Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
- Thread starter
- #21
Hawawezi kujifunza kitu maana ni wabinafsi sana.wana umimi sana. Ni watu wanaojali matumbo yao tu.chadema wanachakujifunza walah
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hawawezi kujifunza kitu maana ni wabinafsi sana.wana umimi sana. Ni watu wanaojali matumbo yao tu.chadema wanachakujifunza walah
Linganisha misaada ya Chadema na Ccm, ndipo utapata jibuHuyu mleta mada kumbe ni mke wa pili wa Prof J,maana anadai kwamba Cdm hawajatoa msaada wowote.
Na ni matapeliNa wala hana hata dalili ya kutoa na kutimiza ahadi yake. CHADEMA na viongozi wake ni watu wabinafsi sana .
Chadema kumejaa matapeliLissu na kelele zake million 2 tena y ahadi mpaka Leo apokei simu😆😆😆😂
Wao CHADEMA watakujali na kukuchekelea wakiona unawapatia vijisenti lakini ukipatwa na matatizo wanakuruka kama mwewe aliyenyakua kifaranga.Kwahiyo watoa taarifa wao huwa wako pamoja katika raha tu, ila kwenye shida kila mtu na njia yake.
jamaa wanakula ruzuku mpaka tone la mwisho hovyo kabisaNdo ujue kuwa ccm ni mume wa vyama vyote hasa hiyo chadema, ukiangalia michango ya wanachadema wenzake na wanaccm ni tofauti kabisa
CC Erythrocyte
CHADEMA wamechangia nini ulichokiona? Tangia lini CHADEMA ikaguswa na shida za watu? Tangia lini CHADEMA ikawa na huruma na wenye kuhitaji msaada?Huyu mleta mada kumbe ni mke wa pili wa Prof J,maana anadai kwamba Cdm hawajatoa msaada wowote.
Acheni porojo ninyi CHADEMA mmeshindwa kumsaidia prof Jay Lakini mnaumia ,kuona wivu,kuwa na chuki binafsi pale mnapoona wenye mioyo ya upendo na huruma wakitoa misaada kwa wingi kwa prof Jay ,ambaye ninyi mmemtelekeza na kuona hana thamani tena kwenu. Ninyi. Hamna utu wala upendo wala ubinadamu. Ninyi ni wabinafsi sana CHADEMA.ni watu wa ajabu sana ninyi.
Unatwambia ili iweje? Ulitaka upewe wewe? , kama hiyo fedha imetolewa kweli ni kodi yako au ni zao la ukora alioufanya tangu enzi ya JPM.Ndugu zangu Watanzania,
Mheshimiwa Paul Makonda Katibu wa itikadi na uenezi wa CCM Taifa leo ametimiza ahadi yake ya kumpatia prof Jay million 20 kwa ajili ya Taasisi yake ya prof Jay Foundation,Ambayo imeamua kutafuta na kukusanya pesa kwa kuwashirikisha na kuwaomba watanzania kwa ajili ya kuwasaidia watu wenye matatizo ya Figo.
Lakini pia Mheshimiwa Makonda ametoa ahadi nzito iliyo Gusa moyo wa prof Jay na kumpa tabasamu na furaha katika moyo wake ,baada ya mheshimiwa Makonda kumwambia kuwa atamtafutia nyumba maeneo ya upanga ili iwe rahisi na kumpunguzia safari au umbali mrefu prof Jay wa kufika hospitalini kwa ajili ya uchunguzi zaidi na matibabu mbalimbali kulingana na namna alivyopangiwa na madaktari wake.
Hatua hii na ahadi hii imekuwa ni kama nuru katikati ya Giza, Tumaini katikati ya kukata Tamaa na faraja katikati ya huzuni. Mh Paul Makonda ambaye ni mpambanaji na jasiri aliyepindukia na asiye ogopa kuwapigania wanyonge amewataka wale wote waliotoa ahadi zao wahakikishe kuwa wanatimiza ahadi hizo.
Wakati haya yakifanywa na Mheshimiwa Makonda pamoja na CCM na Serikali yake kwa ujumla hali imekuwa ya kusikitishaa ,kuumiza ,kutia hasira ,kuleta maswali kwa chama cha prof Jay yaani CHADEMA chama ambacho amekuwa mbunge wake kwa miaka mitano mfululizo.watu wanashangaa na kusikitika kwa namna chama kilivyo mtelekeza mwanachama wake na mbunge wake wa zamani .hakina msaada kwake wala kumpa faraja wala nguvu wala kumtia moyo walau hata kuweka hata harambee ya siku moja kwa ajili ya kumchangia katika taasisi yake, zaidi ya kutoa ahadi ambazo mpaka leo hii wahusika walishajikausha kama majani yaliyopigwa na jua.
Hii ni kutokana na ukweli kuwa CHADEMA itakujali na kukupenda kinafiki pale itakapoona unaiingizia Ruzuku na kuipa michango kutunisha mfuko kwa ajili ya viongozi wake kuzitafuna. Jiulize prof Jay ambaye alikuwa anakipa chama Ruzuku kupitia ubunge wake,kukatwa pesa kila mwezi kwa ajili ya CHADEMA lakini leo huoni mchango wala msaada wa aina yoyote ile kutoka kwa chama. Leo prof Jay ameachwa na chama chake ili ajipambanie mwenyewe na Mungu wake. Hivi prof Jay Ndio wakufanyiwa haya na CHADEMA kweli? Ndio wakutelekezwa na chama kweli?
