Paul Makonda amkabidhi Prof Jay millioni 20 ,Atoa ahadi nzitoo ya kumtafutia nyumba upanga ili kuwa karibu na hospitali.

Ndugu zangu Watanzania,

Mheshimiwa Paul Makonda Katibu wa itikadi na uenezi wa CCM Taifa leo ametimiza ahadi yake ya kumpatia prof Jay million 20 kwa ajili ya Taasisi yake ya prof Jay Foundation,Ambayo imeamua kutafuta na kukusanya pesa kwa kuwashirikisha na kuwaomba watanzania kwa ajili ya kuwasaidia watu wenye matatizo ya Figo.

Lakini pia Mheshimiwa Makonda ametoa ahadi nzito iliyo Gusa moyo wa prof Jay na kumpa tabasamu na furaha katika moyo wake ,baada ya mheshimiwa Makonda kumwambia kuwa atamtafutia nyumba maeneo ya upanga ili iwe rahisi na kumpunguzia safari au umbali mrefu prof Jay wa kufika hospitalini kwa ajili ya uchunguzi zaidi na matibabu mbalimbali kulingana na namna alivyopangiwa na madaktari wake.

Hatua hii na ahadi hii imekuwa ni kama nuru katikati ya Giza, Tumaini katikati ya kukata Tamaa na faraja katikati ya huzuni. Mh Paul Makonda ambaye ni mpambanaji na jasiri aliyepindukia na asiye ogopa kuwapigania wanyonge amewataka wale wote waliotoa ahadi zao wahakikishe kuwa wanatimiza ahadi hizo.

Wakati haya yakifanywa na Mheshimiwa Makonda pamoja na CCM na Serikali yake kwa ujumla hali imekuwa ya kusikitishaa ,kuumiza ,kutia hasira ,kuleta maswali kwa chama cha prof Jay yaani CHADEMA chama ambacho amekuwa mbunge wake kwa miaka mitano mfululizo.watu wanashangaa na kusikitika kwa namna chama kilivyo mtelekeza mwanachama wake na mbunge wake wa zamani .hakina msaada kwake wala kumpa faraja wala nguvu wala kumtia moyo walau hata kuweka hata harambee ya siku moja kwa ajili ya kumchangia katika taasisi yake, zaidi ya kutoa ahadi ambazo mpaka leo hii wahusika walishajikausha kama majani yaliyopigwa na jua.

Hii ni kutokana na ukweli kuwa CHADEMA itakujali na kukupenda kinafiki pale itakapoona unaiingizia Ruzuku na kuipa michango kutunisha mfuko kwa ajili ya viongozi wake kuzitafuna. Jiulize prof Jay ambaye alikuwa anakipa chama Ruzuku kupitia ubunge wake,kukatwa pesa kila mwezi kwa ajili ya CHADEMA lakini leo huoni mchango wala msaada wa aina yoyote ile kutoka kwa chama. Leo prof Jay ameachwa na chama chake ili ajipambanie mwenyewe na Mungu wake. Hivi prof Jay Ndio wakufanyiwa haya na CHADEMA kweli? Ndio wakutelekezwa na chama kweli?

Kama wameutendea hivi mti mbichi vipi kwa mti mkavu? Vipi kwa wale wasio na majina? Hivi mliopo huko CHADEMA mnasubiri nini huko? Hamuoni chama hakina habari na nyie mkipatwa na matatizo? Hamuoni kinawatelekeza? Humuoni thamani yenu inakoma pale mnapoacha kukipa chama Ruzuku na michango?

Sasa leo msaada wa prof Jay unatoka na kupewa na CCM na Wana CCM na Serikali yake kwa ujumla wake.leo CCM Ndio yenye uchungu mkubwa na prof Jay na kumpatia faraja na tabasamu.leo CCM na Serikali yake ndio inayomshika mkono na kuwa karibu naye na inayoendelea kupambana kwa hali na mali na kwa uweza wa Mwenyezi Mungu ili prof Jay Aendelea kuimarika kiafya kila uchwao kwa msaada wa Mwenyezi Mungu. Huku wao CHADEMA wakiwa Bize kutafuta michango ili wapige na kutafuna kama walivyofanya kwenye pesa za join the chain ambazo mpaka leo hii ni kiza kinene juu ya pesa hizo.

Namuomba Mungu aendelee kumsaidia Prof Jay katika yote apitiayo,Amjalie nguvu na moyo wa kuendelea kugusa maisha ya watanzania wengine wenye uhitaji wa matibabu ya Figo kupitia taasisi yake hiyo.

