al-baajun
JF-Expert Member
- Sep 11, 2015
- 283
- 209
Siku hizi kila mtu anazungumzia Kagame kwa mabaya, mara ooh ni dikteta, mara anatufanyia figisu, mara atoke madarakani. Lakini wachache sana wanajua ukweli wa historia yake na jinsi Tanzania ilivyoshiriki kwenye safari yake ya kuwa kiongozi mkubwa barani Afrika.
Kwanza kabisa, Kagame si mtu wa kuokoteza. Jamaa alipikwa vizuri sana na Tanzania, tena na jeshi letu wenyewe. Miaka ya 70 na 80, Tanzania ilikuwa base kubwa kwa wapigania uhuru wa Afrika. Hapo ndipo akina Kagame na Museveni walikuja kupata mafunzo ya kijeshi na ujasusi. Tena si mafunzo ya kawaida, ilikuwa ni full intelligence training,mbinu za vita, ujasusi, na jinsi ya kuendesha mapambano ya msituni. Hivi vitu vilimwandaa Kagame hadi akawa yule jamaa aliyesimama kidete wakati wa vita vya Rwanda.
Leo watu wanamsahau haraka na kumchora kama adui. Lakini ukweli ni kwamba Kagame ana heshima kubwa kwa Tanzania. Hata ukiangalia historia yake, mara nyingi amekuwa akisema wazi jinsi Tanzania ilivyomsaidia. Sasa hivi watu wanataka kumtupa kwenye shimo la propaganda bila hata kujua alikotoka.
Tanzania siku zote tumekuwa na mkono wa kusaidia wapigania uhuru. Hatukuwasaidia Kagame na Museveni tu, hata akina Samora Machel, Mugabe, na Mandela walihifadhiwa na kupikwa hapa. Hii ni legacy yetu kama taifa, hatuwezi kuipuuza eti kwa sababu ya siasa za leo.
Hata hizi idara zetu za usalama zilishafanya kazi kubwa sana. Leo hii Kagame ni mmoja wa viongozi wenye akili kubwa Afrika, na hilo halitokei kwa bahati tu. Kuna kazi ilifanyika nyuma ya pazia, na Tanzania ilikuwa sehemu kubwa ya hiyo kazi.
Kwa hiyo badala ya kuchukuliwa na propaganda za mitandaoni, tujue kwamba Kagame si mtu wa kubebwa kirahisi. Jamaa alikuwa na vision, akapitia magumu, na Tanzania ilikuwa sehemu ya safari yake. Tunabaki na tofauti zetu kisiasa, lakini tusimsahau kama sehemu ya historia yetu ya ukombozi wa Afrika.