Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Wachambuzi wa kivita wa Marekani wamekiri kuwa mfumo wa Patriot pamoja na sifa zake kadhaa lakini si mfumo salama mbele ya jeshi la Urusi.
Mtambo huo wa Patriot kimsingi umeundika na vitu sita katika ufanyaji kazi wake ambavyo ni generators, radar set, control station, antennas, launcher station na interceptor missiles.
Vitu hivyo sita vinaweza kutandazwa kila kmoja pake kuanzia mita chache mpaka kilomita kadhaa na kila mtambo mmoja unahitaji kikosi cha watu zaidi ya 100 kuuendesha hata kama wako mbali mbali.
Adui akiweza kuharibu kifaa chochote kimoja kati ya hivyo basi hata kama hasara ya kifaa si kubwa lakini atakuwa ameuharibu mtambo mzima usiweze kufanya kazi .
Sehemu ya mtambo huo ambayo ndiyo dhaifu zaidi kuweza kupigwa ni launcher station na ambayo ndiyo inayoipa sura yake halisi mbele ya macho ya watazamaji.Kasoro ya kifaa hicho ni kuwa kwanza ili iweze kufanya kazi yake vizuri basi haiwezi kufichwa vichakani.Daima inapokuwa ipo mawindoni kuyangoja makombora ya adui basi huwa inatoa sauti kama king'ora na mionzi ambayo ni rahisi sana kugunduliwa na droni na vifaa vyengine vya kipelelezi vya adui.
Ni kweli kuwa kombora hatari la hypersonic la Urusi ambalo Marekani hajafanikiwa kulitengeneza laweza kudunguliwa na Patriot lakini ni pale tu linapokuwa liko karibu na kutua kwenye shabaha yake na wala si linapokuwa likisafiri angani kuelekea hapo.