Hongera sana Mheshimiwa Makonda kwa moyo wako wa jua wa kuwapa watu matumaini, furaha, faraja na tabasamu katika nyuso zao.ndio maana Mungu amekuwa akikuinua katika namna ya kipekee kabisa.watu wakikutangazia mwisho lakini wanashangaa Mungu wako anautangaza mwanzo wako kwa kishindo .wakikutangazia kushindwa Mungu wako anakuweka katika kilele cha ushindi.

wewe ni mshindi kwa kuwa Mungu amekuwa upande wako muda wote. Mungu anasema ukiwasaidia maskini na wenye shida unakuwa unamkopesha Mungu mwenyewe na atakulipa kwa mema makubwa .Mungu Anaendelea kukulipa mema mengi kwa kuwa umegusa mioyo ya wengi na kuipa tabasamu.umesaidia wenye matatizo ya moyo wakapata tumaini na tabasamu katika nyuso na mioyo yao.

ndio maana Mungu hakuachi uwapo vitani. Hakuachi maadui wakuzingilapo na wakushambulia.ndio maana amekuwa akikupatia ushindi wakati wote na kuwaduwaza maadui zako ambao wanakuwa wanahisi wamekumaliza na huwezi kuinuka tena.lakini wanashangaa ukiibukia mbele yao kishujaa.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
Hongera Makonda kwa kumpigania mnyonge prof J ambae ni msanii maarufu na mbunge mstaafu
 
Wewe inajulikana humu kuwa una chuki binafsi na mheshimiwa Makonda. wewe ndio wale mliomtangazia mwisho lakini Mungu akautangaza Mwanzo wake wa ushindi.ninyi ndio mliojisemea mioyoni mwenu kuwa mmemumaliza na kwamba hawezi kuinuka tena lakini mkaduwaa kuona akiinukia na kuibukia mbele yenu kishujaa na kijasiri akiwa na kibali cha baraka za Mungu mkononi mwake.usishindane na aliye barikiwa na kuwa na Mungu ndani yake. Mungu siyo mwanadamu kama wewe .
Mmhh! Kama Makonda ana Mungu basi huyo "mungu" atakuwa siyo yule anayebainishwa na vitabu vya dini.
 
Ndio maana nikasema kuwa Mungu siyo mwanadamu na wala hana mawazo ya kibinadamu wala kuwa na chuki binafsi kama ilivyo kwa mwanadamu.
 
Asante kwa taarifa Mrs Joseph Haule na hongera kwa kumsemea mmeo.
Ndugu zangu Watanzania,

Mheshimiwa Paul Makonda Katibu wa itikadi na uenezi wa CCM Taifa leo ametimiza ahadi yake ya kumpatia prof Jay million 20 kwa ajili ya Taasisi yake ya prof Jay Foundation,Ambayo imeamua kutafuta na kukusanya pesa kwa kuwashirikisha na kuwaomba watanzania kwa ajili ya kuwasaidia watu wenye matatizo ya Figo.

Lakini pia Mheshimiwa Makonda ametoa ahadi nzito iliyo Gusa moyo wa prof Jay na kumpa tabasamu na furaha katika moyo wake ,baada ya mheshimiwa Makonda kumwambia kuwa atamtafutia nyumba maeneo ya upanga ili iwe rahisi na kumpunguzia safari au umbali mrefu prof Jay wa kufika hospitalini kwa ajili ya uchunguzi zaidi na matibabu mbalimbali kulingana na namna alivyopangiwa na madaktari wake.

Hatua hii na ahadi hii imekuwa ni kama nuru katikati ya Giza, Tumaini katikati ya kukata Tamaa na faraja katikati ya huzuni. Mh Paul Makonda ambaye ni mpambanaji na jasiri aliyepindukia na asiye ogopa kuwapigania wanyonge amewataka wale wote waliotoa ahadi zao wahakikishe kuwa wanatimiza ahadi hizo.

Wakati haya yakifanywa na Mheshimiwa Makonda pamoja na CCM na Serikali yake kwa ujumla hali imekuwa ya kusikitishaa ,kuumiza ,kutia hasira ,kuleta maswali kwa chama cha prof Jay yaani CHADEMA chama ambacho amekuwa mbunge wake kwa miaka mitano mfululizo.watu wanashangaa na kusikitika kwa namna chama kilivyo mtelekeza mwanachama wake na mbunge wake wa zamani .hakina msaada kwake wala kumpa faraja wala nguvu wala kumtia moyo walau hata kuweka hata harambee ya siku moja kwa ajili ya kumchangia katika taasisi yake, zaidi ya kutoa ahadi ambazo mpaka leo hii wahusika walishajikausha kama majani yaliyopigwa na jua.

