Patrobas Katambi "adindishiwa" na mwananchi

Patrobas Katambi "adindishiwa" na mwananchi

Hawa maafisa waache ulimbukeni bhana, waheshimu wananchi kwani ndo wanatengeneza nchi inayowafanya wawe maafisa....sijui watu wasiojulikana.
 
Hivi Naibu waziri ana mamlaka ya kuagiza kukamata mtu na kumuweka ndani kwa vile wamepishana kauli?
Nielimishwe.
 
Watu wamechoka! Katambi alianza kwa kusema "huo ujinga fanyia wengine".

Mwananchi akaonya na kupinga vikali kutukanwa (kuambiwa mjinga) hadharani. Na Katambi alipoamuru polisi wamkamate mwananchi aliamua kukaa chini.

Tazama video hii ya nusu dakika ujionee mwenyewe.

View attachment 1861876
Mbaya sana kuwa kiongozi kunafanya uone ataa wakubwa zako wajinga !?
 
Ila viongozi tusimlaumu Waziri. Kwa tuliokuwepo eneo la tukio huyo kwanza sio mwananchi ni Afisa wa Serikali ambaye ni mmiliki wa Bar na Hotel maarufu hapa Shinyanga. Kuna mwananchi alilalamika kuwa Afisa huyo amepora eneo Lake na kuwekeza ujenzi wa ukuta kuzunguka hotel yake.

Ndipo Waziri Katambi alimtaka huyo mmiliki(Afisa mifugo, hapa mmemwita mwananchi) kutoa ufafanuzi. Badala ya kujibu madai ya mwananchi anayemlalamikia yeye akawa anajibu vinginevyo. Kukatokea majibishano mabaya baina ya huyo Afisa na Waziri.

Kwa ufupi Afisa alijibu vibaya, japo nalaani hatua alizochukuliwa lakini hakupaswa kumjibu vile Waziri.

Na mnaofikiri huyo mwananchi ni raia wa kawaida, mjue kuwa huyo ni Afisa Mifugo na mfanyabiashara mwenye bar na hotel maarufu hapa Shinyanga. Na malalamiko ya huyu mwananchi aliyeporwa eneo ni ya miaka mingi sana lakini hakuna msaada wowote wa kisheria aliopatiwa considering kwamba alinyang'anywa eneo na mtu ambae ni giant.

Tusihukumu kwa kutumia incomplete infos. Kwa mashuhuda wengine waliokuwepo wanaweza kunisahihisha. Tujifunze kuheshimu viongozi, kulikuwa na majibishano mengine zaidi ya haya yaliyorekodiwa.
Upo sahihi,watu wanamtetea Huyu vellan mwaluko bila kujua ukweli.Huyu jamaa ana kiburi na dharau sana.Laiti watu mngeona namna alvyokua anatumia nguvu yake yakifedha vibaya msingemtetea namna hi.Hii kesi ilifika mpaka mahakani,hiyo haitoshi mahakama ikasimamisha ujenzi lakini huyu mtu akawa anachukua polisi wenye silaha kutisha walalamikaji anaweka na mafundi wanaendelea na ujenzi licha ya zuio la mahakama.Hiyo haitoshi kesi ikiwa inaendelea mahakaman anawawahi mashahidi wa mlalamikaji pembeni anawaweka sawa wanaacha kutokea,ata majuzi Kuna watu waliitwa ofisi ya mkuu wa mkoa kila mmoja hakutokea akawa anatoa Sababu zake za uongo kutohudhuria,na wengine walipigiwa simu nakuchengesha kua mawasilaona yanashida.Hiyo haitoshi baada yakutoka lockup ya hili sakata la juzi bado anatoa maneno yakashfa kwa katambi nakua atamuharibia kazi,(Arejee tambo zake mahakama ya mbuzi Jana).Wote wamekosea
 
Katambi mpuuzi sana, huyo Anayemuita mjinga ana weza kuwa ni 'saizi' ya mume wa mama yake.
Apunguze 'hang over' na ulevi wa kiki za mwendazake.
AKili ya katambi ipo kimnadani nadani tu. Tuna watu wamepata akili ya ujanja mapema ya kuigiza u ccm kindaki wakiona fursa ya shotikati za ajira nauongozi, kichwani hakuna kitu. Ni sawa na kujindai mkristo kumpita Kristo mwenyewe. Kiongozi/Rais mkuu katika nchi Hana LUGHA ZA KIFEDHURI KWA WANANCHI NYINYI MNAO TEULIWA KUMSAIDIA MNAZITOA WAPI? " Usiniletee Ujinga wako, unaongea kiongozi wa chama na serikali kwenye mkutano wa Umma" kisha unaelekeza polisi weka jela huyu....nini ? Mkoloni mzawa wewe? Lameki naye anazungusha kiti KIFEDHURI anasema anayeona hawezi kulipa tozo yake aliyosomea phd akaishi Burundi..... jiangalieni wananchi Hawa.... "Siku yako ipo mwanangu nimekuwekea, utakapogeuka upepo usije kulia"
 