Kama wameutendea hivi mti mbichi vipi kwa mti mkavu? Vipi kwa wale wasio na majina? Hivi mliopo huko CHADEMA mnasubiri nini huko? Hamuoni chama hakina habari na nyie mkipatwa na matatizo? Hamuoni kinawatelekeza? Humuoni thamani yenu inakoma pale mnapoacha kukipa chama Ruzuku na michango?
Sasa leo msaada wa prof Jay unatoka na kupewa na CCM na Wana CCM na Serikali yake kwa ujumla wake.leo CCM Ndio yenye uchungu mkubwa na prof Jay na kumpatia faraja na tabasamu.leo CCM na Serikali yake ndio inayomshika mkono na kuwa karibu naye na inayoendelea kupambana kwa hali na mali na kwa uweza wa Mwenyezi Mungu ili prof Jay Aendelea kuimarika kiafya kila uchwao kwa msaada wa Mwenyezi Mungu. Huku wao CHADEMA wakiwa Bize kutafuta michango ili wapige na kutafuna kama walivyofanya kwenye pesa za join the chain ambazo mpaka leo hii ni kiza kinene juu ya pesa hizo.
Namuomba Mungu aendelee kumsaidia Prof Jay katika yote apitiayo,Amjalie nguvu na moyo wa kuendelea kugusa maisha ya watanzania wengine wenye uhitaji wa matibabu ya Figo kupitia taasisi yake hiyo.
Hongera sana Mheshimiwa Makonda kwa moyo wako wa jua wa kuwapa watu matumaini, furaha, faraja na tabasamu katika nyuso zao.ndio maana Mungu amekuwa akikuinua katika namna ya kipekee kabisa.watu wakikutangazia mwisho lakini wanashangaa Mungu wako anautangaza mwanzo wako kwa kishindo .wakikutangazia kushindwa Mungu wako anakuweka katika kilele cha ushindi.
wewe ni mshindi kwa kuwa Mungu amekuwa upande wako muda wote. Mungu anasema ukiwasaidia maskini na wenye shida unakuwa unamkopesha Mungu mwenyewe na atakulipa kwa mema makubwa .Mungu Anaendelea kukulipa mema mengi kwa kuwa umegusa mioyo ya wengi na kuipa tabasamu.umesaidia wenye matatizo ya moyo wakapata tumaini na tabasamu katika nyuso na mioyo yao.
ndio maana Mungu hakuachi uwapo vitani. Hakuachi maadui wakuzingilapo na wakushambulia.ndio maana amekuwa akikupatia ushindi wakati wote na kuwaduwaza maadui zako ambao wanakuwa wanahisi wamekumaliza na huwezi kuinuka tena.lakini wanashangaa ukiibukia mbele yao kishujaa.
Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
0742-676627.
Wewe inajulikana humu kuwa una chuki binafsi na mheshimiwa Makonda. wewe ndio wale mliomtangazia mwisho lakini Mungu akautangaza Mwanzo wake wa ushindi.ninyi ndio mliojisemea mioyoni mwenu kuwa mmemumaliza na kwamba hawezi kuinuka tena lakini mkaduwaa kuona akiinukia na kuibukia mbele yenu kishujaa na kijasiri akiwa na kibali cha baraka za Mungu mkononi mwake.usishindane na aliye barikiwa na kuwa na Mungu ndani yake. Mungu siyo mwanadamu kama wewe .Makonda asije akampa prof. Jay nyumba aliyoipora toka GSM
Kama unamfahamu mwingine hata wewe ni mwanadamu unaweza kumsaidia na kuwaomba wengine pia wakuunge mkono umsaidie huyo mtu.Aise,huyu ndiyo mgonjwa wa kwanza kupata matatizo ya Figo
Ova
Utakufa na wivu wako na chuki zako binafsi.usishindane na aliye barikiwa na Mungu. Mh Paul Makonda amebarikiwa na Mungu kwa kuwa amekuwa anagusa maisha ya wengi kwa kuwasaidia kwa hali na mali. Wakati mtu kama wewe huna msaada wowote ule hapa Duniani zaidi ya mitusi yako tu kama kichaa au mwendawazimu.Unatwambia ili iweje? Ulitaka upewe wewe? , kama hiyo fedha imetolewa kweli ni kodi yako au ni zao la ukora alioufanya tangu enzi ya JPM.
Wivu tu ndio unaokusumbua wewe.Kuna Watu wana Fedha Zao hawataki sifa hivyo wanawaachia nyinyi mkijitangaza wakati wao wamemsaidia Prof. Jay na foundation yake kwa sharti la kutotangazwa!
Acha uongo wako wewe.najuwa ni wivu na chuki tu ndio vinakusumbua moyoni mwako.Ametoa yeye au ccm? Kama ni yeye basi ni zile hela alizokuwa anaibia watu akiwa RC.
Hiyo nyumba prof ajitafakari vizuri, labda apewe na hati miliki. Prof alikuwa na nyumba kimara, jpm na makonda wakaivunja, tena ya thamani kubwa