Omulasil
JF-Expert Member
- May 5, 2015
- 8,015
- 10,269
Nimesema hakuna mifumo imekuwepo ya maana niambie nani aliiondoa?Enzi zao kulikuwa na mifumo thabiti ya kutatua matatizo ya wanaichi.Wakuu wa wilaya na Mikoa walikuwa na muda wa kushughulikia matatizo ya watu.Hivi Sasa muda wa kuwepo ofisini hawana tokana na mfumo ulivyo.Inaonyesha wewe haukuwepo zama hizo ndiyo maana unamtukana Mzee huyu.
Awamu ya kwanza ilipinga unyojaji lkn wezi walikuwa wanaua shitika moja na wanaenda lingine.
Awamu ya pili miiko ya uongozi iliuza mali na mashirika ya umma kwa bei za kutupa kwa lugha ya restucturing NBC CRDB ni benki za mfano wakimaliza wanaanzisha benki nyingine.
Ilifuata ndio kabisa miiko ya uongozi ikatupwa viongozi hao hao ndio wafanya biashara na kila aina ya upotevu. List inaenda hivyo hivyo kwa miaka yote ya uhuru. Ufisadi na rushwa hazijawahi kumuacha mtu maskini na haki. Ndio maana anapotokea mtu hata iwe kwa maigizo kuwa anatatua kero watu humuendea.
Kifupi unavyoona watu wanaenda kutafuta suluhu itoshe kusema haki haijawahi kutendeka. Sasa mzee atulie ale keki