Prof Phraoh AI
JF-Expert Member
- Mar 25, 2024
- 1,269
- 2,311
Paul Dirac anajulikana kama mmoja wa waanzilishi wakuu wa quantum mechanics, lakini simulizi za watu waliomfahamu zinaonyesha alikuwa mtu mwenye aibu sana na aliyekwepa attention na umaarufu kwa gharama yoyote.
Katika kumbukumbu na wasifu wake zilizohifadhiwa Cambridge alipokua akifundisha, inaonyesha alikua ni mtu mkimya kupindukia.
Mwaka 1933 alipoambiwa kwamba ameshinda Tuzo ya Nobel pamoja na Erwin Schrödinger, alifikiria kuikataa ili kuepuka attention na umaarufu.
Lakini watu wake wa karibu wakawa wanamshauri asiikatae. Mtu mmoja akafanikiwa kum convice kwa kumwambia kwamba kuikataa Nobel ndo kungezua gumzo kubwa zaidi. Angekua ni mwanasayani wa kwanza kuikataa Tuzo ya Nobel ya Physics na kwamba ndo ingesababisha ajadiliwe zaidi na attention ingekua kubwa zaidi, hivyo Dirac akaamua kuipokea.
Story nyingine inamuelezea akiwa kwenye dinner party ya watu wa science yeye alikua amekaa kimya kwa muda mrefu sana, mwenyeji wao alimfata akamuuliza,
“Professor Dirac, are you enjoying yourself?”
Dirac akajibu: Yes, kisha baada ya muda wakashangaa Dirac hayupo ameshaondoka kwenye Party.
tukio lingine maarufu ni alipokua professor Cambridge aliombwa aandike recomendation letter, ila sasa kwenye hiyo barua aliandika sentensi moja tu
“X is a good physicist.”
Wenzake walikua wanamtania wakasema SI Unit ya maneno ambayo mtu anaweza kuongea kwa saa inaitwa Dirac, kwaiyo Dirac = neno moja kwa saa.
Licha ya kukwepa sifa na spotlight, mchango wake kwenye sayansi ulikuwa mkubwa sana. Aliunda Dirac equation iliyounganisha quantum mechanics na special relativity, na kupitia hesabu zake alitabiri uwepo wa antimatter miaka 100 kabla haijathibitishwa maabara.
Kazi yake iliweka msingi muhimu wa quantum field theory na particle physics, na imeendelea kuathiri vizazi vya wanasayansi hadi leo. Mwishowe, hadithi hizi hazionyeshi tu aibu yake, bali zinaonyesha akili ya kipekee iliyokuwa inaamini kwamba ukweli ni kama hesabu hauhitaji maneno mengi.
Dirac ni moja ya wanasayasi wakubwa zaidi physics ambao unaweza kuwaweka level moja na Newton na Einstein
Equation yake ni hii: (iγμ∂μ−m)ψ = 0
iliyotabiri uwepo wa antiparticle miaka 100 kabla haijathibitishwa maabara !