Paul Kagame: Mwanajeshi Aliyelelewa na Tanzania, Shujaa wa Ukombozi wa Afrika

Mkuu, kwanza kabisa, kusema eti “Watutsi hawawezi kuwa reasonable beings” ni ushenzi wa hali ya juu. Huwezi ku-generalize watu wote kwa matendo ya viongozi wao. That’s like saying “all Tanzanians are corrupt” just because kuna mafisadi wachache wanakula nchi. Kila jamii ina watu wazuri na wabaya, na historia imetufundisha that power doesn’t belong to any one tribe, it belongs to those who can take it and keep it.

Now, let’s talk leadership. Watu wengi wanaamini eti democracy is the best system, lakini ukweli ni kwamba not everyone is born to lead. Kuna watu wana akili ya biashara, kuna watu wana akili ya tech, na kuna watu wamezaliwa kuwa bora kwenye leadership. Ndio maana hadi leo bado kuna mfalme wa Uingereza, Sultan wa Oman, na Mfalme wa Saudi. Watu wengine huzaliwa na vipaji vya uongozi, hata kama mfumo wa kidemokrasia unajaribu kupinga dhana hiyo.

Demokrasia nayo ina mapungufu. Watu wanapopewa uhuru wa kuchagua kiongozi, mara nyingi wanachagua kwa hisia badala ya hekima. Wanasiasa hodari wanajua kucheza na hisia za watu, wakitumia propaganda kuwadanganya. Matokeo yake ni kwamba tunaweza kupata viongozi wabaya kwa sababu mfumo wa kura hauangalii hekima ya mgombea bali umaarufu wake. “The masses are too emotional to elect good leaders.” Plato

Halafu bro, another thing life sio fair. Kuna watu wanaingia kwenye power kwa connections, wengine kwa hard work, wengine kwa bahati, na wengine kwa kuwa wanajua kucheza mchezo. Ndiyo maana kwenye nchi kama Rwanda, Kagame aliingia kwenye game akiwa sharp upstairs, akajua kucheza siasa za Afrika, akajenga connections, na leo yuko hapo alipo. Whether watu wanampenda au hawampendi, the guy knows how to rule.

Na hii sio Rwanda tu, hata hapa kwetu Tanzania kuna watu wameweza kushika madaraka kwa sababu ya networks, ujanja, na ability ya kuwa na vision. Kama huwezi kuona mbele, utapotea tu. Ndio maana ukiangalia world politics, viongozi wenye charisma, ambition, na ruthless strategy ndio wanao survive.

At the end of the day, watu hawajali kama nchi inaendeshwa na dictator, mfalme, au rais wa kidemokrasia, as long as kuna peace na pesa inaingia mfukoni. People want security, food, education, and opportunities. Ndiyo maana hata kama China sio democratic, wananchi wake wanaendelea kuishi fresh kwa sababu uchumi unapaa.

So, instead ya watu kutumia energy kushambulia Watutsi wote just because of Kagame, tujifunze from history. Uongozi sio swala la kabila, ni swala la ability, vision, na power dynamics. Kama mtu anaweza ku-maintain stability, anaweza kucheza world politics vizuri, basi he will stay in power. Kama akikosea, history will take care of him. That’s how the world works. Ngoma ikivuma sana, mwisho wake ni kupasuka – hiyo ni nature ya power.
 
Leta hapa ushahidi wa Tanzania kumsaidia Kagame kushika nchi ya Rwanda sio mbaambaa za vijiweni

wakati mashambiulizi yote RPF yalitokea Uganda na Museveni kumpa wanajeshi wake
 
Leta hapa ushahidi wa Tanzania kumsaidia Kagame kushika nchi ya Rwanda sio mbaambaa za vijiweni

wakati mashambiulizi yote RPF yalitokea Uganda na Museveni kumpa wanajeshi wake
Sawa basi,

FRONASA na RPF ndiyo walijipa mafunzo ya kijeshi na kijasusi wenyewe, na wao ndiyo waliipindua serikali ya nduli IDD AMIN DADA na kujirudisha wenyewe kutawala UGANDA.
 