Hii ni kutokana na ukweli kuwa CHADEMA itakujali na kukupenda kinafiki pale itakapoona unaiingizia Ruzuku na kuipa michango kutunisha mfuko kwa ajili ya viongozi wake kuzitafuna. Jiulize prof Jay ambaye alikuwa anakipa chama Ruzuku kupitia ubunge wake,kukatwa pesa kila mwezi kwa ajili ya CHADEMA lakini leo huoni mchango wala msaada wa aina yoyote ile kutoka kwa chama. Leo prof Jay ameachwa na chama chake ili ajipambanie mwenyewe na Mungu wake. Hivi prof Jay Ndio wakufanyiwa haya na CHADEMA kweli? Ndio wakutelekezwa na chama kweli?

Kama wameutendea hivi mti mbichi vipi kwa mti mkavu? Vipi kwa wale wasio na majina? Hivi mliopo huko CHADEMA mnasubiri nini huko? Hamuoni chama hakina habari na nyie mkipatwa na matatizo? Hamuoni kinawatelekeza? Humuoni thamani yenu inakoma pale mnapoacha kukipa chama Ruzuku na michango?

Sasa leo msaada wa prof Jay unatoka na kupewa na CCM na Wana CCM na Serikali yake kwa ujumla wake.leo CCM Ndio yenye uchungu mkubwa na prof Jay na kumpatia faraja na tabasamu.leo CCM na Serikali yake ndio inayomshika mkono na kuwa karibu naye na inayoendelea kupambana kwa hali na mali na kwa uweza wa Mwenyezi Mungu ili prof Jay Aendelea kuimarika kiafya kila uchwao kwa msaada wa Mwenyezi Mungu. Huku wao CHADEMA wakiwa Bize kutafuta michango ili wapige na kutafuna kama walivyofanya kwenye pesa za join the chain ambazo mpaka leo hii ni kiza kinene juu ya pesa hizo.

Namuomba Mungu aendelee kumsaidia Prof Jay katika yote apitiayo,Amjalie nguvu na moyo wa kuendelea kugusa maisha ya watanzania wengine wenye uhitaji wa matibabu ya Figo kupitia taasisi yake hiyo.

Hongera sana Mheshimiwa Makonda kwa moyo wako wa jua wa kuwapa watu matumaini, furaha, faraja na tabasamu katika nyuso zao.ndio maana Mungu amekuwa akikuinua katika namna ya kipekee kabisa.watu wakikutangazia mwisho lakini wanashangaa Mungu wako anautangaza mwanzo wako kwa kishindo .wakikutangazia kushindwa Mungu wako anakuweka katika kilele cha ushindi.

wewe ni mshindi kwa kuwa Mungu amekuwa upande wako muda wote. Mungu anasema ukiwasaidia maskini na wenye shida unakuwa unamkopesha Mungu mwenyewe na atakulipa kwa mema makubwa .Mungu Anaendelea kukulipa mema mengi kwa kuwa umegusa mioyo ya wengi na kuipa tabasamu.umesaidia wenye matatizo ya moyo wakapata tumaini na tabasamu katika nyuso na mioyo yao.

ndio maana Mungu hakuachi uwapo vitani. Hakuachi maadui wakuzingilapo na wakushambulia.ndio maana amekuwa akikupatia ushindi wakati wote na kuwaduwaza maadui zako ambao wanakuwa wanahisi wamekumaliza na huwezi kuinuka tena.lakini wanashangaa ukiibukia mbele yao kishujaa.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
TMy
 
Wivu gani wewe chawa; kumsaidia mtu mwenye shida sio sifa bali ni wajibu wa binadamu mwenye hekima!
Sasa mbona hekima hizo hazipo ndani ya CHADEMA? Mbona moyo huo wa kusaidia huukuti ndani ya mioyo ya viongozi wa CHADEMA? Mbona hisia hizo za huruma huwezi kuziona ndani ya vifua na nyuso za wana CHADEMA zaidi ya janja janja tu?
 
Kuna mambo yasisyoelezeka kwa lugha nyingine ya kistaraabu au heshima, ni ya kuyaita kama yalivyo ''upumbavu'. Kuna watu kwa kukosa utu wanamgeuza Prof kama mtaji wa siasa. Huu kama si upuuzi nielimishwe ni kitu gani

Kama aliahidi na ametoa hiyo inahusu nini wanajamii! Kinachofanyika hapa ni kutumia maradhi kujieneza.

Nadhani wewe ni mmoja wa 'chawa' wake lakini uchawa hadi katika maradhi ni kukosa moral compass , na ni mora decay . Hivi tumefika mahali hatujali maisha ya watu tunatumia matatizo katika siasa.

