Sasa tayari utekelezaji wa ujenzi njia nne za barabara umeanza ili hali wao Bado hawajui hatma yao, Jambo lililobebwa na chama Cha mapinduzi CCM Mkoa wa Mbeya na kuahidi kulifanyia kazi.

Mhandisi Matari Masige ni meneja wa wakala wa barabara TANROADS Mkoa wa Mbeya, amesema serikali ipo kwaajili ya kutenda haki na hakuna mwananchi yeyote atakaye onewa, hivyo atakaye guswa na mradi wa barabara njia nne lazima atalipwa fidia kwa mujibu wa tathmini za serikali.

maxresdefaultzxcderwqa.jpg
 
Back
Top Bottom