Hili bandiko lako linadhihirisha kabisa nilichokisema, MOST OF TUTSI ELITES ARE NOT REASONABLE BEINGS. Yaani niwe nina chuki na watutsi kwa kuzungumza ukweli wa kile kinachoendelea Rwanda ???
Typically, decrepit Tutsi Chauvinism.
Kwahiyo wewe unaamini kwamba Paul Kagame alizaliwa kutawala si ndiyo ???
Demokrasia nayo ina mapungufu. Watu wanapopewa uhuru wa kuchagua kiongozi, . “The masses are too emotional to elect good leaders.” Plato​
Plato hajawahi kusema hayo uliyoyanukuu hapa. Unaokoteza vitu mtandaoni na kuja kuvileta hapa bila kufahamu muktadha wa alichokuwa anakisema Plato.

Book Six of The Republic, Plato alikuwa anaelezea kuhusu mwalimu wake Socrates ambaye alikuwa haamini katika mfumo wa Demokrasia ya Athens, na akatoa mfano wa nahodha baharini na kusema siyo kila abiria kwenye meli anayetamani kuwa nahodha anaweza kufanya kazi za nahonda. Hivyo unaposema Plato alisema hivyo nakushangaa.

Halafu muktadha wa alichokisema Socrates kuhusu Athenian Democracy havishabihiani kabisa na ujinga wa madikteta wa Afrika. Socrates kupinga Athenian Democracy haimaniishi alipendekeza Wagiriki wafuate mfumo wa kidikteta, ila alipendekeza A Governance by Philosopher Kings, jambo ambalo ni mataifa machache mno yameweza kufanikiwa, na Rwanda siyo mojawapo.
Kagame failed in school, twice. Sasa sijui hizo akili unazozitaja hapa ni zipi.

Kuhusu kuongoza vizuri, hata Mobutu alisifiwa sana tena sanaa. Nikwambie tu ambacho wengi hamkifahamu ni kwamba, kipindi cha utawala wake, ndicho ambacho ZAIRE ilifika hadi kuwa ya pili kiuchumi barani Afrika, tena kutajwa kuwa na jeshi bora kabisa ukanda wa Sub-Sahara.
Inaonesha unaongea usichokifahamu vizuri. China is a COMMUNIST State, led by a single party, not whims of a single wannabe tyrant. Uchaguzi unaofanyika ndani ya CCP-Congress is more democratic and transparent than those conducted in GOP or DEM Primaries.

Huwezi kufananisha taifa kama Uchina na Rwanda, au RPF na CCP. Ndani ya CCP kuna demokrasia kubwa mno, kuliko ndani ya RPF. Kuanzia 2010, CCP iliwashindanisha Bo Xilai na Xi Jinping, ilhali Rwanda kina Ingabire au Rwigara wamechukua fomu tu, hadi wakwekwa ndani na ndugu zao kufyekelewa mbali.

Kagame is in power not because he's savvy or a shrewd prayer of geopolitics. It's because he's a faithful lieutenant of Western Corporate Interests, as Mobutu and Savimbi were. He is serving his purposes well, and they keep him on good graces.

But an Imperial Signature Move is this, once a pawn has outlived his usefulness you let him loose and cut of his leash. It happened to Pinochet, Pol Pot, Bokassa, Mobutu, Banda, Shah, and it may eventually happen again here in Africa.

Hivyo ni suala la muda tu.
 
