Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Wakuu,
Makonda ameendelea kutoa spana huko Arusha baada ya kusema kuwa wakazi wa mkoa wa Arusha kwa muda mrefu kwa sababu walikuwa wanaendekeza majungu, ushirikina na siasa uchwara.
Kauli hii inakuja baada ya Waziri wa TAMISEMI kufanya ziara mkoani hapo leo October 4.2024 na ndipo mkuu huyo wa mkoa alidokeza kuwa kwa sababu Arusha ilikuwa inaendekeza majungu na ushirikina pamoja na siasa uchwara kwa muda mrefu ndio maana barabara zimechelewa kujengwa.
"Na kwa kweli Arusha hawakupata barabara nyingi kwa muda mrefu kwa sababu waliendekeza majungu, ushirikina na siasa uchwara. Yaani huko ndio walipokuwa wamebobe. Ni wazee wa shoti."
"Yaani unaweza ukawa umeomba kama hapa jambo tumeliomba kwako, tukichelewa anaweza akazunguka mtu uko ukashangaa barabara inaanza tena kubadilishwa badilishwa."
Huu ni muendelezo wa kauli tata na kandamizi kutoka kwa kauli hiyo ya mkuu wa mkoa!