Paul Makonda anakwenda kulifanya Jiji la Arusha kuwa maarufu kuipita Washington DC Marekani au Dubai


Mambo mengine uwe unakaa kimya Tu

Ameshindwa kuwa mwenezi Bora atakuwa mkuu wa mkoa Bora?

Huko Arusha hatomaliza hata huu mwaka
 
Kaa kwa kutulia ndugu yangu uone nini kinakwenda kutokea chini ya uongozi wa Mheshimiwa Makonda
Mkuu
Kaa kwa kutulia ndugu yangu uone nini kinakwenda kutokea chini ya uongozi wa Mheshimiwa Makonda
Sawa lakini siamini katika hawa wanasiasa wasaka vyeo, naamini katika watu ambao ni watendaji, huyu hadi JPM alisema vijana wa miaka ya 1980s wana tamaa,
 
Nisiwe na maneno mengi.
Mimi kuandika risala refu sipendi kabisa.
Makonda Paul Christian kapandishwa hadhi, wadhifa.
Kamishna wa mkoa ni cheo kikubwa na chenye hadhi zaidi kuliko Ukatibu wa kueneza chama.
Cheo cha Katibu mwenezi wa chama ni cheo kidogo tu na mandate yake yanaishia kwenye chama.
Ki protocol Katibu mwenezi wa chama yuko chini ya Katibu mkuu wa chama.
Sasa mtu kapandishwa cheo ( kaingizwa kwenye mfumo wa serikali ) kutoka kwenye chama munasemaje kuwa katumbuliwa?
Kwa aina hii ya Watanzania maendeleo bado sana.
Itachukua miaka zaidi ya mia moja kuondoa umaskini , ujinga na upumbavu miongoni mwa Watanzania.
 
Hadhi ya konyo, mwanzoni alikuwa anazurura nchi nzima, sasa hivi ana kamkoa tu
 
Ila kweli mkuu wa mkoa ni mkuu wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa ni boss wa mkoa ila mwenezi hawezi kumuamrisha hata mgambo
 
Lucas sijui kama umewahi kutoka nje ya Tanzania, pengine hata tuseme nje ya Afrika kutokana na kujilipua hapa jukwaani na kutaka kufanya mlinganisho wa jiji la Arusha na majiji hayo mawili ambayo ni maarufu sana hapa duniani.
 
Si amewatukana mawaziri wote mpaka waziri mkuu, ngoja tuone kama ana nguzo ya kuegemea
Ame upgrade kwa sasa anapaa nguzo hazihitajiki.......kama mlidhani hii shoo anapiga 1 man army nyie vilaza
 
Huu sio uchawa tena huu ni ujinga
 
Hadhi ya konyo, mwanzoni alikuwa anazurura nchi nzima, sasa hivi ana kamkoa tu
Subiri tu utaona kwanini Mheshimiwa kapelekwa pale. Huyo ndiye meneja Kampeni wa Mheshimiwa Rais mwakani na baadaye anaingia Bungeni na kupewa nafasi nyeti kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…