Sawa basi,

FRONASA na RPF ndiyo walijipa mafunzo ya kijeshi na kijasusi wenyewe, na wao ndiyo waliipindua serikali ya nduli IDD AMIN DADA na kujirudisha wenyewe kutawala UGANDA.
Hata sijui unaongea nini mstaafu
Idd Amini hana uhusiano wowote na kuondolewa na RPF, Kina Kagame na Rwiygema walipigana kumtoa swahiba wa Nyrere, Obote
Huko Kagame alikopita Monduli ni kwa muda mfupi sana ambao hauna mashiko sana, ndio maana alipelekwa WestPoint na Museveni.
Kwa ujumla Tanzania haikusaidia chochote kwa RPF, na ndio maana fadhila zote analipa Uganda ambako alikuwa Mkuu wa ukachero jeshi la Museveni, na ndio maana hana time na TZ.
Sana tuseme yeye ndio kaisaidia Tanzania kwenye kumtoa Idd Amin akiwa na kikundi cha FRONASA kilichoongozwa na Museveni
Na huu ndio uhasama na Tanzania ulipoanzia katika Battle of Kabamba.....
Kagame akiwa kiongozi wa ambush na kukuta jeshi la TZ kama walinzi....

 
Kagame hajasoma Monduli na pia Kagame hakumaliza masomo yake WESTPOINT.

This is a Moth-Eaten-Second Class Propaganda.

NB: And Wikipedia is not a credible source of information.
 
Kagame hajasoma Monduli na pia Kagame hakumaliza masomo yake WESTPOINT.
Safi kabisa, I had vivid memory lakini alikuwepo na alichaguliwa
Kwahiyo inathibitisha kuwa hakuna msaada wowote wa mafunzo ya kijasusi unayotapatapa kuwa yalitolewa kwa Kagane ,kutoka Tanzania


NB: And Wikipedia is not a credible source of information.
Wikipedia ndio ilikuwa Chatgpt yetu sisi wakubwa wa leo, kumbuka sio wazee waleo, maana ndio nyinyi inaonekana mliokuwa mkiiponda wikipedia iliosaidia generation yangu kwa kupatika kwa elimu ya bure iliyoua mambo ya twisheni..
Na sisi leo tunaiponda chatgpt
Wikipedia ni lidude likubwa sana kwa wenye akili ya kujua taarifa gani wanaitafuta.....na hauna validity yoyote wewe mtu wa kutoka bara la giza, to dicredited the most visited site in the world for source of info or education.....
 
Acheni kujipendekeza. Kagame alilelewa Uganda. Hana ushujaa wowote kama mchango wake kwenye mauaji ya kimbari ukifukuliwa na kushghulikiwa. Hata ushujaa wowte ni sawa na mwalimu wake Museveni.
 
Hii ukipata na maandazi ya moto au chapat za moto saf sana
el
 
Hebu angalia unavyotapatapa kupiga propaganda.

Uliandika kwamba Paul Kagame alipita Monduli, saa hizi unageuka na kusema hakupita baada ya kushindwa kunidanganya. Msomi unatakiwa uwe na kauli moja, alipita Monduli au hakupita. Siku nyingine unafanya propaganda, First, know all the facts and nuances of the matter.

Sasa nikuulize tu: Ilikuwaje Uganda wamkatae Kagame kuwa mwanajeshi wao kisa unyarwanda wake lakini wakubali apewe mafunzo ya ujasusi ???

Hebu wewe mtaalamu nieleweshe vizuri.....
 
unamsifia mwizi wa madini?
 
Kagame amepita Monduli baada ya Museveni kuwa Raisi, na ndio kipindi hiki Museveni alimfanya kuwa mkuu wa ukachero jeshi la Uganda, get your fact right.......
Au wandikie barua BBC, kuwakosoa



Sasa nikuulize tu: Ilikuwaje Uganda wamkatae Kagame kuwa mwanajeshi wao kisa unyarwanda wake lakini wakubali apewe mafunzo ya ujasusi ???
Hapa unaongelea wakati wa utawala wa Obote,
Kagame amekulia ujana wake Uganda, huku akiishi kama raia wa Uganda
Ndio kipindi hiki alipata nafasi ya mafunzo Monduli,
Lakini kwa kuwa utawala wa Obote ulikuwa na uhasama na watusi wa Rwanda , ndio kukawa na kampeni ya kuwafukuza watusi wote waliokuwa serikalini na jeshini, na ndio hapa Kagame hakuweza kwenda Monduli kwa kuwa ni myaruanda...



Na ndio hapo watusi wengi walijiunga na Museveni ili kumtoa Obote.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…