Pre GE2025 Paul Makonda: Arusha hawakupata barabara kwa muda mrefu kwa sababu waliendekeza majungu, ushirikina na siasa uchwara!

Pre GE2025 Paul Makonda: Arusha hawakupata barabara kwa muda mrefu kwa sababu waliendekeza majungu, ushirikina na siasa uchwara!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kwahiyo majungu na kuzunguukana kwa wana-R-chuga kuna nguvu zaidi ya
Sera, Mipango, Nia na Utashi wa Wakubwa?
Haijanibamba vizuri hii.
Au ugonjwa wangu wa kutokuelewa umenirudia?
 
Ha
Wakuu,

Makonda ameendelea kutoa spana huko Arusha baada ya kusema kuwa wakazi wa mkoa wa Arusha kwa muda mrefu kwa sababu walikuwa wanaendekeza majungu, ushirikina na siasa uchwara.

Kauli hii inakuja baada ya Waziri wa TAMISEMI kufanya ziara mkoani hapo leo October 4.2024 na ndipo mkuu huyo wa mkoa alidokeza kuwa kwa sababu Arusha ilikuwa inaendekeza majungu na ushirikina pamoja na siasa uchwara kwa muda mrefu ndio maana barabara zimechelewa kujengwa.

"Na kwa kweli Arusha hawakupata barabara nyingi kwa muda mrefu kwa sababu waliendekeza majungu, ushirikina na siasa uchwara. Yaani huko ndio walipokuwa wamebobe. Ni wazee wa shoti."

"Yaani unaweza ukawa umeomba kama hapa jambo tumeliomba kwako, tukichelewa anaweza akazunguka mtu uko ukashangaa barabara inaanza tena kubadilishwa badilishwa."

Huu ni muendelezo wa kauli tata na kandamizi kutoka kwa kauli hiyo ya mkuu wa mkoa!

a Makonda..kweli ni jasiri. Ni kweli Kuna mtu wanasemaga anacheleweshaga miradi Hadi Leo hamna stendi
 
Angekaa kimya tu kuficha ujinga wake.
 
Hivi hujui kuwa huyu chizi hadi alipewe jina la nabiii 🙆‍♂️🙆‍♂️🙆‍

Kama hajengi Barabara, kwenye kampeni Huwa ananadi sera zipi?

Kama CCM inapeleka maendeleo kwenye maeneo waliposhinda tu then kwanini serikali inakusanya kodi kwa wananchi wa vyama vyote?

Ccm kwanini inachukua kodi kwa Wanachadema na vyama vingine?
 
Pelekeni shida zenu Chadema sio CCM
Na sisi tusiwaone na yale manguo yenu ya TRA mnataka kodi kwenye maduka yote.

PAYE kateni kwa wanachama wa CCM tu, CHADEMA na vyama vingine msiguse.

Kodi mnachukua kutoka kwa wananchi wa vyama vyote lakini maendeleo mnapeleka sehemu mnazojisikia nyie.

Ccm akili zenu mnazijua wenyewe!
 
Ndio maana nikasema ulitaka kufanya hivyo kwenye maendeleo uwe chama kimoja. Ukiwa vyama vingi peleka maendeleo kote na sio kwa chama chako tu. Ukifanya hivyo unavunja katiba .
Naongezea hapo.

Kodi pia wawe wanawatoza wanaCCM tu, wanaCHADEMA na vyama vingine wasitozwe maana hawaletewi maendeleo.

It's a simple math.
 
Na sisi tusiwaone na yale manguo yenu ya TRA mnataka kodi kwenye maduka yote.

PAYE kateni kwa wanachama wa CCM tu, CHADEMA na vyama vingine msiguse.

Kodi mnachukua kutoka kwa wananchi wa vyama vyote lakini maendeleo mnapeleka sehemu mnazojisikia nyie.

Ccm akili zenu mnazijua wenyewe!
Kodi tutakusanya Kwa sababu sie ndio tumepewa ridhaa ya kuunda Serikali.

Tutatumia kwenye vipaombele vya ilani yetu sio Chadema 😆😆

Jtakula.ulikopeleka mboga.
 
Back
Top Bottom