Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Paul Makonda akiwa kwenye mkutano jijini Arusha ameongelea mambo kadhaa ikiwemo kumkumbuka Rais wa awamu ya tano, Hayati John Magufuli jinsi alivyokuwa makini na mkali inapofika suala la uongozi.
Paul Makonda: Ametoa takwimu hapo Ngorongoro girls watoto wanashindwa kuendelea na masomo, yaani kweli katika kipindi hiki Rais Samia amejenha na madarasa.
Mimi nakumbuka mwamba yule anasema sitaki kusikia watoto wanakaa chini kamaliza mjadala, chuma hicho. Yaani Mkuu wa Mkoa eeh, Mkuu wa Wilaya watoto wanakaa chini! Halafu wewe upo, aah tutapimana tuone!
Hapo utatafuta mwenyewe mbinu yako, mimi nilikuja na mambinu kibao, nimetengeneza madawati karibia laki tatu, tumejenga maofisi ya walimu na nini!
Mama kaleta fedha za kujenga madarasa yenye kila kitu na elimu ni bure halafu eti watoto wanaharibika. Sasa badala ya kuitumia hiyo fursa kwamba tulikuwa hatuipati, watoto ndio wanazidi kuharibika.
Bahati mbaya kuna mambo mengine huwezi kuyajadili, ukiyajadili zitaingia siasa, zikiingia siasa maana yake inapotoshwa. Tumekubali kuondoa fimbo shuleni, sawa! Lakini ndio zimetukuza sisi tumefika hapa tulipo, nidhamu tuliyonayo.
Mwalimu anapokosa namna ya kum-discipline mtoto anamuacha aende anavyotaka na mtoto akienda anavyotaka, mama sasahivi kila mtu yuko busy anatafuta pesa.
Sasa hivi Familia hazitengenezi tena mume wala mke, familia ziko busy kutengeneza mchumi, mhasibu, mwanasheria, injinia. Sasa akija kwenye familia, mtoto analelewa na housegirl, na sisi wazazi tuna jukumu la kufanya.