Kadhia hizi kwa wanachi waliojichokea na wenye misimamo yao huletaga matokeo mabaya sana. Zama hizi haitofautiani na zama za kuujenga ujamaa wa mwalimu. Historia ya mkuu wake mkoa na Iringa Dr Cleruu na mkulima mzee Mwamindi iwatafakarishe Viongozi walevi es madaraka....
 
Ila viongozi tusimlaumu Waziri. Kwa tuliokuwepo eneo la tukio huyo kwanza sio mwananchi ni Afisa wa Serikali ambaye ni mmiliki wa Bar na Hotel maarufu hapa Shinyanga. Kuna mwananchi alilalamika kuwa Afisa huyo amepora eneo Lake na kuwekeza ujenzi wa ukuta kuzunguka hotel yake.

Ndipo Waziri Katambi alimtaka huyo mmiliki(Afisa mifugo, hapa mmemwita mwananchi) kutoa ufafanuzi. Badala ya kujibu madai ya mwananchi anayemlalamikia yeye akawa anajibu vinginevyo. Kukatokea majibishano mabaya baina ya huyo Afisa na Waziri.

Kwa ufupi Afisa alijibu vibaya, japo nalaani hatua alizochukuliwa lakini hakupaswa kumjibu vile Waziri.

Na mnaofikiri huyo mwananchi ni raia wa kawaida, mjue kuwa huyo ni Afisa Mifugo na mfanyabiashara mwenye bar na hotel maarufu hapa Shinyanga. Na malalamiko ya huyu mwananchi aliyeporwa eneo ni ya miaka mingi sana lakini hakuna msaada wowote wa kisheria aliopatiwa considering kwamba alinyang'anywa eneo na mtu ambae ni giant.

Tusihukumu kwa kutumia incomplete infos. Kwa mashuhuda wengine waliokuwepo wanaweza kunisahihisha. Tujifunze kuheshimu viongozi, kulikuwa na majibishano mengine zaidi ya haya yaliyorekodiwa.
Lakini vipi yeye katabi alifuata taratibu za usuruhishi au na yeye alileta mihemuko. Kiujumla tukio lile sio zuri panda zote ila inakula zaidi kwa katabi kwasababu kwanza yeye waziri pili mgogoro wenyewe na wa muda mrefu na unajulilana kwaiyo kulikua hakuna haja ya kuzungumzia barabaran kwanini wasiitane ofisini kila mtu akiwa ametulia
 
Swadaktaaaa!!
 
mbona video imekatwa kihuni huni!!!!

lakini mwananchi kwa kumwangalia tu si mtu mpuuzi mpuuzi kama wafuasi wa chadema, atakuwa na hoja ya msingi kukataa kutukanwa.
Katambi aliagizwa jamaa awekwe ndani hapohapo na alikalishwa chini baadae sijui kilichotokea
 
Watu wamechoka! Katambi alianza kwa kusema "huo ujinga fanyia wengine".

Mwananchi akaonya na kupinga vikali kutukanwa (kuambiwa mjinga) hadharani. Na Katambi alipoamuru polisi wamkamate mwananchi aliamua kukaa chini.

Tazama video hii ya nusu dakika ujionee mwenyewe.

View attachment 1861876

Safi kabisa na angemtwisha ndoo ya haja. Wapuuzi sana hawa 😂😂😂😂.
 
Watu wamechoka! Katambi alianza kwa kusema "huo ujinga fanyia wengine".

Mwananchi akaonya na kupinga vikali kutukanwa (kuambiwa mjinga) hadharani. Na Katambi alipoamuru polisi wamkamate mwananchi aliamua kukaa chini.

Tazama video hii ya nusu dakika ujionee mwenyewe.

View attachment 1861876
Ni vema jeshi la polisi likaacha kutumika namna hii, na ni aibu kuwa na kiongozi anayefikiri kuwa jeshi la polisi ni chombo cha kuadhibu wananotofautiana na mwanasiasa kwenye jukwaa la sissa
 
Back
Top Bottom