Jiulize,unayesema nI mwema, mikono yake ni misafi?
Kila siku ana nyooshewa vidole kwa madhila , dhambi na damu za watu, leo unataka kutuambia nini!

Hivi ni Watanzania wangapi wenye matatizo kama ya Prof.

Kwanini hatujamuona akienda kusaidia watu kutoka Vijini mikoani wasio na mahali pa kulala pale muhimbili. Watu wanaolala katika korido za Hospitali. Acheni uhayawani huu! Ugonjwa ni tatizo si ngazi kisiasa. Acheni ! acheni upuuzi

Hizi taarifa umepewa na nani? Familia ya Prof Jay au unatunga!
Acheni kutumia matatizo na maradhi kufanya siasa majitaka, ni upuuz jisikie aibu kufanya uhayawani huu.

Ruzuku inaingia vipi katika maradhi?
Huu ni uhayawani tusiufumbie macho, hawa watu wakiwa wengi hatuna Taifa. Nchi imejaa watu wa ajabu

Soma upuuzi huu! rudia kusoma halafu ufanye tathmini ya akili yako, kisha umuombe mwenezi msaada wa matibabu. Tumedharau mabandiko yako lakini sasa tunaamini sis wewe peke yako, unatumwa !

Wakati unatoa mrejesho, muulize nini kilikuwa kinatokea Coco Beach! Alimpata wapi ROMA, akina Ben na Azory wapo wapi, na misheni ya Dodoma kwanini ilifeli. Haya ndiyo wanauliza Watanzania.
Povu likizidi kanye boga
 
Lissu na kelele zake million 2 tena y ahadi mpaka Leo apokei simu😆😆😆😂
Hahaha kazi kubwabwaja tu!Na Lema mwizi wa magari hajatimiza ahadi
Wao CHADEMA watakujali na kukuchekelea wakiona unawapatia vijisenti lakini ukipatwa na matatizo wanakuruka kama mwewe aliyenyakua kifaranga.
Unakumbuka kipindi cha ajali ya MV Nyerere Ukerewe wote walipotezea ikabidi mbunge wa Ukerewe ahame! Wabinafsi na wana Ukabila na ukanda sana!
 
Hahaha kazi kubwabwaja tu!Na Lema mwizi wa magari hajatimiza ahadi

Unakumbuka kipindi cha ajali ya MV Nyerere Ukerewe wote walipotezea ikabidi mbunge wa Ukerewe ahame! Wabinafsi na wana Ukabila na ukanda sana!
CHADEMA ina laana kubwa sana inayoiandama .ndio maana kwa sasa ni kama wanajenga mnara wa babeli.kila mtu na lugha yake .
 
Makonda hana shida na kupora nyumba ya GSM yeye mwenyewe ana majumba tena Sehemu za Maana kama Masaki Dar,Capri point Mwanza na kingamboni ndo usiseme!
Kwa kifupi jamaa hana njaa!
Achana na huyo mwenye moyo wa wivu,chuki na roho mbaya.
 
Asante kwa taarifa Mrs Joseph Haule na hongera kwa kumsemea mmeo.

TMy
Acha dharau ndugu yangu .tangia lini mwanaume akawa mrs? Hata kama una chuki na mimi basi jaribu kuwa na heshima au kuheshimu utu wa mtu na siyo kuandika kwa lugha za dhihaka na kudhalilishana.
 
Acheni porojo ninyi CHADEMA mmeshindwa kumsaidia prof Jay Lakini mnaumia ,kuona wivu,kuwa na chuki binafsi pale mnapoona wenye mioyo ya upendo na huruma wakitoa misaada kwa wingi kwa prof Jay ,ambaye ninyi mmemtelekeza na kuona hana thamani tena kwenu. Ninyi. Hamna utu wala upendo wala ubinadamu. Ninyi ni wabinafsi sana CHADEMA.ni watu wa ajabu sana ninyi.

Ni hivi, msitumie matatizo ya mtu kujisafisha au kupanda ngazi za siasa. Huo si tu ni uhuni bali ujinga na upumbavu.

Mngalikuwa mnajali mungemuuliza huyo 'Boss' wenu, nini kilitokea Cocoa Beach. Vile Viroba mto Ruvu, wale waliopotea na kwanini alikwenda Dodoma siku ile.
Wiki hii kuna nyuzi nyingi za kumtukuza, tunajua ! kinachotusukuma kusema hapa ni udhalili wa kutumia maumivu ya mtu kujitangaza.

Hili lipo chini ya kiwango, acheni haya mambo ya njaa. Kuna mambo mengi ya kitaifa na ya muhimu kwa umma kuliko kueneza uchawa.
 
Back
Top Bottom